Wakuu nimeona hii taarifa kuwa Mbunge wa Chadema wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenan, ametangaza kuwa atashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu, akipinga kaulimbiu ya chama chake ya "No Reform, No Election," inayosisitizwa na Mwenyekiti Tundu Lissu.
Taarifa imeongeza kuwa akizungumza na wananchi wa jimbo lake, Khenan alisema kaulimbiu hiyo haina mashiko kwani ni msimamo wa mwenyekiti pekee na si wa wanachama wote. Alibainisha kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa Chadema hawaungi mkono kususia uchaguzi, wakiona kuwa hatua hiyo inakiuka sheria na kuwanyima wananchi haki yao ya kupiga kura.
Kama kweli, basi atakuwa amekisaliti chama kilichompa dhamana.