Sasa basi huo si uamuzi mgumu huo ni ubishi.. Mkuu kama unafanya kazi kampuni x na ukaona mambo hayaendi unafanyaje?? Unalilia lia tu huku unaskills na uzoefu wa kutosha?? Ni ujinga tu kumuamini huyu.. 2010 alipata kura chini ya 50% jimboni kwake, hata madiwani 10 hana jimboni kwake kigoma nzima mbunge kwa cdm ni yeye tu, hakuna mission aliwahi kuarchieve, si mabilioni ya uswisi wala si buzwagi...huyu anajidanganya na ndio anakufa kama ndugu yanke nyange kabouuru... Atawadanganya wasio mjua mimi nipo kigoma hapa kikazi naelewa sana wakati mgumu alaonao huyu jamaa.. Baada ya kuazsisha mizozo na cdm hapa kigoma watu wamemtoa thamani kabisa, watu wamezidi kujitolea kufungua vijiwe vya cdm kwa gharama zao na kukisapoti chama....
Ben sijui kwann sijui sana siasa ila nilikua naona kama ndio uamuzi sahihi kabisa huo....kama anataka kwenda mbali kwa siasa za kitanzania ni lazima abake CDM tumeona wengi kina kaborou,lamwai walipoishia..kusema tu samahani ni shida gani
Kwa sasa ni Zito pekee anayeweza kuamua hatima yake. Ni yeye tu ndiye anayejua alicholipwa kuihujumu CDM!! Nyie wengine msiojua kilicho moyoni mwa Zito mnahangaika bure!! Pesa kala yeye na Wapambe wake, sisi inatuhusu nini? Ila kwa Wapambe wake na labda ukiwemo wewe mna haki ya kufa naye!! Sisi Watanzania wengine tuliomwamini KATUANGUSHA; na namna pekee ya kumuadhibu ni KUMKATAA. CDM amueni na sisi tupo nyuma yenu.
Kumbukeni kuing'oa CCM ni Vita ya kufa na kupona! CCM wa Pesa sana japo ni hizo walizotuibia, wana vyombo vyote muhimu japo ni kama Haramu, Wameweza kutoa ujira kwa masikini wanaojua kusoma na kuandika ili wawatetee kwenye mitandao ya kijamii. Waendelee kufanya hivyo ila asitokee mtu miongoni mwetu akatumika na tukaogopa kumwajibisha, TUTAKOSEA SANA.
Maswali hayo ndiyo wanaojiuliza Watanzania. Zito kwa dharau zake anadhani Watanzania hawawezi kujihoji na kuuliza. Ajue kabisa kwamba watu wenye akili zetu TUNAJIULIZA SANA!!
Zitto, aombe msamaha kwa kosa gani.
Ni Dr. Walid Amani Kabourou na si mwanamichezo Nyange Kaburu
Kosa la zitto kufukuzwa chadema sio kudai mahesabu na wala sio kutaka kugombea uenyekiti kosa lake kubwa na kuandika waraka wa kimapinduzi wakutaka kupindua viongozi
Ni kweli mshauri wake, aombe msamaha kwa kosa gani, na yeye ndio kila kitu chadema hata mwaka jana serikali za mitaa bila yeye chadema wasingeshinda kwa kishindo.....
Naona kwenye Fb yake kasema hatagombea tena ubunge jimbon kwake
Upo sahihi kabisa Ben Saanane, kuna haja ya kufanyika maridhiano kati ya CHADEMA na Zitto, kufukuzana katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ni hatari sana kwa pande zote!
Hakuna atakaefaidi moja kwa moja, iwe Zitto au CHADEMA, kila mmoja atapoteza kwa kiwango chake!
Yaandaliwe mazungumzo yenye lengo la kusameheana, bila kuwekeana masharti yoyote magumu...
Kwani amepata washauri wapya!? Kama ni walewale mbona hawakuonyesha huo umakini wakamuacha aende mahakani...hamna kitu hapo,CCM wabaya!Zitto ni makini na washauri wake ni makini pia, huenda maamuzi magumu anayotaka kufanya ni kuendelea na chama kwa kuomba msamaha. Maana hakuna kitu kigumu kama kuomba msamaha.
Kuna nyepesi mitaa ya kwetu ati ameandaliwa kuwa mgombea mwenza wa Lowasa ili kupata kura za vijana. Labda ndo maamuzi magumu yenyewe hayo. Kugombea kama wagombea binafsi not affiliated na vyama
Hamna kitu. Mtu mzima hatishiwi nyau
mzee Mtei akifa itabaki kuwa ya nani??