Ziwa Nyasa ni milki halali ya Malawi

nyembeason

Member
May 4, 2009
44
21
Sote tunajua kuwa Malawi wamesema ziwa Nyasa, ambalo kwa Malawi linaitwa Ziwa Malawi, ni mali yao na Tanzania haina hata tone moja la maji. Mazungumzo yanayoratibiwa na Tanzania yameshindwa kubadili msimamo wa Malawi. Malawi imejiandaa kwenda mahakamani ya kimataifa, ICJ, kutafuta suluhu ya kile wakisemacho. Uwezekano wa kushinda kesi ni mkubwa, tena mkubwa sana.

Malawi ina ushahidi wa kutosha kuhusu wasemalo: mkataba wa Heligoland 1890 kati ya Mjerumani na Mwingireza uliipa Uingereza (Malawi kwa sasa) ziwa lote. Mjerumani (Tanganyika/Tanzania) iliachiwa Heligoland na makoloni mengine Afrika ya Magharibi.

Kuna ushahidi wa kutosha pia kuwa waziri mkuu wa Tanzania, kwa wakati huo, Kawawa, aliwahi kutoa matamko Bungeni, mara nyingi tu, kuwa Tanganyika/Tanzania haina hata tone moja la maji katika ziwa Nyasa/Malawi. Kwa maneno mengine ziwa Nyasa au Ziwa Malawi ni mali ya Malawi.

Ni mhimu kujua kuwa maneno/matamko yanayotolewa na viongozi wa serikali ya nchi husika, kwa sheria za kimataifa, yanahesabiwa kuwa ni sera ya nchi na hivyo huibana nchi anakotoka kiongozi aliyetoa maneno/matamko hayo. Kwa wafuatiliaji wa mambo, angalia kesi zilizoamuliwa na mahakama ya mbalimbali za kimataifa hasa ICJ. Kuna kesi tatu mhimu kwenye hili: Tamko la Ihleni (Ihlen Declaration), kesi ya Peninsula ya Bakassi na Matamshi ya mwakilishi wa Marekani katika WTO. Kesi mbili za mwanzo ziliamuliwa na mahakama ya kimataifa ya ICJ.
(Pakua na Soma zaidi....liliandikwa siku nyingi)

=========

Tanzania kubaki na Ziwa moja tu-Eyasi: Membe lazima awajibike sasa kwa kauli zake

Tanganyika/Tanzania, kwa muda mrefu, kupitia kwa Mwl Nyerere, ilikuwa na sera ya kutokutambua mikataba ya kimataifa iliyoingiwa na wakoloni kwa niamba ya makoloni yao mpaka Tanganyika/Tanzania huru iwe imeridhia au kuipitia upya (The Nyerere Doctrine of selective succession of treaties). Sera hii ilitumika sana na mataifa mengine Afrika.

Mikataba aliyoikataa Nyerere in pamoja na wa Heligoland (the 1890 Heligoland treaty au The Ango-German treaty au Zanzibar treaty), ulioipa Malawi ziwa lote la Nyasa/Malawi na Mkataba wa maji ya Mto Nile (the 1929 Nile waters Agreement) kati ya Misri na Uingereza(kwa niaba ya Tanganyika, Kenya, Uganda) ambao uliipa Misri umiliki wa Maji ya Mto Nile na vyanzo vyake vyote. Kwa lugha rahisi, Ziwa Victoria ni mali ya Misri. Hakuna nchi inayoruhusiwa kutumia maji ya Mto Nile/ziwa Victoria bila idhini ya Misri.

Tanzania/Tanganyika, chini ya viongozi wazalendo, wenye kufikiri kwa kutumia vichwa, ilisema waziwazi kuwa hawautambui mkataba huu wa Misri na Uingereza. Lowasa, waziri wa maji miaka ya nyuma, pia alikataa hili pamoja na serikali ya Mkapa. Tukajenga mradi wa maji safi ya kunywa kwa mikoa ya kanda ya ziwa. Kumbuka, maji ni shida kubwa Tanzaniahivi sasa kabla ya mabadiliko ya tabia nchi yanayokuja (climate change). Watanzania mamilioni hawana maji ya kunywa.

