Zitto: Nitamuunga mkono Mbowe

Zitto: Nitamuunga mkono Mbowe

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
4,769
Reaction score
5,103
Mtwara. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

Zitto aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mkoani hapa uliandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kuwachagua viongozi wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Najua bado mnalia kuhusu bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam, machozi yenu yatafutika kwani tayari habari za ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hili zimeanza kuchomoza.

“Kiongozi wa Upinzani Bungeni (Mbowe) ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi katika ujenzi wa bomba la gesi. Pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia, tunaamini gharama za mradi huu zimezidishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya Dola ya Marekani 600 milioni (zaidi ya Sh1 trilioni) zimegawanywa kwa watu kama rushwa kuanzia China mpaka hapa Tanzania. Machozi yenu wana Mtwara yatafutwa kwa uwezo wa Mola,” alisema Zitto.

Alisema katika miaka ya hivi karibuni Mkoa wa Mtwara umechukua sura mpya kitaifa baada ya kugunduliwa kwa gesi na wao (wananchi) wameonyesha kwamba wakiamua wanaweza kupigania masilahi ya Taifa.

“Mmesimama kidete kuhakikisha utajiri huu hauporwi na haturudii makosa yaliyofanyika Kanda ya Ziwa pale tuliporuhusu madini kuporwa na mabeberu wa kimagharibi,” alisema.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwahutubia wakazi hao, aliwataka viongozi wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa kuongoza kwa misingi ya chama ya haki sawa kwa wote.

“Profesa Muhongo (Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter) hana uwezo wa kuendelea kuwapo madarakani na hapaswi kufumbiwa macho, wote waliohusika na sakata hili lazima wachukuliwe hatua,” alisema.

Kuhusu uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura alisema, “watakapokuja kuwaandikisha jitokezeni hiyo ndiyo njia pekee ya kutafuta ukombozi wa pili wa Taifa hili lakini msipofanya hivyo hatutawaondoa hawa CCM.”

Mapokezi yalivyokuwa

Pilika pilika za mapokezi ya viongozi hao zilianza tangu asubuhi na ilipofika saa 5.20 zaidi ya magari 40 yaliyopambwa kwa bendera za CUF, pikipiki 300 na bajaji 30 zilikusanyika katika daraja la Mikindani kuwapokea viongozi hao.

Wakiwa wamevalia sare za chama chao, wafuasi hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali ukiwamo wa “Tunataka fedha zetu za escrow zirudi... mtumbwi wa Chenge umetoboka.’

ACT wapata kipigo

Wanachama wa chama kipya cha ACT-Tanzania waliosafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mtwara wakitumia basi dogo aina ya Coaster walikumbana na kipigo kutoka kwa wafuasi wa CUF waliowazuia wakidai kuwa hawakualikwa.

Mmoja wa wanachama wa ACT ambaye pia ni Mwenyeji wa Mkoa Kigoma anayeishi Dar es Salaam, Monalisa Ndala alisema; “Tuliambiwa huu mkutano siyo wa kwetu na ACT hawahusiki, ndipo walianza kutupiga wakitutaka kuvua sare kama tunataka kuendelea na msafara.”
chanzo mwananchi

mbowe yupo nyuma ya mengi anarimotiwa kama nyoka wa kutengenezwa
 
Duuh, kumbe hata kwenye bomba tumepigwa. Basi ni balaa! Hata hivyo si ajabu tukaambiwa hizo pesa sio zetu bali ni za wachina kana kwamba mkopo wataulipa wao.
 
Tony Gwanco nyuma ya mafisadi anarimotiwa kama jini mahaba wa kutengenezwa!

naona ugomvi wa mengi na muhongo utazua mjadala mkubwa siku za usoni.
mengi amegombana na wafanya biashara wengi sana wakiwemo manj na rostam sasa ameona akimbilie kwa wana siasa siku maadui zake wakijikusanya atakuwa pabaya sana
 
Last edited by a moderator:
Cuf hawana tofauti na kundi la wabaguzi wapigania matumbo yao.
 
naona ugomvi wa mengi na muhongo utazua mjadala mkubwa siku za usoni.
mengi amegombana na wafanya biashara wengi sana wakiwemo manj na rostam sasa ameona akimbilie kwa wana siasa siku maadui zake wakijikusanya atakuwa pabaya sana

Mengi mjinga sana ila zake zinahesabika sidhani kama anaweza kuachwa aendelee kufanya ujinga wake huu lazima watawala watafanya kitu dhidi yake.
 
Mengi mjinga sana ila zake zinahesabika sidhani kama anaweza kuachwa aendelee kufanya ujinga wake huu lazima watawala watafanya kitu dhidi yake.

Acheni vitisho nyinyi, hii nchi sio mali yenu wenyewe, hili ni Taifa la watanzania wote. Mnataka muifilisi hii nchi bila kuulizwa, si ndio?!!.
 
Sielewi kwa nini watu wanamshambulia Mengi? kwa hiyo kama hela zimeibiwa kweli kosa lipo wapi hapa?
 
Nilidhani mbowe kavunjika mkono na zzk amekuwa daktar
 
Mengi mjinga sana ila zake zinahesabika sidhani kama anaweza kuachwa aendelee kufanya ujinga wake huu lazima watawala watafanya kitu dhidi yake.

Baadhi ya watanzania wapumbavu sana hivi nikisema wewe mwizi unaitwa mnafiki mchonganishi tuache ujinga jenga hoja je kunawizi kwenye wizara ya nishati na madini mikataba iko sawa nchi inaumia kiasi gani na mikataba hii sio kujadili ugomvi na mtu,
Hata wewe utakuwa unawachukia baadhi ya watu kwa sababu zako
 
Yule Mzee wa IPP tayari kila mtu anajua janja yake na jitihada kubwa anazozifanya katika kuangusha CCM, tunajua kila kitu alichokifanya katika kusaidia CDM na jitihada zake.

Kwa mwenendo huu siku ya mwisho atapata aibu kubwa sana na kama kawaida yake asije kulia hadharani maana kwa kulalamika na kulia kama mtoto wa kike ni namba Moja!

Alifanya hila kubwa uchaguzi wa serikali za mitaa lakini mwishowe aliangukia pua sasa tunaratibu kila kitu na tutakuja kuweka hadharani.
 
Duuh, kumbe hata kwenye bomba tumepigwa. Basi ni balaa! Hata hivyo si ajabu tukaambiwa hizo pesa sio zetu bali ni za wachina kana kwamba mkopo wataulipa wao.

Hawa hawana akili! Watasema "pesa ni zetu ila bomba si letu"
 
UKAWA vipi tena haikuwepo maana zitto alishakana kwamba si mwana ukawa
 
Hawa hawana akili! Watasema "pesa ni zetu ila bomba si letu"
halafu inaonekana hawaamini, waliamndamana kutaka muhongo asiondolewe eti kapeleka umeme wakasahau BRN
 
naona ugomvi wa mengi na muhongo utazua mjadala mkubwa siku za usoni.
mengi amegombana na wafanya biashara wengi sana wakiwemo manj na rostam sasa ameona akimbilie kwa wana siasa siku maadui zake wakijikusanya atakuwa pabaya sana

Rostam ni mfanyabiashara wa nini.
 
Back
Top Bottom