- Source #1
- View Source #1
Wakuu ni kweli hii imetoka kwa Mrema?
- Tunachokijua
- John Mrema ni Mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi wa chama cha ukombozi wa umma (CHAUMMA), awali alikuwa na nafasi hiyo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) KABLA hajahama na baadhi ya wanachama wengine.
Madai
Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanasambaza grafiki yenye utambulisho wa Mwanahalisi digital ikiambatana na ujumbe unaosomeka “CHADEMA IMEKUWA KAMA CHOMBO CHA HABARI”.
Taarifa hiyo imeambatana pia na pichaskrini inayoonesha andiko kutoka ukurasa wa X likionekana kuchapishwa na John Mrema akiishhutumu CHADEMA kupoteza muelekeo na kutoa taarifa kwa Umma mara kwa mara kuliko vyombo vya habari.
Uhalisia wa taarifa hiyo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
JamiiCheck imefuatilia kwa njia ya mtandao na utafutai wa maneno muhimu na kubaini kuwa taarifa hiyo haijachapishwa na Mrema kama inavyoonekana. Pia hadi kufikia wakati ripoti hii inaandikwa John Mrema kupitia ukurasa wake wa X hakuwa ameandika kitu chochote kile.
Aidha grafiki inayotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachapishwa wala kutolewa na chanzo hicho kupitia kurasa zake rasmi za mitandao yakijamii.