Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Arumeru ndilo jimbo pekee kwenye uchaguzi wa ubunge, ila nasikitishwa na campaign za uko, zimeelekeza concetration kwenye kupigana vijembe zaidi ya kuzungumzia matatizo ya wananchi na ufumbuzi wake.
Udiwani naelewa CHADEMA wana wagombea vijibweni-Kigamboni DSM, Kiwira-Mbeya, Lizaboni-Songea, Tanga and Kirumba-Mwanza. Nafikiri kuna maeneo mengine pia lakini haya ndiyo ninayoyafahamu.

Asante; ndio maana mwenzenu nimesema wakishindwa huko Arumeru Mashariki uongozi mzima wa Taifa wa CDM NI LAZIMA ujiuzulu! Wamejipa too many distractions in the middle of a battle!
 
Asante sana Zitto, kwa hoja yako hii nimeendelea kutambua ufupi/urefu wa upeo wa watu wengi walio ndani ya JF.
Nadhani ngoja niendelee kutibu watanzania kwanza...
 
[h=6]Mjadala unaoendelea kuhusu umri wa urais ni mjadala chanya kwa taifa letu, kwani umri sio busara, umri sio uchwara na wala umri sio uyakinifu wa maamuzi na kinyume chake, wote mnaotaka kujadili hoja hii ya umri wa urais jikiteni kwenye uwezo wa atakaeogombea na sio umri kwani umri sio kipimo kabisa, tunao wazee walioipeleka nchi shimoni tunao wazee wahuni tele, tunao wazee majizi na wanafiki tel, na kinyme chake pia, kwa hiyo hoja ya umri wa urais izingatie mgombea na uwezo wake tu na sio umri....! pia mwanachadema yeyote anaepingana na hoja ya ujana na urais basi anakosa pia legtimacy ya kumkosoa jk kuwateua watendaji wakuu wa kamati na wizara au tume wenye umri wa uzee, naona tunaanza kununua ngua na kuondoka nazo nyumbani bila kuijpima ndio maana tunajikanganya[/h]
 
wakati mwingine ni hofu ya baadhi ya watu waliotegemea kuupata urais kwa bahati nasibu za mezani ndi wanaohamaki, watu wenye uoga wa ushindani wasio na uwezo wa kihoja
 
Umri usiwe hoja bali hoja iwe uwezo wa atakaesimamishwa na chama, tunao vijana wenye vipaji tele, tunaowazee wahuni tele, tunao wazee waliopeleka nchi shimoni tele, so umri sio hoja
 
Ni uhuru wake na hisia zake juu ya dhamana ya Taifa hili, tutazidi kukuunga mkono kadri utakavyopikwa.Its a gud vision but not 2015
 
Makosa ya Zitto tunayafahamu wote, hivi wana Chadema wote wangeyapuuza makala hiyo, wote wakamuunga mkono Zitto dhidi ya mwandishi wa makala ilomtafuna Zitto wangepoteza kitu gani?..Majuzi kuna makala ilitolewa ktk gazeti la Mtanzania yakidai kwamba Rostam ameipa support Chadema huko Arumeru, lakini sikuwasikia CCM wakirushiana marungu hata mara moja, badala yake waliyadharau makala hiyo na kuendelekeza nguvu zao ktk uchaguzi, CDM tumeshindwa kitu gani?
- Vijana vijana ukomavu wa kisiasa hamna...
 
Mkuu inaitwa hekima. Changamoto ya vijana wetu viongozi siyo elimu wala umri ni hekima. Sasa hekina haifundushwi chuoni wala haiji na cheo. Hekima huja kwa kusahihisha makosa, kwa kujiuliza maswali, kwa kutarajia matokeo na kukaa kimya kutafakari. Hekima ni zao la ukimya. Ndio maana mfalme Suleiman alipopewa nafasi ya kuomba lolote kwa Mungu aliomba hekima. Hakuomba sifa, hakuomba cheo, hakuomba marafiki wala utajiri - alitambua kuwa bila hekima hivyo vingine vyote viko matatani. Tatizo ni kuwa ili kuwa na hekima ni lazina mtu awe na hekima ya kutambua anahitaji hekima.
 
