BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa ya kuanza kwa kazi ya kuunganisha kituo cha kupoza umeme cha Chalinze kitakachopokea umeme kutoka Bwawa la Nyerere na Gridi ya Taifa kwenye njia ya msongo wa kilovoti 220 inayoanzia Kinyerezi hadi Morogoro.
TANESCO imesema Kazi hii itakapokamilika itawezesha kupeleka umeme wa Gridi kwenye Mitambo ya Umeme ya Bwawa la Nyerere (JNHPP) kwa ajili ya kuanza majaribio ya mitambo hiyo “Kuanza kwa zoezi hili ni mafanikio makubwa kwa Shirika, na Taifa kwa ujumla kwani tumeweza kuanza mwezi mmoja kabla ya muda uliokuwa umepangwa awali”
“Zoezi hili lililoanza leo tarehe 01 Disemba 2023 litafanyika kwa siku 10 na kukamilika tarehe 10 Disemba 2023, awali zoezi hili lilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Disemba 2023 lakini kuongezeka kwa kasi ya utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere kumewezesha majaribio kuanza mapema zaidi”
“Aidha, kipindi zoezi hili linapoendelea kutakuwa na athari za kutokupatikana umeme katika baadhi ya maeneo yaliyounganishwa na Gridi ya Taifa, kwani njia hiyo ya umeme italazimika kuzimwa kwa siku hizo”
“Kuanza kwa kazi hii ni katika hatua za ukamilishwaji wa Bwawa la Nyerere ambalo litasaidia sana kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa makali ya mgao wa umeme, hatua nyingine zitakazofuata baada ya kukamilisha zoezi hili, zitakuwa za kuunganisha kituo hicho na njia ya kusafirisha umeme kutoka Luguruni, Dar es Salaam hadi Morogoro, kuunganisha kituo na njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Ubungo Dar es Salaam, na hatimaye njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze kwenda Tanga, kukamilika kwa hatua hizi zote itapelekea kituo kuwa tayari kupokea na kuingiza umeme wa Bwawa la Julius Nyerere kwenye Gridi ya Taifa, tunaomba radhi kwa
usumbufu utakaojitokeza”