Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Kuna haka katabia mtu ukileta mada humu jf kuna baadhi ya members wanataka ziwe za mapambio ya chama tu hawajui kuna habari nyingine au mawazo yanaweza kujenga na sio kubomoa kama wanavyodhani.

Ushauri wangu endelea kusimamia unachokiamini achana na waoga ambao hata kutumia majina yao wanaogopa!


Nashukuru sana somo [Mohamedi] bahati mbaya zaidi sina chembe za woga kwenye kuujadili ukweli, baadhi ya wanachadema wenzetu ni wanafiki maana wanapenda kusikia mijadala ya kujadili mazuri tu ya chadema, mada zikiletwa kama hivi huwa hawasomi kwa umakini na kuelewa na matokeo yake wanakuwa wachangiaji wa siokijua.
 
January alikurupuka vibaya sana hajui mlaji wa mwisho ndiye atakayebeba mzigo wote wa kodi kibaya zaidi kodi yenye itakwenda kununua maVX L/Cruiser VDJ 200 na kugharamia safari za watawala.

Mkuu wangu huu upuuzi wa kuweka sheria ya kodi kwa wenye nyumba ni hoja hovyo kabisa ya January Makamba.Hakika hiki ni kitanzi kwa vijana wote mijini wanaoishi nyumba za kupanga.Hivi ni mwenye nyumba gani ataacha kupandisha kodi kufidia hasara atakayopata? Ninaomba CDM waongoze maandamano ya kulaani sheria hii haramu.CDM fahamuni nguzo kuu yenu ni Vijana na sisi ndio tutaumia kwa sheria hii ya hovyo isiyojali umasikini wetu.Nimuulize swali January hivi haoni kila serikali inapopandisha kodi vitu vinapanda bei? Sasa anadhani kodi ya kwenye nyumba atabeba mwenye nyumba au mpangaji? Nitalia na Mungu na hii sheria ya hovyo ya kuwaangamiza vijana mpaka siku Mungu atakapojibu maombi yangu.
 
Ben,

Huo mtandao wenu na akina Zitto utapeleka nchi pabaya.Nilishawahi kutaadharisha hapa kama mbowe atawania uenyekiti wa chama au urais atarajie kudhalilishwa na hawa vijana.

Hii makala nimeona mahali Zitto anasema atachukua maamuzi yatakayochukiwa na mabwana wakubwa wa magahribi. Ninachojiuliza hivi ben na akina Zitto mmeunganishwa kwa mrengo wenu wa kushoto au kumpinga na kumdhalilisha mbowe? Sijawahi kujua Zitto nae ni leftist basi naona huko mbele chadema ina kazi kuliko CCM. Zitto naona nae ameanza kuwa na chuki na wazungu kama ulivyo ila nilishamshauri Mbowe awe makini na hili kundi naona limebadili uelekeo na linavuta vijana wasomi kwa kasi.

Ben saanane na wenzako ni wasalaiti wa chadema, kisirani chenu na Mbowe kitawafanya mtoane roho sasa
 
January alikurupuka vibaya sana hajui mlaji wa mwisho ndiye atakayebeba mzigo wote wa kodi kibaya zaidi kodi yenye itakwenda kununua maVX L/Cruiser VDJ 200 na kugharamia safari za watawala.

Mkuu Ngongo tuko pamoja.Ni wakati sasa vijana wote bila kujali itikadi zetu tuungane kupaza sauti na kulaani sheria hii ya kuwamaliza masikini.
 
Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.

Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!

Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.

Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com
Ninyi ni waroho wa madaraka pamoja na uwezo wenu mkubwa wa kujenga hoja ila mnautumia kuwahadaa watanzania...wasaliti wakubwa, mmedhamiria kumdhalilisha mbowe na kumpindua.Uchaguzi wa BAVICHA uliopita uliona kundi lako lilivyodhibitiwa kwa mara ya tatu
 
Yap nimesoma[BOFYA -UDADISI].
Hakika CDM ndio kumekucha kama michezo yenyewe ndio hii,vijana wana miaka -35 wanawaza Urais hakika, tumepotea sana tena sana ukizingatia chama ambacho tuliamini kingepigania dhamira ya ukombozi wa Mtanzania,bali vijana wadogo baada ya kujituma kuprove wanaweza kumbe kwenye masaburi yao wanawaza kuwa Marais 2015.Mama Tanzania tusaidie wendawazimu huu wa mawazo mfu kwa sasa ufe hata kabla ya kuanza.

