Zungu: Wabunge wapo huru kutoa mawazo na kufanya majadiliano. Sijatoa Kibali Mbunge kuhojiwa TAKUKURU

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, amekanusha madai ya vyombo vya habari yanayodai kuwa baadhi ya wabunge wameitwa kuhojiwa na TAKUKURU kutokana na michango yao wakati wa mjadala wa hotuba ya Rais. Akizungumza bungeni Dodoma Februari 5, 2026, amesema ofisi yake haijapokea wito wowote wala kutoa kibali kwa mbunge yeyote kuhojiwa.

Amesisitiza kuwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge, wabunge wana uhuru wa kutoa maoni na kushiriki mijadala bila hofu, shinikizo, kushtakiwa au kuhojiwa. Uhuru huo unalindwa na Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na kifungu cha 3C cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge.

Soma: TAKUKURU yawaita Shabiby na Kangi Lugola

Hata hivyo, Spika Zungu amesema endapo mbunge atakiuka kanuni za Bunge kwa kuchangia hoja zisizoruhusiwa, Spika ana mamlaka ya kuagiza mchango huo ufutwe au mbunge husika kufuta kauli yake. Akikaidi, hatua za kinidhamu zinaweza kuchukuliwa ikiwemo kupelekwa kwenye Kamati ya Bunge kwa mahojiano.

Speaker wa Maana sanaaa mtoto wa Mjini ni mtoto wa mjini tuu😂
 
TAKUKURU huwa ni wapumbavu sana kama wafuasi wa Lissu. Nakumbuka Zitto aliongelea hili na kuwaonya TAKUKURU ila wafuasi wa Lissu wakamshambulia.
 
well done Zungu
Screenshot_20260204-173407~2.png
 
TAKUKURU huwa ni wapumbavu sana kama wafuasi wa Lissu. Nakumbuka Zitto aliongelea hili na kuwaonya TAKUKURU ila wafuasi wa Lissu wakamshambulia.
Wafuasi wa samuya form 4 failure ndio hawana akili kama boss wao alivyo, lissu ni big brain special school Illboru product acha kumfananisha na kiazi cha kizimkazi!
 
Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan Zungu, ametoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa kwenye vyombo vya habari juu ya baadhi ya wabunge kuitwa na TAKUKURU kuhojiwa kuhusu michango yao waliyotoa bungeni wakati wakichangia hotuba ya Rais.

Ameeleza kuwa kwa mujibu kanuni ya 5 za kudumu za bunge 2025 ameona kuwa ipo haja ya kufafanua suala la haki na uhuru wa majadiliano bungeni. Wabunge wapo huru kutoa mawazo na kufanya majadiliano bila shinikizo, hofu, kushtakiwa au kikwazo kingine chochote ambapo uhuru huo unalindwa chini ya ibara ya 100 ya Katiba 1977 na chini ya kifungu cha 3,6 sheria ya kinga madaraka na haki za bunge sura ya 296.
Kuna uhuru gani kama kuna masuala ambayo hawaruhusiwi kuzungumzia? Alipaswa kutaja hayo masuala na kutoa sababu za zuio hilo.

Aidha, azitaje sheria ambazo zinazuia mbunge kuhojiwa na chombo chochote cha dola bila kibali cha Spika.

Amandla...
 
Speaker wa Maana sanaaa mtoto wa Mjini ni mtoto wa mjini tuu😂
Acha tu nisiseme lakini ukweli ni kwamba maspika walikua Msekwa na Sita.
Ila Tanzania tumepitia, mnakumbuka enzi za kile kigurunyembe?
 
Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azzan Zungu, ametoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa kwenye vyombo vya habari juu ya baadhi ya wabunge kuitwa na TAKUKURU kuhojiwa kuhusu michango yao waliyotoa bungeni wakati wakichangia hotuba ya Rais.

Ameeleza kuwa kwa mujibu kanuni ya 5 za kudumu za bunge 2025 ameona kuwa ipo haja ya kufafanua suala la haki na uhuru wa majadiliano bungeni. Wabunge wapo huru kutoa mawazo na kufanya majadiliano bila shinikizo, hofu, kushtakiwa au kikwazo kingine chochote ambapo uhuru huo unalindwa chini ya ibara ya 100 ya Katiba 1977 na chini ya kifungu cha 3,6 sheria ya kinga madaraka na haki za bunge sura ya 296.
Sema self imposed Spika, siyo spika!
 
Hayo maigizo ya ccm na takukuru yanachosha sana
Yanalenga kututoa Kwenye reli

Hilo bunge na serikali njia iliyopatikana tarehe 29 sio
 
Kuhojiwa na takukuru ni hadi spika atoe kibali? Nchi ya kipumbavu sana hii.
 
TAKUKURU huwa ni wapumbavu sana kama wafuasi wa Lissu. Nakumbuka Zitto aliongelea hili na kuwaonya TAKUKURU ila wafuasi wa Lissu wakamshambulia.
Hayo maigizo ya CCM TU
TAkukuru wangekuwa seriously hakuna mbunge wa Ccm angekuwa bungeni
 
Back
Top Bottom