The Hunter
JF-Expert Member
- Dec 25, 2010
- 1,049
- 307
Tuna tatizo la kufagilia watu kishamba ndio maana watu uhishia kujiona special, Zitto asimami wala si hata nusu ya mchambuzi kisiasa tazama walipo kwenye ufahamu wakijamii kuhusu hawa wanasiasa wawili. Ndio Khali.Watanzania basi angalau tuwe tunafanya kazi za kutupa kapiriensi katika mambo ya utendaji. Unamaliza shule. Unaingia kwenye siasa na unataka urais. Lini tunapata rais aliye na uzoefu wa viwanda, biashara au uchumi?
Na kwa cdm huyu ndio mtu anae faa kuwa Rais. Wengine wote wakina M & S Company wana tamaa tu za madaraka. Nawaomba wana cdm muungeni mkono Zitto na apitishwe na chama
Zitto anafaa walau kuanzia 2025 atakuwa amepikwa na kukomaa vizuri.Kwa hivi sasa ni nafasi ya Dr Slaa.Dr Slaa kwa sasa hana mbadala ndani ya CDM.Ni kujilisha upepo kudhani kuna mtu mwingine atapitishwa kugombea Urais zaidi ya Dr wa ukweli walau kwa sasa.CDM ina vijana wengi na hakika huko Mbeleni kina Zitto na Mnyika na wengine ni hazina kubwa ya chama
Mkuu kuna tofauti kubwa kati ya umaarufu wa Zitto na JK. Zitto ameonyesha kuokosoa serikali na kujenga hoja zinazokubalika, sijui JK alijenga hoja gani zilizompatia umaarufu ukilinganisha na Zitto.Mimi namkubali Zito kuwa kiongozi mwenye umakini wa hali ya juu, lakini dhana inayojengeka hivi sasa ya kudhani kila kiongozi mzuri ni lazima awe katika ngazi ya urais siiungi mkono! Mtazamo wangu kiongozi mwenye kuleta mabadiriko anatakiwa kutoka katika chama chenye dhamira ya kufanya mabadiriko, ambamo wabunge wake, madiwani, pamoja na wafuasi wake wote wataamua kuyaendea mabadiriko. Na wala si msimamo wa mtu mmoja. Tunayashuhudia yanayotosha kuwa mafundisho. Kiongozi anakuwa na dhamira ya kufanikisha jambo lakini anakosa uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wahafidhina wa kwenye chama chake au jamii. Katika mazingira kama hayo ni rahisi sana Rais kugeuka DIKITETA. Ninaipenda mno kazi anayoifanya Zito hivi sasa ya kuipa challenge Serikali kwa kuukosoa utendaji usiofaa wa Serikali na kutoa shule pana kwa uma kuujua udhaifu wa serikali kwa upana wake katika sekta mbalimbali.
Hilo ndilo linalomjengea Heshima hivi sasa na kumpa umaarufu. Sitashangaa umaarufu huo ukipungua sana baada ya kuupata urais. Umaarufu aliokuwa nao JK kabla ya urais si huu alionao leo!
Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.
Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!
Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.
Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com
Mkuu Nyerere alipohutubia pale Kilimanjaro hotel alisema watu wanaoutaka urais wajitokeze mapema ili watanzania wawapime. Pia alikosoa mfumo wa CCM wa kukaa kwenye halmashauri kuu na kutoa majina matatu na siku hiyo hiyo yanapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu bila hata kuwapa wajimbe hao fursa ya kuwapima. Nyerere hakukataza watu kujitokeza ila iliwaonya wale wanaojitokeza kwa hila na hasa wakiwa wanatumia pesa.Swali kwa zito & pro Zito plus mamluki wa ccm- je kwa sasa ina maana haujaona mgombea yoyote anayefaa zaidi yako??? Umekuwa ni mshabiki mkubwa sana wa panafricanisim kama Mwalm /yerer na umekuwa una kili Nyerere ni role model kwako-e unasemaje kuhusu onyo la mwalm Nyerere kuwa tuwaogope watu wanaokimbilia ikulu?? Kwa sasa naomba niishie hapo tu ndugu japo nina mengi!!
Mkuu nadhani Zitto amekumbushia tu. Nakumba 2010 wakati anaomba kura kule MWandiga aliwaambia wazi wazi wapiga kura wake kwamba hiyo ni mara ya mwisho anaenda pale kuwaomba kura za ubunge, akirudi atakuwa akiwaomba kura za Urais. Pia mkuu uchaguzi wa Arumeru unasimamisha mambo yooote hapa nchini? Yaani watu wanatakiwa wakiamka ni Arumeru wakila ni Arumeru? Twende navyo kwa pamoja Arumeru na mambo mengine pia.Mwanzoni nilifikiri Zitto alikuwa ameandikia article kwa unknown news media. Lakini gazeti la Mwananchi Jumapili limeandika hii habari kwa kina na according to this paper ni kwamba Zitto alifanya nao mahojiano! Infact kule Mwananchi Sunday Zitto more explicity kuwa 2015 anautaka urais!
Shida niliyonayo hapa ni timinig. Kwanini Zitto ameamua kuwa kwa sasa mjadala unaofaa ni kuhusu mikakati yake ya kupata urais wakati anajua kuna uchaguzi huko Arumeru? Amebadilisha public dabate kabisa kwanini?
Mimi namkubali Zito kuwa kiongozi mwenye umakini wa hali ya juu, lakini dhana inayojengeka hivi sasa ya kudhani kila kiongozi mzuri ni lazima awe katika ngazi ya urais siiungi mkono! Mtazamo wangu kiongozi mwenye kuleta mabadiriko anatakiwa kutoka katika chama chenye dhamira ya kufanya mabadiriko, ambamo wabunge wake, madiwani, pamoja na wafuasi wake wote wataamua kuyaendea mabadiriko. Na wala si msimamo wa mtu mmoja. Tunayashuhudia yanayotosha kuwa mafundisho. Kiongozi anakuwa na dhamira ya kufanikisha jambo lakini anakosa uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wahafidhina wa kwenye chama chake au jamii. Katika mazingira kama hayo ni rahisi sana Rais kugeuka DIKITETA. Ninaipenda mno kazi anayoifanya Zito hivi sasa ya kuipa challenge Serikali kwa kuukosoa utendaji usiofaa wa Serikali na kutoa shule pana kwa uma kuujua udhaifu wa serikali kwa upana wake katika sekta mbalimbali.
Hilo ndilo linalomjengea Heshima hivi sasa na kumpa umaarufu. Sitashangaa umaarufu huo ukipungua sana baada ya kuupata urais. Umaarufu aliokuwa nao JK kabla ya urais si huu alionao leo!
Swali kwa zito & pro Zito plus mamluki wa ccm- je kwa sasa ina maana haujaona mgombea yoyote anayefaa zaidi yako??? Umekuwa ni mshabiki mkubwa sana wa panafricanisim kama Mwalm /yerer na umekuwa una kili Nyerere ni role model kwako-e unasemaje kuhusu onyo la mwalm Nyerere kuwa tuwaogope watu wanaokimbilia ikulu?? Kwa sasa naomba niishie hapo tu ndugu japo nina mengi!!
mi sio mwana CMD ila zitto akigombea hakyamama nampa kura yangu . hii itaondoa manee kuwa CMD ni chama cha wachaga na wakristo.