McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,075
- 3,391
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema kutoa Kitambulisho cha Taifa (NIDA) unapotembelea nyumba ya kulala wageni hakumaanishi kuanika taarifa binafsi, kwani kitambulisho hicho si taarifa binafsi.
Soma Pia: Waziri Katambi: Wamiliki wa Hoteli, AirBnB, Guest Houses na Lodge nchini wasajili wageni wote kwa kutumia kitambulisho cha NIDA
Akizungumza Juni 29, 2026, jijini Dodoma alipokuwa akizungumza katika mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Katambi amesema taarifa zilizopo kwenye Kitambulisho cha Taifa si za siri, ndiyo maana hutolewa pale zinapohitajika katika taasisi au maeneo mbalimbali, hata katika mazingira ya wazi
"Kitambulisho cha taifa sio taarifa binafsi. Taarifa binafsi.. kitambulisho cha taifa ni public na ndio maana umesajilia namba ya simu eh... NIDA yako umejisajili, umeionyesha popote, umeipiga fotokopi, umeambatanisha kwenye mikataba ya kuuziana ardhi na nini, hio sio taarifa binafsi. Particular za mtu za yeye ni nani, eh anaishi wapi, ana umri gani, hizo sio taarifa binafsi. Ni public kwa sababu kila mahali lazima mtu utaulizwa hivyo, na ndio maana mnafanya na birthday."