BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,526
- 3,802
Salama wakuu,
Sio leo wala kesho lakini baada ya miaka mingi mbele kutakuja kuwa na changamoto ya maeneo ya kuzikia.
Najua wengi tutasema nchi bado ina maeneo mengi sana lakini ukweli ni kwamba watu wanaongezeka kwa kiwango kikubwa, mwaka 2050 tunategemea kuwa na watu zaidi ya milioni 137 nchini Tanzania. Wakati huo huo, kati ya watu 1000 basi watu sita wanakufa Tanzania.
Binadamu unatakiwa kuishi kwa kutatua matatizo yanayoweza kujitokeza huko mbeleni kabla hayajakukuta, nchi za wenzetu kwa kuona hilo sasahivi wanazika kwenye maghorofa.
Huu utaratibu wa kujengea makaburi, hasa huu utaratibu wa kisasa ni changamoto itakayo kuja kujitokeza miaka mingi ijayo. Pengine wakati hiyo changamoto inakuja kujitokeza mimi sitakuwepo na hata wewe unayesoma hutakuwepo ila andiko hili litakuwepo na litawahukumu.
Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app