Ziwa Nyasa halipo tena Tanzania

Ziwa Nyasa halipo tena Tanzania

sinajinasasa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
2,989
Reaction score
4,169
Mgogoro wa mpaka wa Malawi na Tanzania bado unafukuta sana. Sasa hivi ziwa Nyasa linaitwa ziwa Malawi na limeisha anza kuingia kwenye Ramani mpya za Dunia. Hata ukiangalia kwenye google map mpaka unaonyeshwa unapita pembezoni mwa Songea maana yake hata maji tunayotumia watanzania toka ziwani ni ya Malawi.
Hii vita ya rasilimali lazima ije, sidhani kama JPM atakubali hawa jamaa watunyang'anye nchi yetu. Kadri rais wetu anavyojitahidi kuijenga nchi vizuri wapo wageni wanataka tuwe masikini ili wachukue rasilimali.

Capturemal.PNG
Capturemal.PNG
 
umeona wapi hilo?embu tupe source kwanza
 
Sina wasiswasi na jeshi letu pindi itakapofikia uamuzi wa kuidabisha kwa nia ya kurejesha mipaka yetu.
 
kwanza nani kakwambia hatuna tena sehemu ya hilo ziwa Nyasa? umesoma habari hiyo kutoka chombo cha Malawi unategemea nini? halafu huo mgogoro sio mpya wewe ndio umechelewa kupata taarifa ulikuwa hujui kwa hiyo unaona kama taarifa ya jana. mgogoro upo, tena wa mda na hilo linajulikana kimataifa na ziwa tunalitumia kama kawaida, na hata mazoezi ya kijeshi tushafanya kwenye hilo ziwa. kwa hiyo usipotoshe kuwa eti tumepokonywa. Hizo ramani hata ukiingia google( achana na source ya Malawi) wanakuonesha kuwa mpaka una mgogoro
 
Hebu kumbuka vita ya Uganda, mgambo walienda vitani wanajeshi hawakutosha, vijana walijitolea kwenda vitani, hivyo ikitojea vita jiandae. Idd Amini alitumiwa kuharibu uchumi wetu mzuri, hivyo naamini spidi ya Magufuli wazungu hawaipendi, wamepata chanzo cha kutuharibia kwa kutumia mgogoro wa mpaka.
 
Source sio Malawi...nilikuwa nafuatilia Ramani ya visiwa vya Malawi vilivyopo Msumbiji nikaona mpaka ulivyopita. Mbona ramani za zamani hazionyeshi mpaka upo hadi Songea?
 
Mgogoro wa mpaka wa Malawi na Tanzania bado unafukuta sana. Sasa hivi ziwa Nyasa linaitwa ziwa Malawi na limeisha anza kuingia kwenye Ramani mpya za Dunia. Hata ukiangalia kwenye google map mpaka unaonyeshwa unapita pembezoni mwa Songea maana yake hata maji tunayotumia watanzania toka ziwani ni ya Malawi.
Hii vita ya rasilimali lazima ije, sidhani kama JPM atakubali hawa jamaa watunyang'anye nchi yetu. Kadri rais wetu anavyojitahidi kuijenga nchi vizuri wapo wageni wanataka tuwe masikini ili wachukue rasilimali.
Maandalizi ya bongo movie nyingine? Maana ya Lipumba naona inaelekea ukingoni
 
Mkuu kitambo ukipita Malawi satelite za pale katika Goggle map linatambulika kama Lake Malawi na wamalawi wote wanalitambua hivyo na si Nyasa huku Tanzania ndio tunalitambua hivyo Ziwa Nyasa..
 
Kushinda tutashinda kwa sababu tangu zamani dunia nzima na hats Afrika inajua kabisa kuwa ziwa Nyasa ni la kwetu.
Malawi ilivyoona tuna utajiri wa rasilimali ya ziwa Nyasa na kulitumia tujtajurishe hatuwezi,wakaona bora watumie hila wajaribu bahati yao ya kujitajirisha na wao.
 
Wamalawi wenyewe washaambiwa wawe wapole tu maana tutawachapa wakileta figisufigisu za ajabu ajabu
 
Hebu kumbuka vita ya Uganda, mgambo walienda vitani wanajeshi hawakutosha, vijana walijitolea kwenda vitani, hivyo ikitojea vita jiandae. Idd Amini alitumiwa kuharibu uchumi wetu mzuri, hivyo naamini spidi ya Magufuli wazungu hawaipendi, wamepata chanzo cha kutuharibia kwa kutumia mgogoro wa mpaka.
Unadhani wazungu wana mawazo "MFU" kama yako "u have died idea" ndo maana tunaitwa nchi maskini kwa kuishi na watu kama wewe.
 
Mgogoro wa mpaka wa Malawi na Tanzania bado unafukuta sana. Sasa hivi ziwa Nyasa linaitwa ziwa Malawi na limeisha anza kuingia kwenye Ramani mpya za Dunia. Hata ukiangalia kwenye google map mpaka unaonyeshwa unapita pembezoni mwa Songea maana yake hata maji tunayotumia watanzania toka ziwani ni ya Malawi.
Hii vita ya rasilimali lazima ije, sidhani kama JPM atakubali hawa jamaa watunyang'anye nchi yetu. Kadri rais wetu anavyojitahidi kuijenga nchi vizuri wapo wageni wanataka tuwe masikini ili wachukue rasilimali.
Mkuu vipi kulikuwa na tetesi kuwa yule rais wa huko hajulikani alipo vipi keshaonekana??
 
Daah nlitaka kubisha bila kufanya uchunguzi..hakika malawi wanamtafuta JPM....ziwa lote wamelichukuwa sasa hapa ndo mda muafaka wa kutumia yale mabomu yetu
 
Back
Top Bottom