JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Wakuu, Mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye hivi karibuni nimemsikia akisema akisema mwaka 2018 yeye na wabunge wenzake wa mikoa ya kusini walisimama kutetea zao la korosho bungeni, Pia akitaja mtu anayemuita mjomba pamoja na Lema na wenzake hawakuwa watetezi wa korosho na kwamba leo wakijifanya kutetea ni wanafiki. Anaongeza kwa kusema Mbunge pekee wa upinzani aliyekuwa mstari wa mbele kutetea Korosho alikuwa ni Zitto Kabwe pekee. JamiiCheck Uhalisia ni upi hapa? https://youtu.be/GknHwbaoMdA?si=JeCDz52_jRGSSt_3&t=144
Kumekuwa na akaunti yenye jina la Luaga Mpina inachapisha taarifa mbali mbali kuhusu mambo yanayoendea nchini na kujibu hoja za Mbunge Luaga Joelson Mpina wa jimbo la Kisesa ndani ya mtandao wa X zamani twitter. Naomba JAMIICHEK inisaidia kujua ukweli kama akaunti hii ni mali halali au inamilikiwa na Luaga Joelson Mpina mwenyewe ambaye ni mbunge wa jimbo la Kisesa na kwa sasa yuko nje ya bunge kwa adhabu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu, chama hicho kitaitisha maandamano ya kuuzuia uchaguzi usifanyike. Kauli hiyo ya Lissu, inajibu swali kuhusu mbinu ambayo chama hicho itaitumia kuzuia uchaguzi kuendana na ajenda yake ya ‘No Reforms, No Election’ (bila mabadiliko, hakuna uchaguzi). Lissu amesema hayo leo, Jumatatu Aprili 7, 2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara katika ziara ya kutoa elimu kuhusu ‘No Reforms, No Election.’ Amesema iwapo Serikali haitafanya mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi, chama hicho kitawahamasisha wananchi kuandamana kuuzuia uchaguzi usifanyike. “Hatutaenda kupiga kura...
Tizama hi video kwa makini kabla ya ku-comment. Kiongozi wa Korea kasikazini amelegeza mashariti kwa dini moja tu uko nchini kwake baada ya kushuhudia great miracle en Wisdom katika kitabu cha Qur"an tukufu, wakati anaingia madarakani 2011 Uislamu kama dini zingine zilikua marufuku nchini mwake, mwaka 2015 waislamu kwa kujificha ficha walifika 3000 tu kwasasa waislamu ni 30,000. Adhana ya kila swala kwa kutumia vipaza sauti misikitini imeruhusiwa katika hiyo nchi kali ya kicommunist kuna hofu kubwa kwamba Uislamu ndani ya miaka 10 watagawana hiyo nchi na wa Buddha.
Kama ilivyozoeleka kwenye jamii nyingi kuwa ukiwa Rastafarian basi kwa asilimia kubwa utakuwa unatumia bangi/marijuana na majina mengine lukuki kama inavyojulikana. Leo kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa kuna meme inasambaa ikiwa na ujumbe "Wakati Lucky Dube anaimba "Born to Suffer" me nilidhani ni sababu anavuta bangi" Meme hii ikanikumbusha article niliyowahi kusoma kuwa Lucky Dube alijiepusha na matumizi ya bangi, pombe na sigara ili kuwa mfano mzuri kwenye jamii.
Baada ya kauli ya CDF wa Tanzania Jenerali Mkunda kusema kuwa 'Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi' imenifikirisha sana nikakumbuka nilishawahi kusikia tetesi kuwa Paul Kagame wakati akiwa mkimbizi nchini Uganda, aliwahi kuhudumu kwenye jeshi la nchi hiyo na mpaka kufikia cheo cha Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda. Mpaka sasa tunaona jinsi Kagame anavyoisumbua Uganda labda kutokana na ukweli kuwa anaijua nje ndani. Je, ni kweli Paul Kagame aliweza kuaminiwa na kupewa cheo nyeti kwenye Jeshi la Uganda?
𝐋𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐓𝐎𝐒𝐀 𝐊𝐔𝐆𝐎𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐔𝐁𝐔𝐍𝐆𝐄 , 𝐀𝐏𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐀𝐉𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐘𝐀 "𝐍𝐎 𝐑𝐄𝐅𝐎𝐑𝐌𝐒, 𝐍𝐎 𝐄𝐋𝐄𝐂𝐓𝐈𝐎𝐍" Kupitia ukurasa wake wa Twitter (X), Godbless Lema ametangaza kuwa ameungana na wanachama wengi wa CHADEMA wanaopinga ajenda ya No Reforms, No Election. Lema ameweka wazi msimamo wake wa kushiriki kwenye uchaguzi akisisitiza kuwa ni muhimu kuendelea kupigania mabadiliko ndani ya mfumo wa kisiasa kupitia ushiriki wa moja kwa moja kwenye uchaguzi. Aidha, amethibitisha kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.
Back
Top Bottom