Huyo Mkurugenzi aliye kwenye payroll anaingia kwenye kundi la WAFANYAKAZI wote Tanzania ambao ndio hao wanachangia 75% lakini biashara yake inaingia kwenye kundi la biashara zote Tanzania ambazo kwa ujumla wao ndo wanachangia hiyo 25%!
So, hoja ya Zitto, hata huyu Mkurugenzi anaposimama kama Mfanyakazi; nae anastahili kupunguziwa huu mzigo wa PAYE!
Lakini kwa upande wa pili; kama kuna ujanja ujanja huwa anafanya kwenye biashara yake basi aache huo ujanja ujanja na aanze kulipa kodi stahili za biashara zake ili biashara yake yeye na zingine zote Tanzania; wawe wanalipa kodi kubwa zaidi... ili, let's say, ipande from 25% ya sasa to 65%!!
Lakini kama hakuna janja janja yoyote; basi azalishe zaidi na auze zaidi ili hatimae aweze kulipa kodi kubwa zaidi kupitia hiyo biashara!
Of course, kwa hiyo hoja ya mwisho kutimia panahitaji factors zaidi ya moja!
But all in all, hoja ya Zitto inamaanisha jambo moja la msingi: kwamba, mchango wa kodi unaotoka moja kwa moja kwenye mauzo ya makampuni ni mdogo... inawezekana wengi wanakwepa kulipa kodi au ufanisi wa biashara ni mdogo au yote kwa pamoja! Matokeo yake, mlipa kodi mkubwa ni Mfanyakazi kwa sababu yeye hana namna ya kukwepa kodi kama ambavyo Mkurugenzi uliyemtaja anavyofanya kukwepa kulipa kodi stahiki ya biashara yake!
Anything missing?!