Kumeibuka chapisho la tangazo linalosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, likiwa na kipande cha video kinachomuonesha Abubakari Bakhresa akidai kuwa kampuni yake ya Azam inatoa fedha kwa Watanzania kuanzia TSh 4,000,000 hadi 6,500,000, huku usajili ukidaiwa kufanyika ndani ya siku tisa.
Katika chapisho hilo, pia kuna kiungo kinachoonekana kuhusiana na tovuti ya The Citizen, kikiwa na ujumbe unaosema: “Serikali mpya, fursa mpya: Maelfu ya Watanzania tayari wanatumia fursa hii kupata zaidi ya TSh 4,000,000 ndani ya siku 30.”
Je ni upi ukweli wa Tangazo hilo?