Zitto, Ulimwengu, Shivji na Jaji Mkuu wa Kenya ndani ya Nkrumah Hall - ITV Live

Zitto: mkituacha sisi wanasiasa tupambane juu ya maendeleo mmekwisha maana sisi wanasiasa nia yetu ni kuchukua madaraka....
 
Mh. Zitto yuko Live kwenye tamasha la Kigoda cha Mwl. Nyerere..........anaongelea Azimio na maadili ya viongozi. Fuatilia............

Mjadala unaendeshwa na Generali Ulimwengu, mbele yuko Zitto na Dada mmoja hivi..wanalumbana lakini kwa hoja

Update:

Ulimwengu anasema Tanzania ni nchi ambayo ina kampeni ya Kilimo kwanza lakini hakuna kiwanda cha kutengeneza jembe, panga au shoka wala mundu.!!!!
Mkuu ahsante kwa uzi huu, vipi Bukoba mvua zinanyesha???

 
Kuna watu wagumu kuelewa.

Kihistoria, kikao kama kile lazima kimaliziwe na kauli kama hizo. Kuanzia mwaka 1992 hali hiyo imebadilika kutokana na kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi.

kingunge kama mwanaCCM mkongwe ameona si sahihi kutoka bila kusema CCM oyee, kwa hiyo ameisema kwa style hiyo kuwa anatambua umuhimu wa kauli hiyo ambayo kwa kadamnasi ile hawezi kuisema.

Kuna watu wako kwenye jitihada za kulifanya embe dodo lionekane andazi, ili wapate kitafunio...
Mkuu vipi mbona sikuelewi, angelisema CCM hoyee kwa kuliuwa azimio la Arusha au kwa kudidimiza uchumi wa nchi yetu na kuzalisha mafisadi?????

 
Tanzania tunaigiza kama Wema Sepetu na mama yake


Jenerali Ulimwengu anasema Tanzania ni nchi ambayo ina kampeni ya Kilimo kwanza lakini hakuna kiwanda cha kutengeneza jembe, panga au shoka wala mundu.!!!!
 
AZIMIO LA ARUSHA lilitayarishwa na viongozi wetu, wakataka maoni yetu, tukaona linafaa na tukaandamana kuwaunga mkono. Pakaja kipindi cha kuwatoa viongozi na kuwaweka watawala ikaonekana Azimio la Arusha ni kikwazo, likaondolewa bila kupata maoni ya wananchi na hivo hakukuwa na maandamano. Sasa pana makongamano/mijadala/maoni mbalimbali kutaka Azimio la Arusha lirejeshwe (nakumbuka hata Umoja wa Vijana wa CCM waliishatoa tamko la kulirejesha). Watawala hawawezi na wananchi wanashindwa kulidai kwa nguvu. Sasa nani alirejeshe????????
 
Prof.Wangwe anazungumzia na kusifia development vision 2015,je huu mpango unatekelezwa kweli?
Nafikiri ni Vision 2025. Anasifia kwa sababu aliusika kuuandaa. Hapana haufuatwi bali ni kwa ajili ya kuonyesha ndoto zetu.
 
Back
Top Bottom