Zoezi la bomoa bomoa kuanzia Kimara hadi Kiluvya

Ramani za mipango miji zinaonyesha upana wa barara ni mita 243 na ni zazamani tu kama mtu amejenga bila kufuatilia ramani imepanga matumizi gani ya ardhi katika eneo husika hapo asiilaumu serikali
May be upo sahihi ila najua unajua kwamba serikali ipo kila sehemu ya ardhi yake kwenye nchi hii. Na hapo ndipo kwetu sisi wanasheria huwa tunashangaa sana kwamba inakuwaje watu wanajenga mpaka sehemu inakuwa mji tena mkubwa tu halafu serikali iseme wamevamia????? Hii yote ni kukosekana kwa uwajibikaji serikalini. Watu wanahitaji makazi halafu hawatengewi maeneo na yakitengwa basi serikali inauza viwanja kwa bei ya juu sana ambayomtanzania wa kawaida hawezi kumudu. Unakuta sehemu iliyopimwa wanauza square meter moja kwa elfu 15 sasa ukitaka kiwanja cha square meter 600 unahitaji milioni tisa wakati ukienda unsurveyed area unapewa kwa milioni tatu au nne sasa huoni serikali ndio inachangia haya mambo yote!!!!!! Whether kuna plan au hakuna serikali I walipe fidia hao ni wananchi wake na ni watu wenye familia imagine ingekuwa ni wewe kwa kweli iwaangalie kuwasaidia ndio maana ya kuwa na serikali ni kama mzazi vile
 
Hili janga litaathiri wengi zaidi ya wale wa vyeti fake. Mita mia moja na ishirini kutokea katikati ya barabara sio mchezo
 
tunahitaji maenedeleo na barabara ni nyezo muhimu sana ktk kuharakisha maendeleo.
kwakweli serikali yetu imedhamiria kwa vitendo sio maneno tu,
wenye macho tunaona!!
naunga mkono na nitawashawishi wananchi wenzagu kuhama haraka ili kupisha Ujenzi wa barabara.

hakika Ujenzi wa barabara hii utaondoa au kupunguza msongamano katikati ya jijji.
tunahitaji kazi kwa vitendo Kama hii sio porojo!!
 
Hayo maeneo zamani yalikuwa mpaka na mabango kabisa yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara.. ila sijui yameenda wapi.
 
May be upo sahihi ila najua unajua kwamba serikali ipo kila sehemu ya ardhi yake kwenye nchi hii. Na hapo ndipo kwetu sisi wanasheria huwa tunashangaa sana kwamba inakuwaje watu wanajenga mpaka sehemu inakuwa mji tena mkubwa tu halafu serikali iseme wamevamia????? Hii yote ni kukosekana kwa uwajibikaji serikalini. Watu wanahitaji makazi halafu hawatengewi maeneo na yakitengwa basi serikali inauza viwanja kwa bei ya juu sana ambayomtanzania wa kawaida hawezi kumudu. Unakuta sehemu iliyopimwa wanauza square meter moja kwa elfu 15 sasa ukitaka kiwanja cha square meter 600 unahitaji milioni tisa wakati ukienda unsurveyed area unapewa kwa milioni tatu au nne sasa huoni serikali ndio inachangia haya mambo yote!!!!!! Whether kuna plan au hakuna serikali I walipe fidia hao ni wananchi wake na ni watu wenye familia imagine ingekuwa ni wewe kwa kweli iwaangalie kuwasaidia ndio maana ya kuwa na serikali ni kama mzazi vile
Yaani hivyo viwanja vya milioni 40 watauziana wenyewe tu kwa kweli
 
Bomoa Bomoa ya makazi, nyumba, majengo na mali Morogoro Road Kuanzia Ubungo mpaka Kiluvia.

Leo mbunge wa Kibamba John Mnyika alikuwa na mkutano na wananchi wa jimbo lake kuhusiana na barua zilizosambazwa hivi siku 10 zilizopita kwa wakazi wa maeneo kutoka Kimara Mjini mpaka Kiluvia na TanRoads na alama za kutaka nyumba, majengo na mali kubomolewa kwa kuwa zinasemekana ziko kwenye hfadhi ya barabara ya Taifa.

Barua hizi zimetolewa na TanRoads MKoa wa Dar Es Salaam na mazungumzo ya watu yamechukua mkondo usio makini na kulifanya hili ni jambo la kisiasa.

Wengi wanaongea bila kujua undani wa jambi hili na zaidi ni ushabiki usio na mantiki.

1. Miaka ya 70,80,90 Serikali iligawa maeneo along Barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo a kuendelea hadi Kiluvia kutokana na wananchi waliopoteza makazi maeneo kadhaa ya jiji na hata kusaidia kupanuka kwa jiji.

2. Asilima kubwa 75% ya waliojenga nyumba, majengo ni halali na hata kwenye ramani za mipango miji za wizara ya ardhi, hizo nyumba na maeneo hayako kwenye Road Reserve.

3. Kwa mujibu wa wizara ya ardhi, eneo qualifying kuwa road reserve ni kati ya mita 30 hadi 60 kutoka katikati ya barabara. hii pia iko katika sheria zilizotumika na kuendelea kutumika kuhusu maeneo.

