MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,604
Hon.MP Mkuu, hata kama angesema hivyo, kuna uwezekano wewe ukawa wa mwanzo kuichambua hiyo sentensi:Au kama kwa hekima yake ambayo inashangaza bado aliona ni lazima kutoa taarifa hiyo ya makabidhiano ambayo Wabunge wengine hawahusiki na wala haiongezi chochote cha maana kwenye hansaRd, kwa nini asingesema tu kuwa ‘nilipewa mchango na Mbunge mwenzetu lakini kwa bahati mbaya nimeshindwa kuusoma' .
- Mwenzao gani huyo aliyempa mchango?
- Kwa nini akashindwa kuusoma - una matusi ndani yake, una shutuma zisizothibitishwa n.k.
Moja ninakubaliana nawe, kuwa bora angenyamaza. Laiti watu wangekuwa wanaandika kwanza yale wanayotaka kuyasema, baadae wakatumia japo dakika mbili kutafakari athari zinazoweza kutokana na kauli zao!
Last edited by a moderator: