Zitto: Tumependekeza kumvua ujaji Mh. Werema

Zitto: Tumependekeza kumvua ujaji Mh. Werema

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
Akihojiwa na mwandishi wa Tanzania Daima, mh. Zitto amesema PAC IMEPENDEKEZA

1. Kuanza mchakato wa kumvua UJAJI MH. WEREMA

2. Kumfikisha mahakamani

3. Wote waliohusika kuwajibishwa kulipa na kisha kupelekwa mahakamani.

Mh. Zitto amedai hii haiwezi kuisha kama EPA,lazima wahusika wafike mbele ya sheria.
 
halafu wewe hukupata chochote huko manake naona siku hizi umeanza kuwageuka magamba wenzio
 
Kuna utaratibu wa bunge kumvua ujaji jaji?

Zitto anaelewa process ya kumvua ujaji jaji Tanzania (in any case) ilivyo cumbersome?

Hii si mihimili miwili tofauti ya dola? I am hoping he is not talking about bunge kumvua ujaji jaji.
 
Najua kwakuwa Werema ni mwanasheria mtaalam, hataonewa kipuuzipuuzi. Ila hoja ya msingi ni kutujulisha sisi wakulima ukweli kuhusu umiliki wa fedha za escrow. Je ni za umma? Kwa vigezo vipi? Si za umma? Napo ni kwa vigezo vipi. Msitupe mapendekezo kabla ya kujibu hoja za msingi.

But najua zitto na Deo ni watu makini. Naamini hawatayasahau haya

akihojiwa na mwandishi wa tanzania daima mh zito amesema PAC IMEPENDEKEZA
1. kuanza mchakato wa kumvua UJAJI MH WEREMA
2. kumfikisha mahakamani
3.wote waliohusika kuwajibishwa kulipa na kisha kupelekwa mahakamani
MH ZITO AMEDAI HII HAIWEZI KUISHA KM EPA LAZMA WAHUSIKA WAFIKE MBELE YA SHERIA.
 
Kwani aliyempa ujaji ni nani? Bunge au Serikali?

anyway kwa serikali hii? labda ingekuwa SOMALIA!!
 
Hiyo kazi itafanywa na wahusika kwa kufuata utaratibu na pia kwa kuzingatia ushauri wa bunge.

Wahusika kina nani?

Ulishawahi kusikia mtu kavuliwa ujaji Tanzania maisha yote ya nchi hii?

Hapa kuna kitu kinaitwa "independence of the judiciary". Mahakama haipelekwi pelekwi kwa amri za bunge tu.

Wahusika ni majaji. Habari nzima kuanzia bungeni tu ishaleta doa. Kuna technicalities kibao za checks and balances hapo, halafu kuna precedent ambayo majaji hawatataka kuiweka.

I give you 95% chance that will not happen.

Ingawa kiukweli kauli za Werema bungeni tu zilitosha kum disbar. Let alone hayo ma scandal.
 
Na wale majaji waliopokea mshiko inakuwaje? Prof wa Kichina atawavua madaraka?
 
akihojiwa na mwandishi wa tanzania daima mh zito amesema PAC IMEPENDEKEZA
1. kuanza mchakato wa kumvua UJAJI MH WEREMA
2. kumfikisha mahakamani
3.wote waliohusika kuwajibishwa kulipa na kisha kupelekwa mahakamani
MH ZITO AMEDAI HII HAIWEZI KUISHA KM EPA LAZMA WAHUSIKA WAFIKE MBELE YA SHERIA.

assadsyria3

Jaribu kumwambia huyo ZITTO KABWE - Actions Speaks Lauder than Words....'

Ameongea sana na kutupa Imani lakini vyote vinapotelea Uvunguni, time for REAL ACTION au ajiuzulu hiyo KAZI
 
Najua kwakuwa Werema ni mwanasheria mtaalam, hataonewa kipuuzipuuzi. Ila hoja ya msingi ni kutujulisha sisi wakulima ukweli kuhusu umiliki wa fedha za escrow. Je ni za umma? Kwa vigezo vipi? Si za umma? Napo ni kwa vigezo vipi. Msitupe mapendekezo kabla ya kujibu hoja za msingi.

But najua zitto na Deo ni watu makini. Naamini hawatayasahau haya

Unapotaka kujua kama ni fedha za umma au sio za umma ungejiuliza kwanza TANNESCO ni shirika la nani ukipata jibu nafikiri upumbavu uliojipachika utauondoa.
 
Huu ni ujinga na hilo. Zito atakuwa naye ana mgawo wake ndo maana anachepusha adhabu
 
zzk namkubali anapiga kazi sio km babu na dj kuropoka tu

Unakumbuka sakata la RICHMOND lilianzishwa na nani na mwisho wake ulikuwaje? na pia sakata la mabilion ya USWISS lilianzishwa na nani na mwisho wake ulikuwaje? ukipata jibu utajua na hili suala la ESCROW litaishiaje.
 
Wakina Zitto wasisahau kupendekeza kuimilikisha IPTL kwa Tanesco . Manake huo mkataba mwingine wa miaka 20 wa Tanesco kulipa Tzs mil 238 IPTL hatuukubali,
 
Back
Top Bottom