4. TanRoads (iliyoanzishwa 2000s) inadai kuwa road reserves ni mita 120 kutoka katikati ya barabara ambayo nikutokana nasheria ya barabara ya mwaka 1926/27.

5. Marekebisho kadhaa ya sheria ya barabara yameshafanyika tangu tupate uhuru na ndio maana Wizara ya ardhi, manispaa wanatumia sheria mpya na kuhusisha maeneo katika mipango miji.

6. Barabara ya Morogoro,eneo la Ubungo mpaka KImara mjini, TanRoads imetumia upana wa mita 30 na wakati wa kujenga mwendo kasi ikapanua mpaka mita 45 kutoka katikati ya barabara. Maeneo kutoka KIbaha kuelekea Chalinze, Tanroads inatumia sheria ya sasa ya mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande.

7. Bomoabomoa inayozungumziwa leo ni kutoka KImara Mjini/StopOver mpaka Kiluvia na TanRoads wanadai eneo la mita 120 kutoka katikati ya barabara (pande zote mita 120!)

8. Shauri hili lilishapelekwa mahakamani miaka iliyopita na TanRoads ilishindwa kesi. Hata wakati Waziri wa Ujenzi kati ya mwaka 2000 -2015 alipojaribu kung'ang'ania sheria ya mwaka 1927, si mahakama pekee, bali hata sheria za barabara na baraza la Mawaziri liliafiki kuwa ukubwa wa mwisho ni mita 60 kutoka katikati ya barabara kwa pande zote (jumla upana mzima mita 120). Hili linahitaji uchambuzi wa zaidi pamoja na kumbukumbu husika kuthibitisha hivyo.

9. Inasemekana kuwa miaka ya mwisho ya 90, kwenye mpango wa upanuzi wa barabara hii, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (WB/IMF) waliipa Serikali fedha za fidia kwa watakaolazimika kuhama maeneo yatakayo bomolewa kwa kufanya tathmini ya nyumba, majengo na mali zilizoko kwenye eneo litakaloathirika. Mpaka sasa hakuna mkazi ambaye imethibitika alipatiwa kiwanja kipya cha kuhama na kupewa fidia mali yake kubomolewa na hakuna kumbukumbiu kuonyesha malipo haya yalifanyika vipi.

10. Bomoabomoa ya sasa inafanywa na TanRoads mkoa wa Dar. Inasemekana ngazi zote zilizoulizwa(mawaziri Tamisemi,Ardhi,Ujenzi,TanRoads na hata Waziri Mkuu)kila mmoja inarusha mpira kwa mwenzake na vidole vinaelekezwa mamlaka ya juu ya Mkoa na Nchi.

11. Serikali kutokana na kauli inayosemekana ni ya Rais, inasema haitatoa fidia wala kutoa maeneo mapya kwa waathirika(inabidi kuthibitishwa kama ni kweli).

12. Barabara kuu ya kuingia Dar, imebadilishwa katika mipango ya barabara kuu na kuhamia upande wa Daraja la Kigamboni na highway kuu mpya imeshaanza kukwanguliwa miaka kadhaa iliyopita na itapita pembeni ya mji mpaka Ruvu au Chalinze kwenye maeneo ambayo yako wazi na hayana watu na gharama ni nafuu ukizingatia hakutakuwa na haja ya kubomoa au kutoa fidia kwa watu watakaoathirika kwa kiwango cha kutoka Ubungo pale Sam Nujoma na Morogoro road zinapokutana mpaka Ruvu.

13. Inasemekana mpango wa kupanua barabara hii kutoka Ubungo uko hati hati kutokanana kukosekana kwa fedha na kipaumbele kupelekwa maeneo mengine ya nchi yananayohitaji upanuzi wa barabara, fedha na kipaumbele kuwekwa barabara ya kutoka daraja la kigamboni, fly over za Tazara na Ubungo, Daraja jipya kutoka Aga Khan mpaka Coco Beach, Bandari ya Bagamoyo, Reli mpya na miradi mingine ya miundo mbinu nchini. Mradi unasemekana umesimama kwa kati ya miaka mitano hadi saba na hivyo kuweza kutoa fursa njema kwa mipango inayoeleweka kufanyika ikiwa na kuwapa wakazi watakaoathirika maeneo mapya ya kuhamia na fidia.

Kwa kutazamo hayo mambo 13 niliyataja hapo juu, ni wazi kuna ulazima wa jambo hili kufanywa kwa umakini, haki na kuthamini utu na si kufanyiwa upambe na ushabiki wa kisiasa.

Tafakari ni waathirika wangapi na kiasi gani kitatumika kutoa fidia au hata kufanya zoezi la ubomoaji.
 
Kuna x nyingi znawekwa Kwa majengo ya wat ktk Barbara ya morogoro..wanadai 125m..nyumba lazma ibomolewe..je ni kwl mradi huu upon? Je mradi huu utacover hzo meter? Wenyekua Dar tupen hbr kamili
 
Mita 121 toka katikati mwa barabara kila upande? Kwa hiyo barabara ina upana wa mita 243?

Nadhani anayetafutwa ni gwajima tu.
 
Barabara ya Morogoro road ina buffer zone kubwa sana, kwa hali hiyo vilio vitakuwa vyingi mno!
 
Back
Top Bottom