Tukio la tamasha la tano kigoda cha mwalimu nyerere cha umajumui wa afrika udsm kuriwa live itv

Mabulangati

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
796
164
Wadau katika pitapita yangu nimekutana jambo hili jema toka UDSM na ITV/Radio One, nikaona ni vyema kuwashirikisha wana JF.

Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere kinayo furaha kuwafahamisha kuwa kutakuwa na marudio ya matukio siku ya tatu ya Tamasha la tano la Kitaaluma la Julius Nyerere, yatakayorushwa na kituo cha ITV, siku ya Jumamosi , tarehe 20 Aprili 2013 kuanzia saa 4.00 asubuhi (baada ya kipindi cha Watoto Wetu). Matukio hayo ni:
1: Tafakuri ya Dkt. Willy Mutunga, Jaji Mkuu wa Kenya, juu ya ‘“virusi” vya Azimio [la Arusha] bado vinaniandama’ 2: Uzinduzi wa kitabu: Miongozo Miwili: Kupaa na Kutunguliwa kwa Azimio la Arusha (Neno la uzinduzi: Prof. Issa Shivji; Mzinduaji: Dkt. Willy Mutunga) 3: Shairi: “Wape wape Vidonge vyao” na Jenerali Ulimwengu 4: Malumbano juu ya dira ya maendeleo: Azimio la Arusha vs Dira 2025 (Mlumbishaji: Jenerali Ulimwengu, walumbi: Bi. Rehema Tukai na Ndg. Zitto Kabwe) na maswali na michango kutoka kwa washiriki. 5: Maswali na michango kutoka kwa washiriki 6: Shairi: “Mchezo wa Karata”, na Mshai Mwangola 7: Shairi la shukrani na kuwaaga washiriki kutoka kwa Prof. Shivji 8: Shairi la kufunga Tamasha kutoka kwa Prof. Mukandala. USIKOSE KUTAZAMA KIPINDI HICHO CHA KIHISTORIA
 
Back
Top Bottom