Mkandara,

Uliyosema ni kweli ndiyo maana kuna mahali jana niliwaambia watu wote wanaotumia visingizio vya timing kwamba ati sijui kuna kampeni Arumeru wapuuze basi hii makala.Wote wanajadili kama vile watu wenye hofu fulani,hii mihemko si healthy katika kutoia mtazamojuu ya jambo kubwa linaloathiri mustakabali wa Taifa.Mtu kajibu makala ya mwandishi watu tena wengine ni wasomi kabisa wanalalama.Je,walitaka mwandishi wamakala ile aendelee kupotosha au watu waendelee kuamini kitu ambacho si cha kweli?kwa wale waandishi nguli(simaanishi makanjanja) au yeyote mwenye busara ya pekee anaelewa juu ya falsafa ya reliability na Longevity of an information/story.sasa sijui ni kwa nini busara hiyo isitumike katika mtazamo chanya wa makala ya Zitto?

Umeongelea kuhusu suala la CCM kupuuza ile story ya Mtanzania,sikubaliani na wewe unaposema kuwa ni vijana.Kwenye makala hii ya Zitto umeshuhudia hadi wazee ambao tulitegemea wawe kinara cha kunusuru kampeni zinazoendelea (kama kweli makala ya zitto inaathiri) kwa kuipuuza makala yake,badala yake wamekuwa wakipigana vikumbo kwenye vyombo vya habari kutoa mawazo/matamanio yao juu ya hili jambo.Wapo vijana,wazee,wasomi na waandishi wote wameunga tela.sijawasikia wanaharakati makini kama akina Deus Kibamba,Annanilea Nkya na wengineo wakioongea,kwa muktadha huu i salute them!

Tatizo kubwa hapa ni hofu ya mabadiliko,watanzania tumecharazwa kweli kweli na CCm hadi tunakosa imani/kujiamini kila wakati.Nashangaa ni watanzania wa aina gani waliokubaliana na wimbi la mageuzi ya kisiasa,kiuchumi na kijamii kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi9oh kumbe matakwa yao yalipinduliwa -coup civillien kwa kukataa mfumo wa vyama vingi kwa asilimia 80).Nashanga ni watanzania gani waliokubali masharti ya SAPs ,nashangaa ni watanzania wa aina gani waliokubaliana na masharti ya uwekezaji kiholela.

Nadhani tunaweza kufanya uitafiti kutafiti resistance ya watanzania dhidi ya doctrine ya ujamaa na kujitegemea ambayo baadae walikuja kuishabikia na kuijutia lilipokuja azimio la Zanzibar na kufeli sambamba na matumizi ya fedha na kushamiri kwa ufisadi wa kutisha serikalini na uzembe wa daraja la kwanza

. Mkuu wangu Mkandara,Tatizo ni kubwa kuliko tunalofikiria.siyo Zitto,siyo timing na wala siyo hekima na busara za vijana

Natoka kidogo online niko safarini charge inaniishia,niombee safari njema!
 
Wakuu muwe mnapita na kwenye sub forum ya CHAGUZI NDOGO kupaya updates za campaign
 
