Basi akagombee chama kingine lakini sio chadema. Lazima chama kiwe na malengo. dr.Slaa alishapiga jaramba 2010 kilichobaki ni kuingia uwanjani(ikulu). Zitto bado anao mda wa kujipanga na umri unaruhusu. hatutaki kupoteza nguvu kazi kama Slaa ipotee hivihivi. Inabidi dr.Slaa atoe mchango wake kwa taifa lake nasi tumfaidi.
mkosoe kwa hoja,hakujiunga Chadema baada ya kuchakachuliwa kura na CCM kama wengine,hakuna mwanasiasa asiejisifia,nitajie hata mmoja ili nikiri kuwa sifahamu siasa,hata Mwl Nyrere ambae ndo kioo cha wanasiasa alikuwa akijisifia kwa mazuri alokuwa anafanya, pitia andiko la zitto then edit kila kwenye jina la zitto andika la yule jamaa yako ili uridhike,sera za CDM unazotamba nazo mitaani ni jasho la mboe na zitto upende usipende,usifie usisifie!
Zitto sawa na mtanzania mwingine yeyote anayo haki ya kugombea urais. Lakini watanzania nao kwa upande mwingine wanayo haki ya kumfahamu mtu yeyote anayekusudia kuwaongoza. Tunataka kujua kwa mfano yale mawasiliano ya Zitto na adui namba moja wa watanzania Rostam Aziz usiku wa manane yalilenga nini. Tumekwisha umwa na nyoka hivyo tukiguswa hata na unyasi tunakuwa na wasiwasi.
Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika.
Naomba ninukuu maneni ya Ernesto Sheka kwenye maandiko yake ya The Moment Of Truth:
Can CDM give that a chance to someone from nowhere?
Mh.Zitto....i don't think its bad for you to openly express your personal views as to whether you like vying for presidency or not...i think this is a basic right for any Tanzanian and i really wonder why people are wasting so much of their time on this.....On the positive note though....now that you are here in this thread......please..please please....what are you guys (CHADEMA MPS) doing concerning the implementation of the new mining law??????come on!!!don't you see that the country is being robbed of her natural resources (gold)day and night????What do you say?
Kiongozi, huo ujumbe wako ni murua na rahisi sana kuutoa lakini utamsaidia kidogo sana (if any) Zitto kufanya vizuri zaidi. Kama unamtakia mtu mwema basi ni vizuri ukamstua pale unapoona anaelekea kujikwaa. Na Kama atasema amefanya mengi lakini watu bado wanauliza then it is obvious that 'he's been shooting in the dark'. So, he needs to change his tactics.
Je katiba ya chama chake inamkataza kuwa na ukaribu na Makamba? kama jibu ni ndio kwanini msimvue uanachama? acheni siasa za kijinga wakuu hivi wewe kama ni cdm huna ndugu ambae ni tlp? hamsocialize? kwa kuwa tu huyo ndugu yako hayupo chama kimoja na wewe? au ndugu zako wote ni wa chama unachikisapoort?
Msimsakame Zitto yeye ni mtu jasiri amethubutu kusema tofauti kama wengine wanavyoeleza chini chini au hujasoma hii kitu iliyoandikwa na wabara?
Hatujamsikia Mheshimiwa Mbowe akisema kama anautaka urais ila ukisoma hiyo habari utaona kuwa kuna kundi lake ndio linataka Mhe asimame 2015! Kundi lake linaenda chaka sababu wanayoitoa ni kuwa Mbowe ametumia pesa zake sasa wanamaana inabidi Mbowe awe Rais arudishe pesa zake? mfike mahali muwe mnaleta hoja zisionekana zina maslahi binafsi. Hakuna mtu asietaka kiongozi mwenye uchu wa maendeleo na hakuna atakae kiongozi mwenye uchu wa mali unless/only and if uchu huo huyo mtu atanufaika nao.
Vyama vyote vya siasa vitakuwa na mitikisiko kuelekea uchaguzi wa 2015 cdm hasa wanajf wengi humu mmekuwa mkimshutumu Pro Lipumba kugombea kila mara kama hakuna mtu mwenye uwezo mwingine zaidi yake, kwa kumpinga Zitto na Mbowe na kutaka Slaa aendelee mtajitofautisha vipi na CUF? Mbowe alishajaribu kadhalika na Dr Slaa pia hamuoni sasa apishwe mtu mwingine mwenye ambition atakaeweza kuwawakilisha 2015? nadhani kama mnaamini chama chenu kina sera thabiti swala la nani asimame halitakuwa gumu kwenu.
Tafakari.
Prof. Lipumba amegombea uraisi wa JMT mara nne bila kuonyesha dalili zozote za mafanikio; 1995, 2000, 2005 na 2010,na bado anakusudia kugombea, akijilinganisha na raisi wa senegal abdulaye wade, aliyechokwa sasa na wasenegal.
Maalim Seif amegombea urais wa SMZ, sasa SUKZ mara nne bila mafanikio japo alitoa ushindani mkubwa sana; 1995, 2000, 2005 na 2010.
Sasa unapojaribu kuwalinganisha hao wagombea wa kudumu na Mbowe aliyegombea mara moja-2005 na Dr. Slaa aliyegombea mara moja-2010 na kutoa upinzani mkubwa kwa ccm na hata kuonyesha dalili za kuing'oa ccm madarakani, unakuwa unatumia utaalamu gani ama vigezo gani kusema Dr. Slaa na Mbowe wawaachie wengine wakati umeshindwa kunyanyua kinywa chako kuwaasa viongozi wa chama pendwa chako kuacha kuwa wagombea wa kudumu na kuwapisha wengine.
Huu ugombea wao wa kudumu katika nafasi za uenyekiti wa chama na uraisi wa JMT kwa Lipumba na ugombea wa kudumu wa ukatibu mkuu na uraisi wa znz kwa maalim seif ndio chanzo cha timua timua iliyomkumba hamad rashid kwa kuhofia kumalizwa kwa usultani wao ndani ya chama. Na hapo ndipo mahali muafaka pa wewe kujikita kutoa ushauri mwanana wa kukiboresha chama chako. Kujaribu kujivika ushauri kwa chadema ni unafiki, narudia tena huo ni unafiki kwakuwa unafahamu kwamba hufanyi hivyo kwa moyo msafi bali husda tu ndio inakusukuma.
Na wewe tangu lini ukawa mshauri wa Chadema?Na kwa cdm huyu ndio mtu anae faa kuwa Rais. Wengine wote wakina M & S Company wana tamaa tu za madaraka. Nawaomba wana cdm muungeni mkono zitto na apitishwe na chama
Kabla ya kupost fuatilia matokea ya urais ya maalim seif na shein au karume, nani aliyeonyesha upinzani mkubwa sefi aliyepata zaidi ya 45% au slaa.
Mapenzi yako kwa slaa yasikufanye kuwa kipofu
Zitto = Rostam Aziz
Huyu kaka anamapungufu. Nasikia eti hajaoa!!!!. Hii post ni ya wababa, kijana kama huyu hajatulia, wachumba watamsumbua, Ikulu itajaa vichupi so badala ya ku deal na issue atadeal na vichupi