Zomea zomea ya Mramba huko Rombo


r u serious? tuchague lifisadi kwa vile lime-deliver!kweli bado tupo mbali sana!!
 
kakaa jimboni miaka mingapi? na maendeleo yake yako relevant na muda aliokaa kama mbunge? huyo mtu hafai wataenda bungeni kupinga miswada ya maana kwa kutetea maslahi yao
 
Wakuu Mramba anapumulia mshine sasa. Hana sera kwa watu wa Rombo. Sera zake sasa zimekuwa za matusi kuliko kusema atafanya nini. Ukweli ni kuwa keshajua kuwa watu wa Rombo wanamjua sasa. Mfano kwenye mojawapo ya kampeni zake aliwahi kusema kuwa Rombo hakuna mwanaume kama yeye. kauli hii iliwachukiza sana wanaume wa rombo kuwa yeye ndiye mwanaume pekee Rombo.
Sasa hivi watu wakizomea anawaonyesha alama ile ya kupenyeza kidole gumba katikati ya vidole na kuwafanyia ishara ile ya baadhi ya watu ya kuonyesha kuwa mtu fulani anatumiwa kinyume na maumbile. Hali ni tete kusema ukweli na yote ni kwa kudra za Mwenyezi Mungu.
 

Nadhani wapiga kura wa Rombo ni challenging zaidi ya wa Bagamoyo...kumbukeni 1995 walimbwaga
 
r u serious? tuchague lifisadi kwa vile lime-deliver!kweli bado tupo mbali sana!!

Heshima kwako Chapakazi,

Nadhani umeshindwa kumwelewa JokaKuu na pengine hutendi haki,ukisoma vizuri post yake huwezi kuona sehemu kamfagilia Mramba.

Mramba ni fisadi kwa asilimia zote lakini kafanyakazi vizuri Rombo,wapiga kura wengi Tanzania hasa vijijini hawaangalii sana maslahi ya taifa sana sana wanaangalia maslahi ya jimbo lao.Mkuu Chapakazi kama wapiga kura wengi wangekuwa wanaangalia utendaji wa wabunge kwa maana ya maslahi ya taifa mbunge anayemaliza muda wake Mhe Zitto Kabwe asingekuwa na sababu za kufanya kampeni !.
 

Wote ni ufisadi tu, kuna watanzania wengi tu pamoja na warombo wanaoathirika na ufisadi huo.
 

Bado hujawa na standards zinazopaswa kulifanya taifa la Tanzania kuendelea mbele hata kama unajiita mpinzani. Wakati wote utaifa kwanza na si vinginevyo. Huwezi kumsifu mwizi eti kwa sababu anawatunza watoto wake vizuri, haya ndo yaliyotufikisha hapa tulipo leo na imekuwa kazi kubwa kwetu kuutua mzigo huu.

Tumpinge mtu yeyote anayeiba mali ya umma huku akiwa serious na kuendeleza kwao, in fact hata wa kwao wanatakiwa wamkatae kiongozi wa namna hiyo. Hapo ndipo tutakapoona maendeleo ambayo ni even. Kuna warombo wengi tu hawaishi Rombo so wanahitaji better schools kama zilizopo Rombo. Kwa hiyo priority iwe nchi na sio kwenu.
 

Hilo nalo neno; tofauti kubwa kati ya fisadi wa kichaga na hawa mafisadi wa kikwere toka Bagamoyo!!
 
Chesty,Chapakazi,Eeka Mangi,

..jamani mimi ni kati ya wale waliopinga sana kitendo cha JK kumpigia kampeni Mramba.

..nakubaliana na nyinyi kwamba Mramba ni fisadi, lakini wakati huohuo lazima tutambue kile kinachoendelea huko majimboni.

..wapiga kura huko majimboni wana mambo mengi sana yanayowasibu kimaisha, pia wanakwazwa na elimu ndogo, hivyo basi si rahisi kufuatilia hizi hoja za kitaifa ambazo sisi tulioko mjini tuna access na taarifa nazo.