Hivi majuzi, Tanzania kupitia kwa waziri wa mambo ya nje, Benard Membe, imeripotiwa kukubali kuwa Misri ina haki maalum ya umiliki wa maji ya mto Nile (Ziwa Victoria), hivyo nchi zingine ziheshimu hili. Ziache kutumia maji bila idhini ya Misri na Misri iwe na upendeleo maalum. Nchi zingine zote, Kenya, Uganda, DRC, Burundi, Sudan ya kusini (Juba), Sudan (Khartoum) na Ethiopia zimekataa upuuzi huu.

Waziri Membe ametoa sababu kuwa Tanzania na nchi zingine zina vyanzo wa maji, hivyo waipe Misri hati miliki ya maji ya mto Nile/Ziwa Victoria . Kwa maana nyingine watanzania wanayo maji ya kutosha na hawahitaji maji ya ziwa Victoria. Msimamo wa Membe, kimataifa ni sheria na unaibana Tanzania. Tazama mifano niliyotoa hapo juu.

Pili Membe anadai nchi hizi zina mvua za kutosha. Hii ni sababu ya kiongozi mwenye maono mafupi, asiyejali watanzania na asiyefaa hata kuwa baba wa familia. Nani hajui mabadiliko ya Tabia nchi (Climate change? Nani hajui ukame unaoikumba Tanzania kwa sasa? Nani hajui mvua hazitabiriki? Nani hajui Tanzania inahitaji kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia maji ya baridi ya Ziwa Victoria?

Membe anapaswa kuwajibika mapema iwezekanavyo. Serikali imegawa madini, ardhi, mbuga za wanyama, mapori na sasa imehamia kwenye maji! Hili halikubaliki. Membe awajibike. Haiwezekani watanzania ambao maji yapo kwao wafe kwa ukosefu wa maji kwa ujinga wa aina. Haikubaliki katu. Ni wakati wa waziri Membe kuacha hizi porojo za kuua nchi na watu wake.

Misri inatumia maji kwa umwagiliaji na kulisha watu wake na kuuza pamba duniani kwa wingi. Imeanzisha miradi ya umwagiliaji jangwani. Wanavuna mabilioni ya dola kwa mwaka. Watanzania wanakufa kwa ukosefu wa maji.

Tupo mbioni kupoteza Ziwa Nyasa, Ziwa Victoria limeshapotea, Tanganyika DRC wakisema lao tumeliwa. Tutabaki na Ziwa Eyasi tu.
 
Attachments

  • Tanzania-kubaki-na-Ziwa-moja-tu.doc
    48 KB · Views: 131
Kubaki na ziwa moja nilidhani utasema lolote kuhusu Victoria na Tanganyika!
 
Sote tunajua kuwa Malawi wamesema ziwa Nyasa, ambalo kwa Malawi linaitwa Ziwa Malawi, ni mali yao na Tanzania haina hata tone moja la maji. Mazungumzo yanayoratibiwa na Tanzania yameshindwa kubadili msimamo wa Malawi. Malawi imejiandaa kwenda mahakamani ya kimataifa, ICJ, kutafuta suluhu ya kile wakisemacho. Uwezekano wa kushinda kesi ni mkubwa, tena mkubwa sana.

Malawi ina ushahidi wa kutosha kuhusu wasemalo: mkataba wa Heligoland 1890 kati ya Mjerumani na Mwingireza uliipa Uingereza (Malawi kwa sasa) ziwa lote. Mjerumani (Tanganyika/Tanzania) iliachiwa Heligoland na makoloni mengine Afrika ya Magharibi.

Kuna ushahidi wa kutosha pia kuwa waziri mkuu wa Tanzania, kwa wakati huo, Kawawa, aliwahi kutoa matamko Bungeni, mara nyingi tu, kuwa Tanganyika/Tanzania haina hata tone moja la maji katika ziwa Nyasa/Malawi. Kwa maneno mengine ziwa Nyasa au Ziwa Malawi ni mali ya Malawi.

