Zitto: Rais ni mbaguzi, simple and clear

Zitto: Rais ni mbaguzi, simple and clear

Zitto kachemka Tanzania bara hatuna katiba ya umoja wa kitaifa kama Zanzibar ambayo inaruhusu kuunda serikali ya mseto inayohusisha vyama vingi, kuwa unachukua mtu wa chama chochote na kumuweka katika serikali ya mseto.Serikali inayoshinda inaundwa na wanachama wa chama kilichoshinda ili wakatekeleze ilani ya chama chao.Full stop.

Zitto Asubiri akija kushinda amteue hata waziri mkuu akitaka.Hii ni serikali ya CCM inayotekeleza ilani ya CCM inayotaka mtu atekeleze yaliyomo kwenye ilani bila kinyongo wala kukaa akiota au kuwaza UKAWA au ACT wazalendo
Je vip kuhusu dini mkuu
 
Sasa Zitto alitegemea mwana ACT akatekeleze vyema ilani ya CCM?
Ina maana na wanachama wote wa ACT wasishiriki katika kazi za maendeleo kwa kuwa zinafanywa kwa kutekeleza ilani ya ccm? Sababu viongozi wao wanatengwa, ukisha anza kuteua wana siasa walio simama majukwaani kuomba kula katika nafasi za utendaji tayari ni shida
 
inabidi wateule wetu watukufu waendelee kukumbushwa kuwa kuwapa vyeo watu kwa kutumia tabaka ya aina yoyote ile ni ufisadi tosha kufikishwa kwenye "mahakama mpya" ya mafisadi.

wapi Rev Mtikila (rip)?
 
kwa wale wenzetu kule duniani ambako wameendelea sana na wanajua nini maana ya uwakilishi wa jamiii ktk serikali zao basi leo tanzania ingekua na serikali ya umoja wa kitaifa na hizi fitina nyingi zisingekuapo lakin kwa staili hii ya kutekeleza ilani ya chama safari bado ni ndefu kwa nchi hizi
 
Sasa Zitto alitegemea mwana ACT akatekeleze vyema ilani ya CCM?

Kwa historia ya jinsi Museveni alovyoichukua Uganda, huwezi kuweka kiongozi toka upande wa pili au asiyekua kwenye itikadi au mstari mmoja.

Swali kubwa hapa ni je hawakujua kia aligombea ACT? Hakuna vetting? Majina yanaibuliwaje?
 
Hivi wakikuyu na Waluo walianza lini mpango wao wa kubaguana?
 
Walioteuliwa ni watendaji wa serikali si dhani ni sahihi kwa watendaji kuteuliwa kwa kufuata vyama....
 
Walioteuliwa ni watendaji wa serikali si dhani ni sahihi kwa watendaji kuteuliwa kwa kufuata vyama....
Ni kweli. Huenda sisi hatuelewi. Huenda anawateua makatibu wa ccm wa wilaya sisi tukaaminishwa vingine. Ni kama kuna watu wanakomolewa vile!
 
Ccm ina wanachama takribani 4ml na upinzani una idadi isiyo julikana. Watanzania tupo zaidi ya milioni 46. Iweje watendaji wateuliwe kwa kuangalia vyama badala ya sifa kuu ya uwezo na elimu? Vyeo vya kisiasa hiyo ni haki yao lakini civil servants hapana
 
Hivi wanajeshi walioteuliwa wanatekeleza ilani gani?
 
Ni kweli mh rais ni mbaguzi. Hilo lipo wazi ns mwenyewe aneshasema mara kadhaa kwamba hawezi kuwapa watoto wa jirani chakula! Lakini kila akisimama majukwaani humsikia akisema msema kweli ni mpenzi wa Mungu, sitabagua mtu kidini, kivyama wala kikabila. Lakini matendo yake ni tofauti kabisa! Katika teuzi zake anahakikisha mteule wake ni kada wa ccm. Wengine wanaitwa majizi! Kuns watanzania wengi ambao sio wanachama wa vyama waka hawana interest na mambo ya siasa. Lakini leo wanakuwa ignored eti tu kwa sababu sio makada! Huu ubaguzi wa kivyama utatupeleka kubaya!
 
Wenye upungufu wa uwezo wa kufikiri kutafakari na kuona hawawezi kuelewa maana ya sentensi hizo. Kifupi mkuu wa kaya ana ubaguzi tena bila hata haya. Angalia baraza lake la mawaziri, angalia wakuu wa mikoa angalia wakuu wa wilaya, angalia wakuu wateule wa taasisi mbalimbali za serikali.n.k, utaona jinsi ubaguzi unavyotamalaki. Angalia anavyoshughulikia maafisadi, umewahi kusikia kuna fisadi wa kutoka kanda ile ameshughulikiwa?. Unaona anavyojifanya haoni wala hasikii ufisadi wa Rada Epa Escrow na muhusika mkuu aliyeiingiza serikali mkenge na hadi leo anaendelea kulipwa wala haguswi tena nna cheo kapandishwa. Ukistaajabu ya Musa utaona ya filauni Angalia yule wa sakata la Lugumi kafanywa nini? Kweli hii kanda yetu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! wezi wanatoka kanda zile siyo huku kwetu!?!?!?!?
Wachache wenye uchungu na Tanzania ndio watakuelewa. Lugumi kaongezewa mda.
 
Post ya kuchaguliwa ni lazima mtu atamchagua wa chama chake, mtu ambaye ataweza kumthibiti ki kazi na kichama pia, mtu ambaye anaielewa ilani yake na kuitekeleza. Hata angeshinda ACT au Chadema, asingeteua mtu wa chama kingine kwenye serikali yake. That's simple and clear, msitafute kick kwa mgongo wa raisi
 
Ubaguzi upo sana. Serikali ya Tanzania ni sawa na ile ya kizayuni...100% jews...ingawa kuna Waisrael warabu 30% lakini hawapati kazi serikalini..haiwaajiri ..ni sawa na Tanzania hawawezi na huwezi kukuta mtu coloured akiajiriwa na serikali ya Tanzania. Serikali yetu sio equal opportunity...ni ya kibaguzi sana
 
Ni careful and critical examining something

Sasa inahusiana vipi na uteuzi wa makada?
Inaonekana huelewi ulichoandika, unajibu maana ya kitu hicho halafu unauliza kitu hicho hicho
 
Back
Top Bottom