Nakumbuka kuna watu walionwa vijana ndani ya CCM,wakapewa kwa vigezo hivyo vya ujana lakini leo,imekuwa wazi kumbe kundi lile liloonekana ni vijana,walio kuwa na akili ni wachache waliosalia ni makapi tu, tena wamepewa wakiwa na umri wa miaka 55 sembuse miaka 35 upuuzi wa kuzungumzika tena aibu sana

Nilisha hisi [sense] ujio wa jambo ili,ila CDM ndio wakikosa umakini na kudeaL na watu ovyo wenye akili ovyo wasio fikilia kwa logic na kuamua kwa kutumia Analytical way basi wakiachiwa waendelee ndani ya CDM,hakika KIFO cha CUF kitakuwa na heshima maradufu zaidi ya CDM.

Nilimshauri zitto kwenye thread moja nikamwambia muda wa yeye kuwaza urais sasa ni aibu kwake aachane nao awaze kujenga na kusimama miaka ishirini ijayo kwa maana kwa sasa ndani ya miaka 35 + miaka ishirini [20] ijayo basi miaka 55 ni best Material President ever kwa kuwa ameiva kwa lolote lile.

Kama kuna watu wazima wanamwambia kuwa anaweza kuwa President na wanamwambia watampa support hakika they played him na kuna agenda ya siri,moja kuua upinzani Nchini yani kifo ambacho mwalimu alikihita Natural death, ama kuna watu wanatengeneza conflict of interest ili maeneo yao yawe laini kwa vitu vyao upande mwingine kupita huku CDM ikiwa kwenye kutoana meno,au yeye anataka green pasture upande fulani hivyo anatafuta gear ya kuchomoka kwenda upande wa PIli kutimiza ndoto yake.

Nimetoka kusoma thread ya CDM wanamaongezi na EL na ndio maana wameacha kampeni za ufisadi wakamuachia Nape na wao waanzilishi wamekula kona,nimekutana na hii,nimeunga DOT,kama kweli CDM hakitaki natural dealth baada ya uchaguzi wa Arumeru ni vyema wajipange kutoa jawabu la uozo huu wa kuondoa watu ambao spirtually awako pamoja na CDM kwa faida ya TAIFA. Waswahili tunasema ni heri ya nusu shali kuliko shali kamili,sio kuwa watanzania hawaoni na hawezi kuunganisha DOT,watanzania wanaona na wanasiakia ubaya siku hizi nao wanakuadhibu huku wanacheka kama ilivyo tabia ya Rais wao.

Tatizo la wanasiasa wetu sometimes uwa wanafikilia kuwa wao ni Intelligent and smart kuliko raia huku mitaani kumbe wanasiasa wengine ni remote controlled na raia huku huku mitaani.Sikutegemea speech hiyo ya UDADISI kutoka kwa Zitto,kwa kuwa moja ya vitu ambavyo Zitto alipaswa kuwa navyo ni kuepuka mijadala au forum zozote zinazoonyesha kuchokonoa juu ya ufahamu wake kuhusiana na swala la urais akiwa kama Mwanasiasa kijana.

Tena ukitaka kujua Zitto ni mtoto hata blog iliyotoa taarifa yake iko accurate na dhamira ile ile ya watu intellictual kujua ana dhamira gani je,ni kijana anaefikilia kuhusu kufikilia au ndio wale wasio na chochote bali siasa za popularity.Pole Zitto kama kweli hiyo udadisi ni maneno yako UMEMALIZWA KIJANA, they used you pia watakudump.Vinginevyo awemo katika kutuchezea kujua watanzania wanamuonaje yeye,lakini ubaya wa mchezo huu,unamaliza yeye,wakati mwingine kama ni mdau wa watu aina ya THINK BIG asipende tabia ya kucheza michezo ya kupima Political Atmosphere wakati anajua kuwa si wakati sahihi,kwa kuwa yeye kuwa ni centre of the topic in town inamshushia heshima kwa watu makini kimfumo kumuona kama ni mtu asie tofauti na wema sepetu, tofauti yake na wema ni kuwa wakati wema yuko kwenye front page tasinia ya urembo na filamu,yeye yuko front page kwenye political arena.

Kwa kuwa great thinkers they want to put people bussy kwenye mazungumzo siasa na michezo na sanaa basi uchagua watu ambao ni POPULAR na ndio maana kwa wanasiasa ukionekana kuwa wewe ni centre of attention wanasema unatafuta Cheap Popularity,ok kama ni Mzee wa kuuza sura cool your the best candidate lakini kama ni mtu makini wakujua genuine life ya Mtanzania na kuwa unaumizwa kutafuta majibu ya matatizo yao basi usingekuwa tayari kuusogela urais,watu ndio wanakusukuma kukupa urais,sio unajipigia debe uonekane unafaha kuwa Rais.

KAMA KWELI NIMANENO YAKO ULIKUWA KIJANA SANA KUSHNDWA SIASA ZA TANZANIA KATIKA UMRI MCHANGA WA CHINI YA MIAKA 35.
 