Ni mhimu kujua kuwa maneno/matamko yanayotolewa na viongozi wa serikali ya nchi husika, kwa sheria za kimataifa, yanahesabiwa kuwa ni sera ya nchi na hivyo huibana nchi anakotoka kiongozi aliyetoa maneno/matamko hayo. Kwa wafuatiliaji wa mambo, angalia kesi zilizoamuliwa na mahakama ya mbalimbali za kimataifa hasa ICJ. Kuna kesi tatu mhimu kwenye hili: Tamko la Ihleni (Ihlen Declaration), kesi ya Peninsula ya Bakassi na Matamshi ya mwakilishi wa Marekani katika WTO. Kesi mbili za mwanzo ziliamuliwa na mahakama ya kimataifa ya ICJ.
(Pakua na Soma zaidi....liliandikwa siku nyingi)

Hiyo kesi hata kama TZ tusiposhiriki kabisa Malawi hawezi kushinda kwa maana International law iko wazi kwamba vitu kama Mto, Ziwa, Milima n.k. inapokuwa mpakani baina ya nchi basi ni lazima zimilikiwe na nchi hizo, hiyo ni international law, hivyo hapo Malawi wanajisumbua tu hiyo kesi hawawezi kushinda hata iweje, na sababu ni haki za kibinadamu kwa maana kama unasema Ziwa Liko Malawi vp watu wanaoishi ufukweni wakitaka kuogelea waombe viza Malawi?
 
Barbarosa, nakuhakikishia-....hatushindi. Soma article yangu/research hii hapa!
 
Attachments

  • Research Topic Final.doc
    148 KB · Views: 99
Sote tunajua kuwa Malawi wamesema ziwa Nyasa, ambalo kwa Malawi linaitwa Ziwa Malawi, ni mali yao na Tanzania haina hata tone moja la maji. Mazungumzo yanayoratibiwa na Tanzania yameshindwa kubadili msimamo wa Malawi. Malawi imejiandaa kwenda mahakamani ya kimataifa, ICJ, kutafuta suluhu ya kile wakisemacho. Uwezekano wa kushinda kesi ni mkubwa, tena mkubwa sana.

Malawi ina ushahidi wa kutosha kuhusu wasemalo: mkataba wa Heligoland 1890 kati ya Mjerumani na Mwingireza uliipa Uingereza (Malawi kwa sasa) ziwa lote. Mjerumani (Tanganyika/Tanzania) iliachiwa Heligoland na makoloni mengine Afrika ya Magharibi.

Kuna ushahidi wa kutosha pia kuwa waziri mkuu wa Tanzania, kwa wakati huo, Kawawa, aliwahi kutoa matamko Bungeni, mara nyingi tu, kuwa Tanganyika/Tanzania haina hata tone moja la maji katika ziwa Nyasa/Malawi. Kwa maneno mengine ziwa Nyasa au Ziwa Malawi ni mali ya Malawi.

Ni mhimu kujua kuwa maneno/matamko yanayotolewa na viongozi wa serikali ya nchi husika, kwa sheria za kimataifa, yanahesabiwa kuwa ni sera ya nchi na hivyo huibana nchi anakotoka kiongozi aliyetoa maneno/matamko hayo. Kwa wafuatiliaji wa mambo, angalia kesi zilizoamuliwa na mahakama ya mbalimbali za kimataifa hasa ICJ. Kuna kesi tatu mhimu kwenye hili: Tamko la Ihleni (Ihlen Declaration), kesi ya Peninsula ya Bakassi na Matamshi ya mwakilishi wa Marekani katika WTO. Kesi mbili za mwanzo ziliamuliwa na mahakama ya kimataifa ya ICJ.
(Pakua na Soma zaidi....liliandikwa siku nyingi)

Kama umetumwa nenda kawaambie tunasema, wacha ziwa tu, tutaichukuwa Malawi yote iwe himaya ya Tanzania na kama mnabisha mwende mkawaulize Uganda.
 
Nimesikia kuna mafuta wa Waingereza ndiyo shinikizo usiniulize source.
Lipo wazi hilo. Issue ilianzia hapo baada ya kampuni ya UK kuanza kurusha ndege ziwani wakifanya survey. Tz ikasema itazitungua. Ilibidi waache kwanza!
 
Back
Top Bottom