JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Katika kile kinachoonekana kama tukio la kihistoria na lisilotarajiwa katika ulimwengu wa Kiislamu, taarifa kutoka Mashariki ya Kati zinaeleza kuwa mwana wa kifalme kutoka familia ya kifalme ya Kuwait, anayefahamika kwa jina la Prince Abdullah Al-Sabah, ametangaza hadharani kuwa ameokoka na sasa ni mfuasi wa Yesu Kristo. Katika faili la sauti lililorushwa kupitia kituo cha televisheni ya Kikristo cha Al-Haqiqa, kinachorusha matangazo kwa lugha ya Kiarabu, sauti inayodaiwa kuwa ya Prince Abdullah inasikika akitangaza kwa ujasiri kuwa amemkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Katika ujumbe huo wa sauti, Prince Abdullah anasema kwa uthabiti kwamba: “Iwapo nitauliwa kwa sababu ya rekodi hii ninayozungumzia wokovu...
Baada ya ukimya wa muda mrefu na msimamo wa kutoshiriki uchaguzi bila marekebisho ya kisiasa, hatimaye mwanasiasa John Heche ameonesha mwelekeo mpya. Kupitia mahojiano maalum, Heche amekiri kuwa harakati za “No Reform No Election” zimepoteza mwelekeo na hazina maana tena katika hali ya sasa ya kisiasa. Amesema yuko tayari kushiriki uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa ni muhimu kujipanga ndani ya mfumo uliopo ili kuleta mabadiliko ya kweli. 🎧 Sikiliza mahojiano kamili hapa
Katika chapisho lililopigwa pini kwenye ukurasa wake wa X, Zitto Kabwe ameikosoa vikali CHADEMA kwa kile anachokiita unafiki na kukosekana kwa mfano wa kuigwa. Amedai kuwa ni unafiki kwa viongozi wa chama hicho kuhimiza ususiaji wa uchaguzi huku wakiburuzana mahakamani kuhusu mali za chama. Zitto amehoji iwapo haya ndiyo mabadiliko ya uchaguzi yanayotakiwa na kama kuna jambo la kuigwa katika mwenendo huo. Ametamka wazi kuwa yeye na chama chake hawatasusia uchaguzi, bali wataendelea kupambana kwa ajili ya maslahi ya Watanzania wote.
Waziri wa mambo ya nje wa Cyprus bwana Constantinos Kombos, alitumwa kumwakilisha kamishina wa wambo ya nje katika umoja wa ulaya kuja Tanzania. Moja ya Marengo ya ziara hiyo ilikuwa ni kuangalia jinsi uchaguzi mkuu utakavyofanyika. Ratiba ya awali ilionesha bwana Kombos angeondoka July 10. Lakini cha kustajabisha amehairisha safari Hadi July 15, Ili audhurie kesi ya Lissu. Itakuwa mara ya kwanza Tanzania kiongozi wa umoja wa ulaya kwenda Kisutu kihudhuria kesi ya mtanzania. Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, Constantinos Kombos akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mahmoud Thabit Kombo.
Back
Top Bottom