Lakini siku za hivi karibuni hasa baada ya kifo cha Kamanda Regia Zitto ameonyesha maturity ya ajabu, ameonyesha kuweza kuimudu hii post ya juu nchini. Hata pale ofisini watu wameanza kumkubali na ile hofu yao dhidi yake ni kama inapotea polepole.
Siasa si uadui ndugu yangu kama kungekuwa na uadui basi pale bungeni upande wa wapinzani ungekuwa una senyenge na wanakuwa na sehemu yao ya kuingilia. Kuna wakati huwa nawashangaa mnaokuja na hoja kama hizi za fulani ni chama fulani kwanini ana urafiki na fulani wa chama kingine? acheni fikra za prof long water.

Kama tunajenga nyumba moja kwanini tugombee fito?
 
Zitto aliponzwa na urafiki wake binafsi na JK ambao haukuanza leo wala jana.(Mimi sina tatizo na urafiki wao na napenda waendelee kuwa na mahusiano mazuri) tatizo lilikuja pale ambapo Zitto alilemewa na 'mahaba' ya urafiki wake na Kikwete kiasi cha kujikuta anapata ile kitu tunaita Agent problem ambayo imemletea agent cost, cost ambayo ni kutoaminika kwenye chama na hata nje ya chama. Na ndio maana hata akifanya jambo kwa nia njema na kihalali(kama alivyogombea uenyekiti) watu wanamshukia kwa nguvu nyingi.

Lakini siku za hivi karibuni hasa baada ya kifo cha Kamanda Regia Zitto ameonyesha maturity ya ajabu, ameonyesha kuweza kuimudu hii post ya juu nchini. Hata pale ofisini watu wameanza kumkubali na ile hofu yao dhidi yake ni kama inapotea polepole.

Kitu pekee ambacho ni ngao ya Zitto kupata uongozo wajuu ni kuendelea kuwa fair kwa makundi yote. Hapa nazungumzia udini. Zitto pamoja na kuiheshimu sana imani yake lakini SIO MDINI KABISA! Huwezi kuwafananisha na wale wenzitu wa buguruni. Zitto anaheshimu imani ya wengine na ana marafiki wa dini zote na anasaidia wote bila udini, anachukia udini na hapendi kuwa mdini.

Kudos Zitto

Baba mchungaji Mzito nakubaliana na wewe kabisa kuwa Zitto amekuwa affected na 'mahaba' ya urafiki sio na JK bali hata na vigogo wengine wa ccm. Na hili limefanya watu waanze kuhoji dhamira na hata loyalty yake iko upande gani.

Zitto nakuona uko online, kwa moyo safi kabisa na kwa nia njema nataka nikuleze kuwa you are young fine politician with great potential lakini unatakiwa sasa uamue na kila mtanzania including wana-CHADEMA wenzake wasihoji dhamira yako. Kwenye vita kila askari ananatakiwa aamue you are either with your fellow comrades or against them, lakini huwezi kuwa 'indifferent' - huwezi kuwa hapo katikati. Huwezi kuwa vuguvugu. Nitaeleza:

1. Wakati rais Kikwete anahutubia bunge kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa 2010, wabunge wa CHADEMA walitoka nje kwa kile walichodai kuwa hawakukubaliana na 'mchakato' uliotumika kumpata rais. Wewe Zitto sio tu hukuingia bungeni siku hiyo bali ulikimbilia kwenye vyombo vya habari na kutoa kauli za (a)kupingana na hatua ya wenzako na (b) kueleza umma mambo yaliyozungumzwa ndani ya kika cha CHADEMA - hiki kilikuwa ni kikao cha ndani.

Wako wabunge wengine wa CHADEMA ambao hawakuafikia hatua ya kutoka nje na kura ilipigwa ili kupata a way forward lakini wewe ulienda zaidi kwa kuonesha utoafauti wako mbele ya vyombo vya habari. Hapa uko na comrades wenzako au uko against them?

2. Siasa za vyama vingi sio uadui. Sasa nilitaka tu kuhoji inakuwaje unaonekana kuwa karibu ki-mkakati na wanasiasa wa chama unachopingana nacho CCM kuliko CHADEMA? Huu ukaribu wako na January Makamba ni kwa sababu wabunge wote wa CHADEMA ni wazee? au hawaelewi kitu? Au you just dont like them? Kauli kwamba unafanya jambo fulani 'bila kujali itikadi za vyama' does not holder water. You are either with your fellow comrades or against them. Hata kama wewe unadhani una uelewa mkubwa kuliko watu fulani fulani ndani ya chama chako unalo jukumu la kuwasaidia ili wafike mahala unapoamini ni pa zuri. Wewe ulianza kidogo kidogo na sasa umepiga hatua nzuri. Uko CHADEMA, do your things with your fellow CHADEMAs. Hawa wengine mnaweza kukutana Rose Garden or elsewhere.

