..wanawake ni zaidi ya asilimia 50% ya raia wote wa Tanzania. lakini ukiangalia uwakilishi wao ktk maeneo mbalimbali mfano elimu, biashara kubwa, nafasi za uongozi,umiliki wa ardhi, uwakilishi bungeni, etc etc unaona kuwa wanaume ndiyo wamejaza nafasi nyingi. suala ni kujiuliza ni kwamba, tutaweza vipi kuwainua mama zetu,dada zetu, binti zetu, ili nao waweze kupata mafanikio[have an equal share of the national cake] kama yale waliyonayo wanaume?
Mkuu equal share haiwezi kufumbuliwa kwa kuongeza hesabu kubwa ya wabunge wanawake...
Mkutano wa Beijin, haukuwa na maudhui haya ila wanawake wamekuwa WAKINYIMWA nafasi za uongozi na zipo nchji nyingi duniani hata kusimama kugombea hawaruhusiwi. Kuwezeshwa kulikozungumziwa ni kuondokana na mila za mfumo dume ambao umewadhalilisha wanawake kwa karne nyingi zilizopita na message ya msingi ilotoka ni kwamba wanawake wana uwezo mkubwa au sawa na wanaume ktk utekelezaji wa kazi na haki yao kupokea mishahara sawa na wanaume.
Nadhani hadi sasa hivi Canada na nchi za Nordic ndizo haziweki tofauti ya mishahara kati ya wanaume na wanawake ktk kazi moja na nasema bila kumung'unya maneno Tanzania pia ni moja ya nchi za kiafrika ambayo haina migogoro ya utoaji ajira na mishahara. Hivyo kuhudhuria kwetu mkutano wa Beijin hautupi nafasi ya kutafuta sababu nyingine nje ya kile kilichokusudiwa.
Aidha mkutano huo uliwaamsha wanawake kudai haki hizi na kujitokeza kugombania nafasi ktk uongozi, ajira na maswala mengine ambayo walidhalilishwa kwa sababu ya uke wao. Kwa nini wanawake hawapo wengi bungeni kwetu?.. jiulize ni wangapi hujitokeza kama sii kwamba bado wamefunikwa na utumwa wa kimila kumtumikia mwanaume.... Mkoa wa Tabora sidhani kama una mbunge au Diwani hata mmoja na mwanamke, na sii kwamba wananchi wanashindwa kuwachagua isipokuwa hawajitokezi kutokana na utumwa wa mila zetu. Sheria inawaruhusu lakini bado wao wanataka kuiwezeshwa kwa kupitia viti maalum. na kikubwa zaidi ubunge nchini unahitaji uwe na mtaji mkubwa wa kifedha, hili lingeangaliwa na kupatiwa ufumbuzi.
Elimu ya uraia kwa wanawake inatakiwa kuongezwa hivyo vyanzo kama Taasisi ya kuwawezesha wanawake ndio ziundwe na zipate uwakilishi bungeni. Tuna Umoja wa Wanawake (UWT) badala ya kudeal na wanawake WOTE NCHINI ina deal na maMbo ya chama CCM, kuhamasisha wanawake wajiunge na CCM...tena inaelekeza nguvu zake zote ktk uwekezaji kwa wanachama wa CCM ambao hawafiki hata asilimia 1 ya wanwake nchini, hao waliobakia nje watafute pa kutokea.
Sasa kama tuna nia njema tuvunje Umoja wa wanawake na iundwe taasisi ambayo itawakilisha wanwake wote nchini na hata wapewe wabunge 10 wa kuteuliwa na wanawake wenyewe ktk taasisi zao ni bora zaidi kuliko huu mfumo dume ambao pamoja na kuwepo hivi viti maalum bado ni wanaume wanaochagua kina nani wapewe nafasi hizo..
Mfumo dume ni - Nguvu ya mamlaka alopewa mwanaume kufanya maamuzi ambayo yanamhusu hata mwanamke!