Wanajf wenzangu assalaam aleikum! imekuwa ikijadiliwa kila mara humu jamvini kuwa ZITTO anautaka urais, swali langu ni kwamba anataka urais wa awamu ya ngapi?. Lakini pia nimekuwa nikiwasikiliza watu wenye mahaba binafsi na zitto wakisema eti watu hawajamwelewa zitto,kwanini haeleweki,na je ni kweli kuwa hawajamwelewa au yeye ndo hajaelewa watu.Na kama anautaka urais ni kwa kupitia chama gani? Na kama ni kupitia cdm,je njia anazotumia zitamfanya atimize ndoto zake? Na amejuaje kama katiba ijayo ita-regulate umri wa kugombea urais? Na kama yote hayo nimeyasema kwa sababu sijamwelewa,je haoni sasa ni wakati wa kunifanya mpiga kura wake nimwelewe? Nilimpenda sana zitto jamani na hata nilikuwa nikimwona anazungumza nasisimkwa, lakini kwa mwenendo huu wa sasa ambao kwake yeye kuutaka urais ni kwenda kinyume na wenzake kwa mambo ya msingi,basi itanichukuwa mda kumwelewa.
1)Kutoonekana sana kwenye M4C
2)kutounga mkono uamuzi wa cdm kutomtambua jk
3)kuunga mkono malipo ya tanesco kwa dowans kinyume na msimamo wa chama
4)Kuungana na jk ktk mazishi ya dictator zenawi
Haya yote na mengine mengi tunalalamika tu kwa sababu hatujamelewa? Tutamuelewa lini wakati bado miaka 2 tu ya uchaguzi mkuu. ZITTO kama upo humu nifanye nikuelewe katika haya.
Mkuu just give zitto a break kwani hata yeye ana haki ya kugombea nafasi ya urais kama alivyo Mbowe au Slaa and any other CDM member.
Pia hizi pia hizi dialogue hebu tuzuache na tujenge chama chetu.
Most tuwaheshimu viongozi wote wa chama ikiwemo na Zitto.
Kaka chama hakijengwi kwa tofali na mchanga,kinajengwa kwa hoja.Tutampa break kama na yeye ataamua kutupatia break, maneno hujenga,napenda nimwele zitto anataka nini? kama unafahamu vema niambie tu na hutoniona tena nazungumza habari za zitto.Hakuna aliyemnyima haki ya kugombea,lakini naomba nikuulize,unaridhika na juhudi za zitto katika kujenga cdm ambayo mimi na wewe ni wanachama waaminifu?Mkuu just give zitto a break kwani hata yeye ana haki ya kugombea nafasi ya urais kama alivyo Mbowe au Slaa and any other CDM member.
Pia hizi pia hizi dialogue hebu tuzuache na tujenge chama chetu.
Most tuwaheshimu viongozi wote wa chama ikiwemo na Zitto.
Wewe ndio udini unakusumbua, hakuna cha Slaa hapa.Kinachokusumbua wewe ni udini tu. Jaribu kuangalia habari imetoka wapi sio kukurupuka. Labda anaongelea urais 2025 Dr Slaa akishamaliza vipindi vyake, which kila mwana CDM atamuunga mkono. Lakini kwa sasa Zitto HAJAKWIVA kuwa rais na hata katiba haimruhusu
mchukue ukanywe nae chai huko chama cha mabwe pandeNa kwa cdm huyu ndio mtu anae faa kuwa Rais. Wengine wote wakina M & S Company wana tamaa tu za madaraka. Nawaomba wana cdm muungeni mkono Zitto na apitishwe na chama
Kuna wakati Zitto alituhumiwa na mdau hapa mtandaoni kuwa anamiliki Ghorofa Dodoma maeneo ya Kisasa. Alijitokeza mwenyewe humu jamvini akakanusha kwa nguvu zote hadi wengi tukajiridhisha kuwa anasingiziwa.
Sasa kwa ishu km hii ya Wassira kufika nyumbani kwa Zitto inaleta utata kidogo maana kama ni urafiki-HAPANA. ni urafiki gani uliopo kati ya Nuru na Giza, Uhai na Kifo...ni wazi hakuna!
Zitto, tolea majibu kwa haya mambo yanayoleta kiwingu katika safari yako ya Kisiasa.
Zitto anafaa na ana
uwezo mkubwa sana, ila swala kubwa ni alama za nyakati ndizo huamua.
Yeye azisome tu na wakati muafaka ukifika ataupata tu huo Uraisi.
Singependa sana kumkatisha tamaa. Ana nafasi kubwa ya kuupata, ila
asikurupuke.
Zitto anafaa na ana
uwezo mkubwa sana, ila swala kubwa ni alama za nyakati ndizo huamua.
Yeye azisome tu na wakati muafaka ukifika ataupata tu huo Uraisi.
Singependa sana kumkatisha tamaa. Ana nafasi kubwa ya kuupata, ila
asikurupuke.
hebu mpeni haki yake mh Zitto naye ajaribu....mh Mbowe alijaribu akashindwa.......dr Slaa naye vilevile.....tunahitaji sura mpya.....tena itaondoa dhana ya udini ndani ya cdm.....siyo kila siku walewale....tuko watanzania zaidi ya milioni 40...hakuna chuo kinachotoa elimu ya urais