Kwa kifupi niseme unaonekana kujitenga sana na wenzako na ndio maana mara nyingi nimekuwa nasema nampenda zaidi Zitto wa 2007 kuliko huyu wa sasa. Umejiweka kwenye mazingira ambayo unapogombea nafasi ya juu kwenye chama chako watu wanauliza nia na dhamira yako. Hili sio jambo jema kisiasa.
 
nimepoteza imani na zito ambayo nilikuwa kabla. Huyu na mwenzake wamekaa na mwenzake wanaplani kuwaminya watu waliojenga nyumba na kupangisha,eti itaongeza mapato! Wafanyabiashara kibao wanakwepa kodi,madini yetu, samaki wetu, ardhi yetu wanaacha vinabebwa na wazungu. Wanyama wetu,magogo yetu vyote vinaibiwa, kwa nini umuumize mpangaji? Hawajui kwamba ni kutuumiza sie wapangaji? No matter why walikuwa wanadai umri upunguzwe.
Acha upuuzi wewe, uovu hauhalalishwi na uovu mwingine!
 
Some of you are like kids. Hapa ukiniuliza mimi ndio nataka kuwa rais lakini utapata ridhaa ya chama na wananchi? Huo ni mchakato mwingine. Till then lets wait rather than anticipate
 
Mimi i will support Zitto , kama iwe 2015, 2020 or even 2025 . he has what it takes to be National leader .unajua i read what he wrote and nashangaa uoga wa nini kama mnaona hawezi .watu mnamuogopa Zitto kama mzee wangu EL wote hawa wawili wanauwezo na support kubwa inofanya watu waogope
 
mh. zitto

nakutakia kila la kheri ktk fikra zako za siku moja kuwania urais baada ya ridhaa ya FAMILIA yako,chama, wananchi wa jimbo lako na then waTZ kwa ujumla
 
nimesoma makala vizuri, kuna mengi mheshimiwa ameyaandika,

hili la kuzungumza jinzi akina J J Mnyika na Mdee kwenye chadema, ina lengo la kuwajenga ? au ndio kuwabomoa. watu waone kuwa kumbe ni watu walioingia chadema kwa kusit sita, kwa hio ni maopportunist.

mheshimiwa sidhani kama ni sawa kuandika kila kitu kama ulivyofanya, kufanya hivi ni kuwapa nafasi maadui zenu kukumalizeni.

pili punguza sana kujisifu, fanya kazi na umma utaaamua wakati ukifika


nnakushauri kama mmoja alivyokushauri hii mada achana nayo. fanya kazi ukileta mchezo itakugharibia na kukutengenezea maadui wengi zaidi
 
Nimeisoma hii makala nimeielewa vizuri sana.Zitto amechambua vizuri.Lakini nimegundua kitu kimoja ndani ya makala hii ambacho sikuwahi kukijua. Kumbe John Mnyika alikuwa hataki kujiunga na CDM? Kumbe kama sio Zitto Mnyika leo angekuwa historia.
 
Kuna haka katabia mtu ukileta mada humu jf kuna baadhi ya members wanataka ziwe za mapambio ya chama tu hawajui kuna habari nyingine au mawazo yanaweza kujenga na sio kubomoa kama wanavyodhani.

Ushauri wangu endelea kusimamia unachokiamini achana na waoga ambao hata kutumia majina yao wanaogopa!
Hapa kwenye RED umemlenga MM mwanakijiji!!?? kama kutumia jina lako ndio sio uwoga basi una tatizo la ufikiri. hivi unadhani watu wapo hapa kuuza sura!!??......
 
Kwanza niseme wazi kabisa kabisa kuwa Urais ninautaka.

Ninaamini ninao uwezo wa kuwa Rais. Ninaamini nina uzalendo wa kutosha na utashi wa kuleta mabadiliko stahili wa namna nchi yetu inavyoongozwa. Ninajua kuwa nchi yetu imesahau maendeleo ya watu na kujikita katika maendeleo ya vitu. Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo (styles) badala ya mambo ya msingi (content). Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika.

Ninajua nchi yetu inahitaji Uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) badala ya mabadiliko ya juu juu (cosmetic change). Ninajua 'transformation' inahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi na hasa mabwana wakubwa wa nchi za magharibi mfano kuzuia nchi yetu kuuza malighafi tu.

Ninajua rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma ni kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi. Ninajua rasilimali kama Madini, Mafuta na Gesi, Ardhi n.k. ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu.

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom