Kumbe ishu ya Makonda imemlaza Gwajima na viatu

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Aisee sikutegemea kama ishu ya kuteuliwa kijana Paul Christian Makonda huko CCM imewaumiza, imewakera, imewapagawisha, imewachukiza na kuwafurahisha watu tofauti tofauti na wenye heshima mbali mbali nchini.

Kati ya watu ambao inasemekana kuwa walipagawa na kuchanganyikiwa kwa kuchaguliwa kwa Makonda basi ni kaka yetu, kiongozi wetu wa kiroho na mbunge wetu wa Kawe mh askofu Gwajima.

Inasemekana kuwa kurudishwa kwa Makonda katika nafasi kubwa, na ya ushawishi kichama kimeonekana kuua ndoto yake kabisa ya kuendelea kulifanya Jimbo letu shamba lake la bibi just kwa kupokea mamilioni ya mshahara wa bunge bila kujishughulisha na tatizo au kero yoyote ile iliyopo Jimboni kwetu.

Ikumbukwe kwamba Makonda ashawahi kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni kabla ya kupandishwa cheo na kuwa mkuu wa mkoa mzima wa Dar es salaam. Hivyo anaijua vizuri Kawe na changamoto zake. Maeneo mengi ambayo leo hii yana barabara na miundombinu mizuri jimboni hapa, yalitokana na juhudi za kijana huyo alipokuwa mkuu wa wilaya hii, hivyo kama ataamua kugombea ubunge katika Jimbo hili, basi atakuwa na kazi ya kumalizia changamoto kadhaa zilizobakia, ambazo kwa sasa hakuna mbunge, mkuu wa wilaya wala diwani anaeshughulika nazo.

Inasemekana hata mwaka 2020, alikuwa na lengo la kugombea Jimbo la Kawe, lkn alibadilisha mawazo yake na kukimbilia Kigamboni baada kujua kwamba mwenyekiti wa chama chake wakati huo alikuwa ashamuandaa askofu agombee hapo, hivyo kama Makonda angethubutu kugombea Kawe ni lazima angekatwa tu kama ilivyotokea kwa brother Pascal Mayalla . Hivyo ili kuepusha hayo ikabidi ajitahidi kwenda Kigamboni ambapo alieshindwa katika kura za maoni.

Inasemekana kwamba kabla ya uteuzi wa Makonda, ndugu Gwajima alikuwa ana relax tu ofisini akijua kwamba hakuna kiongozi yoyote mwenye uthubutu wa kugombea katika Jimbo analoliongoza, na ukizingatia alikuwa anajua kwamba Paul Makonda alikuwa tena si lolote wala chochote chamani.

So uteuzi umemshtua na kuanza kufikiria kwamba ikiwa Makonda atahitaji au kuhitajika kugombea yeye atakuwa na mbinu gani ya kumzuia (Makonda) kushinda katika kura za maoni na akizingatia mtu ambae alimbeba kipindi kile hayupo, alaf huyu mwenye rungu wa sasa (mwenyekiti) sio mtu wa kubebana hovyo hovyo.

Presha imempanda zaidi baada ya kusikia kwamba kuna wazee kutoka jimboni Kawe, pamoja na vijana mbali mbali wanapanga namna watakavyomshawishi Makonda aje kugombea hiyo 2025, ili kumng'oa ndugu Gwajima ambae haoneshi kabisa kuguswa na changamoto mbali mbali zilizopo jimboni.

Kwa niaba ya mtonyaji wangu ambae ni mtu wa karibu kabisa na mbunge kiroho, na kisiasa. Anasema kuwa mbunge huyo sasa hivi hana furaha hata kidogo.

Maana inaonekana kijana hapo uenezi kawekwa kwa muda tu, lkn baadae atasogezwa mbele na kuwa na nafasi kubwa ya kuweza kugombea au kuteuliwa nafasi yoyote ya kichama au kitaifa.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom