Zitto umewadhalilisha Wabunge wa Viti Maalum CDM; Waombe Radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto umewadhalilisha Wabunge wa Viti Maalum CDM; Waombe Radhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tambara Bovu, Jul 12, 2011.

 1. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimefuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea hapa JF uliokuwa ukijadili kuhusu Zitto,JK VS gazeti la tanzania daima na mmiliki wa gazeti hilo amabye ni Mbowe. Kuna mengi yamesemwa lakini lililoniku na hili la huyu Naibu Katibu Mkuu wa CDM Zitto Kabwe.Katika kujitetea na kuhamishia lawama kwa wenzake kiongozi huyu ninayemuamini miaka yote tangu nimemfahamu amewadhalilisha na kuwadharau wanachama wapya wa CDM.Naomba ninukuhuu maneno yake hapa chini wakati akimjibu mchangiaji mmoja kwenye ile thread.

  [Ha ha ha ha ha ha. Kwi kwi kwi! Unanifanya nicheke kijuha **** na maneno yako.Chadema ni chama cha kidemokrasia na kitabaki hivyo. Sisi tulio ndani ya chama hiki toka kianze ndio tunajua utamaduni wa chadema. Wewe kwa kuwa ni wa kuja na ukazawadiwa ba Ubunge lazima useme hayo unayosema.Napenda nirudie kusema sina umri wa kugombea Urais kwa sasa. Nitamwunga mkono mgombea Urais wa CHADEMA atakayepitishwa ba vikao vya chama wakati utakapofika. Kwa sasa hakuna mgombea Urais CHADEMA na mie wala sioti kuwa mgombea. Kama uropokaji huu unatokana na Urais, mie simo. Kwamba sitaweza kuwa kama ningekuwa nina vigezo, unajidanganya tu na unajua unajidanganya. Chadema ni wanachama. Bring a free and fair election uone! ]

  maneno haya ni ya dhihaka kubwa na hayakupaswa kuongelewa na kiongozi kama yeye tegemeo la taifa kwasababu zifuatazo
  1. Zitto unaposema kuwa yeye ni mwananchama wa siku nyingi na wenzake ni wakuja ni dharau kubwa kwa wanachama wapya.Anamaanisha kuwa wanachama wazamani ndio wanajua zaidi utamaduni wa chama kuliko wapya na hawastahili kuhoji ukiukwaji wa tamaduni hizo zinapofanywa na wanachama wa zamani.Zitto unapaswa kuwaomba radhi wanachama hawa wapya.

  2. Zitto unaposema kwa huyo aliyekujibu kuwa ni wakuja na amezawadiwa Ubunge ndio maana akaksema livyosema unamaanisha kuwa Wabunge wa CDM wamezawadiwa viti maalum-kauli hii ikitoka kwa kiongozi kama wewe maana yake ni kuwa vitimaalum CDM ni zawadi na hivyo waliopata wamepewa zawadi.Unatumaanisha nini sisi tuliogombea nahatukabahtaika kupata nafasi hizo?kuwa kumbe wenzetu walipewa zawadi?nilikuwa mgombea kwenye mchakato ule na baadaye tulitangaziwa vigezo kuwekwa ili watu wapite kwa vigezo ili kuepusha rushwa iliyotaka kufanyika aabayo iliasisiwa na wewe ndani ya chama,ulitumia pesa nyingi sana ili watu wako washinde. Zitto acha kupotosha umma,usikiharibu chama chako unapaswa kukijenga.Maneno kama hayo hayapawsi kusemwa na mtu kama wewe,ulishiriki kwenye mchakato wa kuwapata,unajua vigezo,mama yako alikuwepo kwenye kamati,rafiki yako Dk Kitilla alikuwa Mwenyekiti wa Kamati.Tueleze hawa wabunge walizawadiwaje?je ni mama yako,ni wewe,ni Kitilla,ni Dk Slaa,ni Mbowe tuambieni na sisi ambao hatkupata ili mwaka 2015 tujipange vizuri.

  Zitto unapaswa kuomba radhi wabunge hawa waliopita kihalali kwa vigezo.

  Nawasilisha.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  alikuwa anamjibu nani kwenye hiyo post?
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  FL nadhani hauna uhusiano wowote na kigeugeu Shibuda?
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  zitto hata kama umri ungeruhusu hana sifa za kugombea urais kupitia CDM LABDA ccm au NCCR.

  zitto anataka kumaanisha KITILIA NKUMBO alitoa upendeleo ???? Zitto,Zitto kuna siku utauza watanzania
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huyu sio FL1....
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  FL jibu basi........alitoa huo uharo wakati akijibu post ya nani?
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  zitto ni pekee katikachadema

  waliobaki ni wafitini na majungu na kwa mchezo wao wataiua chadema
   
 8. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  The whole "viti maalum" circus ni mzigo kwa taifa, hawakutakiwa kuwepo.
   
 9. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  1. Kwanza sioni tatizo la hiyo kauli ya Mh. Zitto (Red color)
  2. Pili ni kweli kila pahala kuna utamaduni wake (Blue color) ambapo kitalaamu huitwa corporate culture, kwa mtu yeyote kama ni mgeni unapoingia sehemu (mfano mazingira mapya ya kazi ktk kampuni mpya) huwa kuna muda wa kujifunza, ndiyo maana mtu mwenye akili timamu na msomi hubidi kuwa mpole anapoingia mazingira mapya na huwa msikilizaji zaidi kabla ya kuropoka ropoka. Mfano mzuri ni wewe na mimi unapoleta mtu wa kuishi naye nyumbani kwako (mfano mtumishi wa ndani) asipokuwa mpole kuizoea culture ya hapo nyumbani na kuanza kuropoka ropoka basi utamtimua na kumuita anatabia mbaya na wale waliopo tangu mwanzo watamshangaa.
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kamanda mbona un-EDIT QUOTE? Anywayz: Kwani unadhani FL ana uhusiano wowote na Shibuda?
   
 11. RR

  RR JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Viti maalum vyenyewe ni udhalilishaji.......
   
 12. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280

  merytina ambaye amepewa ubunge wa viti maalum
   
 13. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  mh, siasa ni shida tu.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hata mimi sioni ubaya wa maneno ya Zitto..
  Watanzania tuna ustaarabu wetu wa lugha na matumizi yake. Majibu yalikuwa safi kabisa kwa mhusika kwani aloanza maneno haya sii Zitto. Nachopenda na kufurahia ni uwezo wa viongozi wa Chadema kuwa mbele ktk kujibu maswali na unapoleta uhuni unapewa dawa! Na nampenda Zitto kwaq kutomung'unya maneno. Ujasiri na kiburi chake kinahitajika sana na hakika tunamuhitaji mtu kama yeye ktk nafasi muhimu.

  Mbunge wa viti maalum ni kuzawadiwa hilo halina ubishi tena kama umejiunga hivi karibuni ndio kabisa inatakiwa ukae kimyaa maanake hujui! na kutojua sii tusi bali ni usia mzuri kwa viongozi wageni wapate kujifunza kuheshimu viongozi wao. Zitto ni naibu katibu wa chama, na lugha inayotumiwa na baadhi ya vijana wa Chadema hapa JF nadhani inavuka mpaka wa heshima wakati wao wamemkabidhi mamlaka hayo..
   
 15. k

  kiloni JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kila siku unadandia hoja unaweka mashiko ya plastic halafu unaleta kwenye moto unategemea nini!? Itayeyuka bila shaka.
  Ukitumwa na CC Magamba kugombanisha CDM kaa tulia kidogo uweze kupika angalau viive pole weye.!!!!
   
 16. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kweli hujui ulisemalo.

  Mbona hukuweka shutuma personal zilizotolewa kwa Zitto tena na mheshimiwa mbunge wa viti maalum? Au kuwa mbunge wa viti maalum one can
  behave the way they want? Safi sana Zitto, Shutuma za chooni unazipa majibu ya chooni.
   
 17. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kila anapoguswa Kiongozi wa Cdm basi huyo mtu ametumwa na Magamba acheni ujuha fungukeni vijana.
   
 18. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Sioni matusi katika kauli ya Zitto kama ni kweli aliyasema hivyo. Ninachokiona ni kwamba mtoa mada anafanya attack tu kwa Mh huyu!
   
 19. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Pamoja na weakness zake lakin watu kama nyie hamumuwez kwa hoja,ukweli ndio unamata hapa,zito kanena point za msingi.
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Kila siku napinga wabunge wa vita maalum ni ubunge wa kupewa Zitto umesema kweli
   
Loading...