Mkuu inaitwa hekima. Changamoto ya vijana wetu viongozi siyo elimu wala umri ni hekima. Sasa hekina haifundushwi chuoni wala haiji na cheo. Hekima huja kwa kusahihisha makosa, kwa kujiuliza maswali, kwa kutarajia matokeo na kukaa kimya kutafakari. Hekima ni zao la ukimya. Ndio maana mfalme Suleiman alipopewa nafasi ya kuomba lolote kwa Mungu aliomba hekima. Hakuomba sifa, hakuomba cheo, hakuomba marafiki wala utajiri - alitambua kuwa bila hekima hivyo vingine vyote viko matatani. Tatizo ni kuwa ili kuwa na hekima ni lazina mtu awe na hekima ya kutambua anahitaji hekima.
Ni kweli hekima haina umri lakini tusipuuze nafasi ya umri kwa mwanadamu na kujifunza! Wanaotetea umri muafaka watuambie umri ushushwe hadi miaka mingapi? Nakubali anaweza kuwepo kijana wa umri mdogo akawa na uwezo mkubwa kiuongozi lakini kijana huyo akiendelea kuandaliwa,kupikwa kuongoza nchi huoni italeta mtu mwenye ukomavu wa pekee? Hivi vijana tukisubiri hadi umri muafaka(bado naunga mkono wazi miaka 40) tutapoteza nini? Tunakimbilia nini ikulu? Hivi matatizo ya Tz ni kwasababu ya umri wa Rais? Hebu tuache unafiki tuwe wawazi kama tunaipenda nchi yetu.naomba nitajiwe kijana anayeonekana ni kiongozi super kweli hadi tunaona tushawishi wananchi umri ushushwe? Inawezekana kuna malaika! Najua hapa tunapiga kelele na mpango uliopo ni kushusha umri lakini lengo lake halitatimia!
 
Acha fikira za hovyo hovyo! Jadili kilicho kwenye mada usimjadili mleta mada, na kama ukigundua kuwa mleta mada ni m-chadema utafanya nini?! Bofya hapa upate uhakika Mohamedi Mtoi | Facebook

Yeye pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM na Mnyika ni baadhi ya vijana wenye mvuto mkubwa wa kisiasa na ushawishi. Kama Katiba mpya itashusha umri wa kukombea uraisi mimi sioni tatizo kama Zito atajitokeza. Kiwango chake cha elimu na upeo wake wa kutazama mambo mbalimbali ya kimaisha vinampa uwezo na sifa ya kuongoza nchi. Mengine tuwaachie chama chake waamue wakati utakapofika
 
Umeongea mengi sana, na umeonesha nia ya kuiongoza Tanzania. Hii ni haki yako kikatiba pale wananchi watakapoamua kukupatia ridhaa, lakini nakushauri my brother ufanye yafuatayo kabla ya 2015
1) Kuwa mtulivu achana na mambo ya media, fanya kazi kwa uzalendo kama mtanzania na naamini utapata coverage ya kutosha bila hata ya kuhonga senti tano.
2) Wewe ni mtu mzima mwenye heshima kubwa katika jamii, achana na mambo ya club na kina wema sepetu ambao kila leo wana scandal za ngono kwenye magazeti ya udaku. Sisemi kwamba ujitenge na jamii unayotarajia kuiongoza ....la hasa nia yangu ni kukushauri uchunge sana image yako isichafulie kwa kujichanganya na aina ya watu ambayo hata jamii inawaona hawana maadili.
3) Achana na unafiki, nikikuuliza siku ile Steven wassira alifuata nini nyumbani kwenu tena na private car....utajibu nini? Siku ile ambayo pia na Mdogo wako Rukia alikuwepo nyumbani.....?????
Ni hayo tu bro Zitto.
 
Umeongea mengi sn mwandishi lkn la muhimu ni hilo la mwisho zitto awajibu watz wasira alienda kufanya nini nyumbani kwake?
 
Watu wanamtuhumu Mh Zitto kuwa anatumika sana kuleta migogoro isiyo ya lazima kwenye chama chake, Hajawahi kukanusha ama kukubali, laki hii asipoijibu ni uthibitisho kuwa ni mnafiki na anatumiwa na Mafisadi kufikia malengo yao, haya na sasa achomoe na hili la Rushwa na kutetea Mafisadi na wezi
Umeongea mengi sn mwandishi lkn la muhimu ni hilo la mwisho zitto awajibu watz wasira alienda kufanya nini nyumbani kwake?
 
Zitto anawashughulisha sana watu inaonyesha jamaa anaogopewa sana! Anyway tutaona na kusikia mengi kuelekea 2015
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom