Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Kama mtanzania mwenye sifa, ana haki ya kutangaza nia yake.
Siyo dhambi Zitto kusema anataka urais
 
Hapa kwenye RED umemlenga MM mwanakijiji!!?? kama kutumia jina lako ndio sio uwoga basi una tatizo la ufikiri. hivi unadhani watu wapo hapa kuuza sura!!??......
Kwanini awe mwoga while yupo ule upande wa "wenye nchi" na hata hoja zake ni za kujipendekeza? Watamfahamuje bila kuweka jina lake halisi!
 
Kura yangu utaipata wakikuteua tu usiwe na shaka hesabu tayari unakula 2 yangu na yako...............
 
Thibitisha maneno yako kwamba nina kisirani na mbowe.Wengine sitawasemea.Acha majungu kama huna hoja ya maana ni bora tu unyamaze.

Thibitisha ni wapi nilipokisaliti chama changu.Kwa hayo majungu yenu hamtaniweza hata kidogo na mnalielewa hilo ila ni kiwewe tu kinawasumbua.nikiwa nagombea uenyekiti BAVICHA mlileta majungu kwa njia zote hadi dakika za mwisho ikashindikana.Nakushangaa leo unaongelea kwamba nimesaliti chama changu bila kujua theme iliyotumika jana kwenye fundraising ya Arumeru Mashariki ya M4C ilikuwa signature yangu hapa JF wakati nagombea uenyekiti bavicha na kwenye vipeperushi vyangu 'Movement for Radical change" ambayo wewe na wenzako mliita ni ya kidikteta na kuleta upotoshaji.Wakati mwingine muwe mnakwepa fedheha kama inawezekana....

Yes,msimamo wangu dhidi ya uovu,ukandamizaji dhidi ya taifa langu na watu wangu siwezi kuuvumilia na siwezi kuogopa kupambana nao.

Kilichotuunganisha na Zitto ni msimamo dhidi ya uonevu,ukandamizaji,dhuluma bila kujali ni nani anayeonea au ninani anayedhulumiwa.Kilichotuunganisha ni msimamo juu ya utekelezaji wa demokrasia ya kweli na kutoa maono ya kule tunakotaka taifa letu lielekee.

Kuhusu kuwa chadema huko mbele itakuwa na kazi kuliko CCM ni matamanio yako tu.CHADEMA itaendelea kusimama na utaona tutakavyoingia uchaguzi mkuu tukiwa na nguvu mpya.

Kwa kuzingatia muafaka na mchakato ndani ya chama changu,kama Zitto ataamua kugombea nitamuunga mkono kwa kuwa nakubaliana na msimamo na dira yake kuhusu kule tunakotakiwa kwenda as a nation.

Kama tafsiri ya kupigania interest za Tanzania kwa kuchukua maamuzi magumu ni chuki kwa wazungu basi nakubali.But you obvisoulsy havent got your own mindset right thats why you are so quick to condemn a man who has refused to be bullied, intimidated and bamboozled by selfish racist imperialist powers.

kitakachokata mzizi wa fitina ni Zitto kuchapa kazi kwa bidii na wale wenye mtizamo unaofanana ijulikane kuwa there is no excuse zaidi ya kuchapa kazi kwa bidii,determination and objectivity.

Wengine jengeni majungu tu,this is what you are good at !Besides, please don't let your anger cloud this debate because I don't want this to disintegrate into meaninless tat for tat.




I doubt kama umesoma makala husika kwa umakini .Sijui umefikiaje hitimisho hili.Tujenge hoja tuache kujadili kitu kwa kuzunguka mantiki au nje ya mantiki(logic)


Nadhani aliyetuingiza mkenge kwa demokrasia ya magharibi alituweza.Hebu tutende haki,hivi ni zitto tu ndani ya chadema aliye karibu na watu wa CCM?Hata Mwalimu J.K Nyerere alikaa mezani na waingereza.Unaweza kuwa rafiki wa mtu bila kuathiri principle zake na taasisi yake

Isipokuwa katika harakati kwa wanamapinduzi wote,kila sekunde ni ya tahadhari.Tusije tukajikuta tu tunafanya maamuzi ambayo hayaleti reform ya kweli.Wengine tunahoji sasa ni kwa nini Mwl. Nyerere alikwepa Africanisation baada ya uhuru badala yake Akina Oscar kambona ndiyo wakalisimamia.tunahoji kuhusu mkataba wa kuipatia Tanganyika kama walivyofanya mataifa mengine ya Africa kule Lancaster house
 
Anatoa yaliyo moyoni mwake, sioni Tatizo. Uraisi sio kazi ya kikundi fulani cha watu.
 

Umefanya utafiti ukapata jibu kuwa zitto ni chaguo la CHADEMA WOTE nyie ndo mtamwalibia zitto
 
Zitto ni kigeugeu, anapenda kuponda wenzie, na anauwezo wa kusaliti wowote ule
 
Kwanini awe mwoga while yupo ule upande wa "wenye nchi" na hata hoja zake ni za kujipendekeza? Watamfahamuje bila kuweka jina lake halisi!
Nimekuelewa vyema mkuu, hii fomular inaitwa jipendekeze ili upendekezwe, ndio maana sikushangaa Richard Kasesera kusikia ameteuliwa kwenye ulaji wa bodi ya madini.
 
Hello Zitto,

Mimi nimesoma yote ...umeandika vyema sana kuhusiana na umri na urais.

Mimi nadhani watu wengi waliokuwa wakikuamini hasa wanaopata updates za whats going on wamepunguza imani na ww that is an issue na wala sio agenda zima ya umri.Imani kushuka juu yako inaonekana kusababishwa na mambo kadha wa kadha ,,,mengi yamesha zungumziwa humu is up to you to come clean kwa kuyatolea maelezo.Hapo ambao bado wana imani na wewe nadhani wengi ni waleambao propaganda hivi tulizopata mwanya sisi wengine kuzisikia na kuzifanyia kazi wao hawanazo...wana jua Zitto yule yule wa jana na leo .Kuna sehemu niliandika matatizo ya vijana wetu tunaojua kwenye siasa wewe kwako nili point out kuwa you are not Royal to your part ...misiguano ipo ila haitakiwi kuonyesha wazi wazi na na katika kujadiliana lazima mpinga ila mwishoni resolution ndio inayobebwa na chama na kila member.

Zito wengi tunataka mabadiliko ,na mimi no matter yanatoka wapi kwa wazee,vijana ,CDM ,CCM ...Kwangu mimi sijali ..najali uadilifu wa mtu maana hata CCM kilichokosekana ni uadilifu ..ambao unatoa imani.So jenga imani kwa wapiga kura wako pamojana wana chama wa CDM watakao kupitisha kama ulivyosema na kulitambua...

Katika point zako nzuri ulizo weka napenda kuwaambia kuwa angenda ya umri ni ngumu kutenganishwa na maslahi ya kijana mlioko kwenye siasa kwa sasa na hasa nyie mliyo iamsha sasa, kwa maana kama itapitishwa vijana mtakao nufaika nayo ni nyie .Kama Mtei aliyosema you can't select someone from nowhere to lead …lazima wale mnao wajua na mna good track record zao.

Kama utapita kwenye chujio la CDM more likely utaukwa urais be royal to party brother jenga imani kwa sisi wenye shaka nawe ,every vote count.

NB
Sehemu ambayo naweza kusema ungeangalia siku nyingine wakati wa kuandia ni pale ulipo andika kuhusu Kwa mfuga mbwa,Tabata na Masaki watu wa kwa mfuga mbwa wanaweza kuwa offended you may be right but not political correctiveness. Hakuna tatizo ku portray Masaki kama sehemu ya high class, Tabata kama sehemu ya middle class but Kwa mfuga mbwa kukuita lower class na haukai huko ni tatizo sawa sawa mzungu amwite black Niga ila black kwa black kuitana niga haina noma (Part haihusiani na suala la umri Vs. urais so maelezo yako kuhusu umri nayapa A+)
 
Kumbuka kauli ya Nyerere "mtu anayekimbilia Ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma". Zitto ngoja watu wakuingize Ikulu sio mahali pa kujipeleka na kukimbilia. Na ole wao CDM mkimkubali mtu "anayeutaka urais"
 

Hizi Alliance/ coliation zitakupeleka pabaya sana Young Man........kama unataka kujifunza siasa na ufike mbali fuata nyayo za John Mnyika hizi akili za kushikiwa na mtu hazitokusaidia.
Wamekuja akina Mr 2 Sugu wamechukuwa kadi mwezi mmoja baada ya miezi mitatu wamekuwa Wabunge na wewe kama unajiamini ni mwanasiasa wa kweli nenda kajijenge kwenu na usimame kwa miguu yako miwili na ushinde ubunge. kama wewe ni Mwanasiasa mzuri unaweza kunieleza sababu za kisayansi ni kwa nini kura za ushindi wa Zitto Kabwe mwaka 2010 zilipunguwa jimboni kwake?
 
Suala hapa siyo Zitto,suala la kujadili ni umri wa kugombea urais.Mnajadili mtu badala ya hoja!
 

Itakuwa jambo la busara sana mumchagulie Zitto marafiki na wengine mumuambie sio asiwakaribie tu bali awanunie hata wakikutana kwenye korido za pale mjengoni. January ni kijana mwenye vision na mwenye uelewa mkubwa sana. Binafsi namkubali sana January kwani kauli zake na matendo yake yanajipambanua na wazee waliopo ndani ya ccm. Haitakuwa jambo la busara kuanza kuchokonoana nani rafiki wa nani kwani kwenye siasa kuna zaidi ya mambo ya majukwaani kwani nani hakustaajabu Rev Mtikila kupewa mil 3 na Rostam? unadhani kila jambo likiwekwa hadharani na uswahiba wanasiasa na nyie mnavyochukulia uadui mtabaki chamani?

Tujaribu kuwa wastaarabu kuwa na uswahiba na mtu mnaetoka itikadi au dini tofauti sio tatizo! angalieni hilo kwa jicho la tatu tukianza hivyo tutaanza kukatazana tusiwe na marafiki na zile sehemu ambazo cdm haina wawakilishi itafika mwisho kwa wale wa dini au dhehebu fulani maana hawakutupa kura! Siasa sio ugomvi wote wana leo la kutuongoza iwe slaa au zitto sioni tatizo ila nyie mashabiki ndio wenye matatizo jaribuni kupunguza umbumbumbu wa siasa.
 
ni vizuri kuwa muwazi ili chama na watz wakupime mapema, kuliko kujenga makundi na mbnu chafundani ya chama!
 
Nashukuru mkuu Ben kwa kutuwekea hii makala hapa. Labda tujikumbushe ule usemi wa 'walk the talk and not talk the talk.

Niliposoma hii artickle nimemkumbuka Barack Obama. Huyu rais ni mzuri mno wa kuongea, anajenga hoja zenye mashiko na ukisikiliza hotuba zake unaweza hata kumkabidhi fungo za gari maana ni rahisi sana kuamini mwisho wa mikosi umewadia, kumbe wapi. Obama sio kama ni sifuri kwenye utendaji lakini he is just as weak as the man standing next to him.

Zitto ni mzuri sana wa kujenga hoja, hilo halina ubishi, je, yukoje kwenye utekelezaji? Wakati wa Speaker Sitta, Zitto alipigania (kwa nguzu zake zote na kwa gharama kubwa) utata wa Barrick/Buzwagi. Fast foward, Barrick hao hao wanampa mabati Zitto kwa ajili ya huko jimboni kwake - ceteris paribus!

