Stories of Change - 2023 Competition
Jul 29, 2023
2
4

1690708692536.png

Picha; The chanzo.

UTANGULIZI
Nchi zote duniani ikiwemo Tanzania, hofu ya ustawi wa maliasili inazidi kuongezeka kutokana na wimbi la ongezeko la watu duniani na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi. Inakadiliwa kuwa ifikapo mwaka 2050, Tanzania itakuwa nchi ya tatu kwa wingi wa watu Afrika baada ya Nigeria na Ethiopia. Hali hii inaongeza hofu na mivutano kati ya wakulima na wafugaji kutokana na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na ushindani wa ardhi, mgawanyo wa rasilimali, tofauti za kitamaduni, na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Pamoja na jitihada za serikali na taasisi mbalimbali za kijamii katika kuondoa migogoro hiyo inayodumaza maendeleo, bado vilio ni vingi sana kwa wakulima na wafugaji huku kila mmoja akimtupia lawama mwenzake. Viongozi wanalalamikia mabadiliko ya tabia ya nchi ndiyo sababu mama ya migogoro hii. Mkulima anapaza sauti kwa umma na mamlaka za serikali kuwa mfugaji adhibitiwe asivamie mashamba na maeneo yenye rutuba kwani anahatarisha uzalishaji wenye tija; mfugaji naye anauliza swali kuwa, katika zile hekta millioni 44 zinazofaa katika shughuli za kilimo na mifugo yako wapi maeneo yaliyotengwa kwaajili ya ufugaji? Swali la msingi linabaki kwa jamii na serikali kuwa ni nini hatma ya migogoro hii?

Tunapoendelea kutafuta majibu ya sintofahamu hii ili kurejesha amani na umoja kati ya makundi haya, serikali, taasisi mbalimbali na jamii kwa ujumla zinapaswa kujibu maswali matatu yafuatayo;

NI NINI HATMA YA UPUNGUFU WA CHAKULA KWA SIKU ZIJAZO?

Swali hili linanikumbusha hadithi ya mwanasayansi wa uchumi na demografia maarufu nchini Uingereza Bw. Thomas Malthus aliyeishi kipindi cha mapinduzi ya viwanda 1766-1834. Katika kipindi hicho, uwiano kati ya ongezeko la watu na uzalishaji wa chakula ulikuwa mdogo sana. Kufuatia upungufu wa chakula, watu walikumbwa na janga la njaa, magonjwa na maafa huku makazi na shughuli nyingine zilizidi kupunguza eneo la uzalishaji. Bw. Malthus Kupitia Makala yake maarufu ya “Misingi ya Idadi ya watu” aliamini kuwa Bara la Ulaya lisingeweza kuwianisha ongezeko la watu na uzalishaji wa chakula, isipokuwa kudhibiti ongezeko la watu kwa kuondoa msaada wa chakula na serikali kujitoa katika kusaidia watoto masikini ili kukuza uwajibikaji katika uzalishaji.
1690709147099.png

Ni dhahiri kuwa, mfano huu unashabihiana na Tanzania ya sasa, ambapo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, idadi ya watu 19,812,197 imeongezeka toka sensa ya mwaka 2012 na kufanya idadi ya watu kuwa 61,741,120 huku uwiano kati ya ongezeko la watu na ukuaji wa sekta za uzalishaji wa chakula ukiwa ni 3.2% kwa 3.4%. Hivyo, pamoja na kutumia sayansi na teknolojia katika kuimarisha upatikanaji wa chakula, bado tunahitaji kujenga mifumo bora ya utawala, itakayotoa haki na usawa kwa kila raia ili aweze kupata na kutumia kwa staha rasilimali zilizopo kama vile ardhi, vyanzo vya maji, misitu n.k.​

NI NINI HATMA YA MAZINGIRA AMBAYO NDIYO NYUMBA YETU YA PAMOJA?

Ripoti ya Umoja wa Mataifa (2015) inatukumbusha kuwa, ifikapo mwaka 2050 Tanzania itakumbwa na athari lukuki katika mazingira. Nusu ya ardhi ya kilimo udongo utakuwa umeathirika; matumizi holela ya mbolea na kemikali katika kilimo pamoja na taka za wanyama kutoka maeneo ya wafugaji zitachangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa vyanzo vya maji na kuongeza uzalishaji wa hewa chafu ambazo zinachangia katika mabadiliko ya tabia ya nchi.

Serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ni muhimu kutatua changamoto zinazowakabili wakulima na wafugaji kwa kutafuta suluhisho litakalowezesha kufanya shughuli zao kwa kuzingatia ustawi wa mazingira. Mwanasayansi kutoka Zimbambwe Bw. Allon Salvory katika wasilisho lake kwenye kipindi maarufu cha runinga cha TED+ mwaka 2013 anabainisha kuwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi njia pekee iliyosalia ni “ushirikiano wa utunzaji wa malisho”. Anabainisha kuwa ufugaji wenye kudhibiti mifugo unaweza kusaidia kupambana na ukame na kupunguza athari katika mazingira yetu. Ufugaji huo unaofuata mwenendo wa asili wa makundi makubwa ya wanyama utasaidia kuboresha afya ya udongo, kuongeza upishaji wa kaboni, na kurejesha mfumo wa ikolojia. Mapendekezo haya ya kisayansi yakifanyiwa kazi ipasavyo kilimo kitakuwa uti wa mgongo imara katika nchi yetu.

NI NINI HATMA YA UCHUMI WETU?
Mchumi maarufu nchini Bw. Zitto Kabwe katika wasilisho lake kwenye Bunge la bajeti ya mwaka 2017/18 akichangia kuhusu sekta ya kilimo alitukumbusha kuwa, ili taifa letu liondokane na umasikini tunahitaji uchumi ukue kwa kasi ya wastani wa 8% kwa miaka 10 mfululizo. Sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ambayo imeajiri watanzania zaidi ya 70% inapaswa kuwa sekta kuu inayochochea ukuaji wa uchumi . Ni dhahirri kuwa, hatma ya uchumi wetu imebebwa na wakulima na wafugaji na katu wasiachwe nyuma kwani ndio wamebeba hatima ya ushindi wetu katika vita ya kiuchumi.
Hivyo ni wajibu wa serikali kutatua migogoro ya makundi haya kwa kuwekeza fedha kuwezesha miundombinu ya umwagiliaji, mbegu za mazao na malisho, kuongeza thamani na kupanua masoko.

MAPENDEKEZO.
Taifa lenye amani na umoja daima hustawishwa na misingi ya upendo, haki na usawa, uwajibikaji, uwazi na kushirikisha wananchi katika maamuzi. Na kwa kuwa Tanzania ni moja kamwe tusiruhusu chozi la mkulima au mfugaji lidondoke kwa kufanya yafuatayo;​
  • Tuboreshe sera ya ardhi iweze kukidhi matakwa ya kila mmoja;​
  • Tutunge sheria zinazozingatia haki na usawa kwa kila raia;​
  • Kipindi cha kuandaa bajeti tuweke upendeleo kwa wakulima na wafugaji ambao wanashikiria uchumi wa taifa letu; na​
  • Mwisho, tusipuuze maendeleo ya sayansi na teknolojia bali tuongeze msukumo wa kisera na kifedha ili kukuza ubunifu na uvumbuzi.​
HITIMISHO
Basi, ikiwa ni wajibu wa kila mtu kuimarisha uchumi wa taifa letu na kufikia kilele cha maendeleo endelevu, ni muhimu kutambua kuwa migogoro kati ya wakulima na wafugaji ni tatizo lenye mizizi mingi. Suluhisho lake linahitaji ushirikiano wa kisiasa, kijamii, kiteknolojia na kisheria ili kuondoa migogoro hii. Kwani kuwepo kwa mivutano kati ya makundi haya mawili kunazidisha athari kubwa na za muda mrefu zinazoweza kuathiri maisha na mazingira kwa vizazi vijavyo.​

KUMBUKUMBU ZA REJEA.

Malthus, T.R. (1798). Insha kuhusu kanuni ya idadi ya watu. J. Johnson.
Savory. A (2013) Jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi [Faili laVideo]. Chanzo
URT (2022). “Sensa ya watu na makazi [2022]”. Ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali. Dodoma
Kabwe. Z (2017) Mapendekezo ya mbunge Zitto Kabwe kuhusu kilimo [Faili laVideo]. Chanzo
 
View attachment 2702901

View attachment 2702914

Kabwe. Z (2017) Mapendekezo ya mbunge Zitto Kabwe kuhusu kilimo [Faili laVideo]. Chanzo​
 
Asee unamawazo kuntu na yenye kulenga mapinduzi katika kuiendeleza Tanzania 👏
 
Back
Top Bottom