Wakuu nimeona hii video inasambaa kwa kasi lakini mbona kama uhalisia ni tofauti?
- Tunachokijua
- Madai
Kupitia mitandao ya kijamii ikwemo Instagram kimesambaa kipande cha video Julai 5, 2026 kikiwonesha baadhi ya watu wakirushiana mawe huku kikiwa kimeambatanishwa na grafiki inayosomeka
"Hatumtaki Samia" Sauti zasikika kwenye Paredi la simba.
Uhalisia ni upi?
Kipande cha video kinachoonekana ni halisi na pia ni tukio halisi lililoteka Julai 5, 2026 lakini sauti inayosikika imehaririwa.
Video hiyo ni kutokea kwenye eneo la Jangwani ambapo parade ya Simba ilipita kushsherekea ushindi wao wa kombe la shirikisho.
Katika video halisi zilizochapishwa katika mitandao mbalimbali ikiwemo Instagram na Youtube hakuna video sauti ya "Hatumtaki Samia' inayosikika badala yake ni sauti za kelele za kawaida za baina ya wananchi hao.
Watumiaji pamoja na vyanzo mbalimbali vilivyochapisha video halisi viliweka ujumbe wa kawaida kuashiria kuwepo kwa ugomvi baina ya mashabiki hao katika eneo la Jangwani, Dar es salaam.
Chanzo kimoja kilichapisha;
Mashabiki wa Simba wakati wakisubiria Parade lipite Jangwani mashabiki hao baadhi wakaanza kurusha mawe Jangwani na kuleta Fujo.
Je, huu no utani kweli?
Chanzo kingine kikachapisha;
Asa sisi Tukachimbe dawa wapi jamni😜😜😅😅😂😂😂😭😭🔥🔥
Na chanzo kingine cha Youtube kilichapisha;
VURUGU | WAPIGANA MAWE | MASHABIKI SIMBA NA YANGA | POLISI WAJITOKEZA 🙌🙌
Uhalisia:
Uhalisia ni kuwa video inayodai kuwa kwenye paredi hiyo sauti za hatumtaki Samia zinasikika inapotosha kwani imehaririwa kwa kuongezewa sauti ambazo hazipi kwenye video halisi.