Lugha/nguvu aliyokuwa anatumia bungeni kipindi hicho wakati anajadili Buzwagi/Barrick ni tofouti kabisa na sasa. Kuna thread moja inaongelea hii issue ya mabati ya Barrick hapa jf, na Zitto alijaribu sana kutoa maelezo na hata kusema kuwa (tafsiri yangu) amekuwa, uelewa wake umekuwa mpana.

Katika hali ya kawaida, ni vigumu kumsimamia vema mtu wakati huo huo unamtegemea akupe push (hata kama ni push ndogo kama ya mabati). Kisiasa unakuwa umesha-compromise your position.

Labda nikumbushe, mwaka jana waziri mkuu Pinda alisoma majina ya makampuni 15 yanayoongoza kwa kulipa kodi kwa miaka 5 iliyopita. Barrick hapo! Hili lilikuwa bunge la bajeti 2011/12. Mchango wa Zitto kwenye hicho kikao ni pamoja kuweka utaratibu wa 'windfall tax' ili bei ya dhahabu inapoongezeka kwenye soko la dunia basi ongezeko hilo liwe reflected kwenye kodi wanayolipa. Lakini sijamsikia Zitto akiongelea kwa kina kuhusu Barrick na kodi kwa ujumla hasa ukizingatia kuwa hawapo kwenye top 15. Sasa leo anataka watanzania waamini kuwa akiwa kwenye top position atasimamia vizuri madini na gas? Hapa ndio Zitto anatakiwa ku- walk the talk and talk the talk.

Sisemi haya kwa kumvunja moyo, hata kidogo. Nataka Zitto ajue exactly ni mambo gani anatakiwa aangalie, na vipi anaweza kujijengea imani mbele ya watanzania - wapiga kura. Mabati yanaweza kuwa ni kitu kidogo sana lakini yanatoa taswira kwamba huyu ni mwanasiasa wa aina ipi?. Huwezi kuniambia kwamba shughuli za mtu huyu zina walakini wakati huo huo unapeleka bakuli kwa hiyo mtu akusadia kutokana na mapato ya shughuli zile zile zenye walakini!. Utanicha na maswali.

Ushauri wangu Zitto, be yourself, rudi kwenye principles zako za zamani. Hauna sababu ya kuzibalisha. Achana na mashorabo wa mjini. Hawaaminiki.
 
Zitto kasema anautaka urais, lakini kuupata urais ni mchakato unaoanzia katika chama, cdm wana taratibu muafaka na bora kabisa katika kusimamia chaguzi zao, yeyote anayeutaka urais aseme tu, hilo si tatizo kabisa, taratibu zitafuatwa
 
kwanza nataka ku-declare interest yangu kwenye mjadala huu.....umri wangu hauangukii kwenye kundi la ujana.

zitto & co wanapo-champion vijana kukamata uraisi ninawaunga mkono kwa 110%.
kwani umri ni nini? si ni namba tu? kinachotakiwa kuzingatiwa ni maturity, and zitto is more than mature already.

i think wa-TZ wengi bado "tuna-suffer" from modesty ya mwalimu nyerere (ambayo kusema za ukweli lilikuwa ni jambo nzuri).
as far as mwalimu was concerned, dhamana ya utumishi kwa umma ni kitu ambacho mtu alitakiwa kwanza asiwe anakitafuta yeye binafsi kwa bidii sana na pili hata pale atakapokuwa ameombwa alitarajiwa kujitathimini sana mwenyewe (in fact he/she should be seen doing it) kabla ya kuikubali.

"syndrome" hii ndiyo inayomfanya zitto aonekane kama vile ni mtu asiyefaa, mwenye tamaa ya madaraka, nk.
ushauri wangu kwa zitto na wenziwe ni kuwa katika desire yao ya ku-aspire for that highest post, their approach should take into consideration this "nyerere factor", probably not in content, but at least in context.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…