- Source #1
- View Source #1
Wakuu ni kweli kuwa huu ujumbe umechapishwa na Sugu?
- Tunachokijua
- Joseph Mbilinyi (Sugu) ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Nyasa. Sugu ni msanii pia ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini.
Madai
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii Septemba 11, 2025 zilisambaa grafiki zenye utambulisho wa baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo Jambo Tv na Mwananchi zikiwa na jumbe tofauti ila zote zikionekana kurejelea kile kinachoonekana kuwa ni chapisho la Joseph Mbilinyi (Sugu) alilolichapisha kupitia ukurasa wake wa X. Sehemu ya Chapisho hilo linasomeka;
"Kwa namna mambo yanavyoenda na hizi kampeni na hizi kampeni zinazoendelea nchini ni dhahiri CHADEMA tulifanya WRONG move kuja na ajenda ya NRNE"
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
Jamiicheck imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Keyword Search) umebaini kuwa taarifa hiyo haijachapishwa na vyanzo hivyo kama inavyoonekana na badala yake zinaonekana katika vyanzo ambavyo si rasmi.
Aidha utafutaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa chapisho hilo linaloonekana kuchapishwa na Sugu kupitia ukurasa wake wa X ni la kughushi kwani halipo katika ukurasa wake rasmi na wala hakuwahi kuchapisha ujumbe wa aina hiyo.
Hata hivyo grafiki zinazoonekana kutumika kusambaza taarifa hiyo, yaani ya Mwananchi na Jambo Tv ni za kughushi kwani hazijachapishwa na vyanzo hivyo licha pia ya kuwa na mapungufu kadhaa ukilinganisha na grafiki halisi za vyanzo hivyo.