..sasa a disconnect btn wapiga kura wa Rombo na masuala ya kitaifa ndiyo yaliyosababisha Mramba akapita kwa kishindo ktk kura za maoni za CCM.

..mpiga kura wa Rombo wa leo haangalii Mramba alisema nini, au alishiriki vipi, ktk suala la ununuzi wa ndege ya Raisi, au Alex Stuart, etc etc, bali anaangali Mramba amechukua hatua gani kutatua kero zinazowakabili wananchi wa Rombo.

NB:

..Mramba aliwahi kushindwa uchaguzi mwaka 1995 kwa tuhuma za kushindwa kutatua kero za wana Rombo. sasa kama kuna maswala ambayo ameshindwa kuyashughulikia tangu mwaka 2005 basi nina imani wananchi wa Rombo watamkataa. They have done it before.
 
Hii tabia ya CCM kupenyeza dole gumba katikati wameitoa wapi lakini lol??!! Nasikia kule tarime, Makamba anasadikiwa kufanya mchezo kama huo pia...Tabia mabaya sana CCM!! HAMNA ADABU KABISA NYIE!!!!!
 
Hii tabia ya CCM kupenyeza dole gumba katikati wameitoa wapi lakini lol??!! Nasikia kule tarime, Makamba anasadikiwa kufanya mchezo kama huo pia...Tabia mabaya sana CCM!! HAMNA ADABU KABISA NYIE!!!!!

hahahahaaaa!!! umenichekesha sana, waqnasema kwenye kampeni ni ruksa kupiga hata chini ya mkanda!
 
matokeo ya Mramba kura za maoni yalichakachuliwa huwezi kushinda kura ati 8000 kamili yaani namba kama 8100 au 8200 ni nadra sana huu ni wizi kuna kura zaidi ya 5000 ziliingizwa kwa taarifa za kiuhakika watu walipigana huko Tarakea baada ya kugundua hayo na hata Kikwete mwenyewe aliambiwa ila alifunika kombe mwanaharamu apite! unajua mramba na click yake wanachangia hela kambi kampeni ya CCM? Muulize Kikwete kwanini alinyuti na kesi ya Mramba iko njiani kufutwa!
 
Nani alikuambia Warombo wanampenda Mramba kwa ajili ya Njaa? Mramba ametufanyia mambo makubwa ROMBO, amevuta maji toka Moshi Vijijini kuja Rombo, amesukuma lami imewekwa hadi msituni, amejitahidi shule za Kata kupata waalimu. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
hivi ni nani mshindani wake huko.hatusikii chadema ama mimi peke yangu?
 

Mkuu Semilong,

Naomba utu/nifafanulie una maana gani unaposema njaa?..................je ni sehemu zipi hizo pale Rombo zenye njaa............?
 
Mkuu Semilong,

Naomba utu/nifafanulie una maana gani unaposema njaa?..................je ni sehemu zipi hizo pale Rombo zenye njaa............?
Kamwanga na Rongai watu walinyang'anyw mashamba yao huko
 
"mtofautishe na Kikwete na Dr.Kawambwa wanaofanya ufisadi kwenye miradi ya ujenzi wa barabara bagamoyo"

Mkuu Joka kuu hii ni kali kuliko lakini yenye ukweli.
 
kura za maoni zilikuwa na maana nzuri tu ila wenye pesa walitumia kupita na kuwaacha wenye uwezo wa utendaji, mramba naamini alipita kwa njia hii, kwa maana hii ccm itapoteza kwa kutokuwa makini kumkubali huyu aiwakilishe rombo, warombo nao waamke wasithamini mno pesa kama walivyo sasa kwa mtaji huu watapata viongozi wasiomakini. mtu kama mramba na pesa yote aliyonayo nawatoto waliosoma vizuri kweli anashindwa kuwatatulia tatizo la maji mpaka leo hii aibu gani hiii haya mapesa atapeleka wapi baala yakuwatumikia wananchi hata huruma hana lo anatisha mavyeo haya wanataka yanini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…