Uamuzi mgumu ni ule wa kujiunga na kijana mwenzake Nchemba na kujiunga CCM iliyomfanya adhalilike kwa kukubali kutumika na kuanzisha chama akiwa ndani ya chama. Otherwise akumbuke wale wote walioanzisha CCJ wakiwa CCM walirudi kuomba msamaha na hadi leo ni mawaziri na vipaza sauti vya chama chao. Take or leave it ZZK.
Kwa hiyo Zito alijipa zamu ya kuongoza si ndio?
Zamu yake aliyokua ameahidiwa ilikua imetimia na wapambe na wapenzi wake wakawa wanamsafishia mtu wao njia ya kuongoza chama kisomi na kidemokrasia.
Alikua anajipanga kimikakati akiamini anakitumikia chama cha wapenda Demokrasia .
Tatizo liko wapi kidemokrasia.
Hayo mambo ya usaliti yanatoka wapi kwenye wakati huu wa mageuzi .
Huu ni woga tu wa Mbowe na maslahi yake.
Sio kweli kwamba Zito anachukiwa na wanachama ambao ndio waliosababisha chadema iwe na nguvu bali ni vita ya madaraka iliyoanza tangu Zito alipotangaza kugombea uenyekiti.
Ulikua ni upumbavu na kukosa mikakati ya wazee ndani ya chadema kumzuia Zito ili hali wangeweza wakamuacha akagombea na mbowe kwani kwa vyovyote Zito angeshindwa kwani wajumbe wengi walikua ni wachaga na marafiki wa Mbowe wanaomwona kuwa Mbowe bado alikua anafaa kuongoza chama.Hata hivyo wazee walishindwa kuiacha demokrasia ifanye kazi yake.Sasa chama kinaishi kwa vitisho na kutoaminiana.
Pia kwa watu wenye maono ya kushika madaraka hakuna haja ya kufukuzana kwenye chama. Hata chama kimoja wakati wa Nyerere kilitokana na vyama vingi vilivyokua na mawazo ya watu tofauti na Nyerere alijua kuwa kuna tofauti kubwa ya kimtizamo ndani ya chama kimoja lakini lengo ni kujenga taifa kwanza sio uadui.
Chadema kimekosa watu wenye dira kwa kuwatimua wakosoaji.Matokeo yake hata wananchi wanakua na wasiwasi wakuwajua viongozi wanaoweza kushika madaraka ya kiutawala kulingana na katiba iliyopo inayomtaka rais Slaa(mfano tu) kuunda serikali kwenye ngazi mbalimbali kuanzia mawaziri,manaibu,makatibu,wakurugenzi,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,makatibu kata na tarafa.Wote hawa tunategemea wawe ni makada wasafi wa chadema ili kuitokomeza kabisa CCM.Hata hivyo hakina dalili za CDM kuingia madarakani ndio maana wanagombea vyeo vya kitoto kabisa mpaka uanachama wanamnyima mtu.