Watu wengi wanadis dstv, bila kujua ukweli juu ya gharama zao. Kiukweli ukiondoa gharama (kubwa) ya installation, lakini jamaa wana packages za hadi tsh 16,000/=(kufuatana na bei ya $) kwa mwezi ukilinganisha na Startimes ya 18,000/=. Na kwa taarifa nilizonazo ni kwamba unaweza ukaongeza fta channels nyingine(ambazo unazilipia kwenye hivyo ving'amuzi vingine). So unaweza ukakuta hata huo unafuu tuanaodanganywa hapa ni hakuna kitu.
Kwa taarifa nilizonazo, ni easy tv tu ndio wanaojitahidi kuonyesha local channels(except Agape), lakini nao service yake ipo Dar tu. Zuku wanaonyesha TBC na ITV pekee tena kwa mazabe. Startime wote tunawajua, ni wezi tu. So tunapokuwa tunachangia tukumbuke wachangiaji wengine tupo mikoani, hakuna Easy tv huku wala Startimes. Kuna baadhi ya maeneo tunatumia Cables, na hii ndiyo nawezasema ni nafuu kuliko zote, ila unaweza ukawa unaishi maeneo ambayo hizi cable hazijafika. Tunahitaji kampuni ambayo itatoa service ya uhakika na bei nafuu.
DSTV: Ngalia
hapa, kisha upime uone kama kweli dstv ni ghali kiasi hicho, ukilinganisha na Zuku ya tsh 40,000/= au 60,000/=
Pitieni packages tofauti tofauti, baadaye nitakuja kuwapa bei ya kila package, au kama kuna mwingine anajua bei zake anaweza kutusidia hapa.
​- Select
Choose your product. Then bofya kwenye hicho kidirisha hapo, itakuletea let's say
Dstv Premium, hapo chini watakuletea list ya channels za package hiyo na maelezo ya kila channel. Kwa kila package unayochagua, itakuonesha list ya channels ktk kifurushi hicho.