Kwanini unaamini hivyo?@mushi
Zitto hawezi kupata urais kupitia chadema NEVER.
Maximum they can offer ni kumsaidia Mbowe na Slaa beyond that anahatarisha uanachama wake chadema..
Tatizo dogo hajui na ni mbishi..
Kwanini unaamini hivyo?
Mkuu Mwanakijiji,
Hizi soga za wanajamvi hapa zinazuia nini kule arumeru? La muhimu makamanda wanaendeleza mapambano.
Huyo anayejiita msomi wa chuo kikuu haikuwa sawa kumsema Zitto mambo ya uongo, ilikuwa sahihi Zitto kumjibu.
sitampa kura yangu na wala hatutampitisha.
Georgina ni muislam kwa sasa
Huyo mchagga unamsema wewe? kama yupo ajitokeze tu tutamshambulia Lipumba..lakini kwasasa hakuna mwanamume aliyesema georgina na mke wake kama asemavyo mahimbo na josephine
usipindishe mada mkuu Slaa anazini au mnataka kubadili maandiko kwasababu ya mahaba, kwani si ajabu kwenu maana kuna kanisa limeshakubali shoga kuwa priest..just declare..
Urais unakutafua mhusika, Urais hautafutwi!!Tizama Pichakula kwa mtindo said:Hadithi yako inatufundoisha nini?
ukweli mada ni defu sana kiasi mtu unaishia njiani kusoma. Nimeelewa kuwa urais unauhitaji na kwa namna fulani unaweza. Kama jakaya kaweza (?) why not you? Kuna hoja hapo juu ya mdau kuwa katiba inasema ni miaka 5 then 5. Sasa kama umefanikiwa kuongoza miaka 10 ukawa na miaka 50 then tutegemee nini? Si uchakachaji tu hapo? Miaka 50 kustaafu urais bado mdogo sana! Zitto utakuja kuwa Rais. Take it from me if the party maintain this pace, ila kwa sasa hata chama kitakukatalia. Wananchi wanaweza kuwa na mahaba nawe kwa sasa na wakasema uwe Rais lakini madhara yake mbele mabaya. Ukiwa na miaka 50 utakuwa Rais. Jiandae kwa urais 2025
Ndio tatizo lenu watu wa kaskazini mnalazimisha Slaa 2015 agombee urais ili hali atakuwa mzee na hatufai tena. Na isitoshe mzee hana jipya kwa sasa, awaachie vijana wakina Zitto. Kuhusu umri katiba ijayo tunalirekebisha hilo na Zitto ambae ni chaguo la CDM wengi ata qualify.
Haijasemekana ni nani atapeperusha bendera ya cdm mnamo miaka 3 ijayo, hivyo hakuna sababu ya kuzibana vinywa muda huu. Kama hujui ni kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Wanaogawanyika hawana misimamo
Je mjadala huu tija wiki hii ambamo Chadema imo vitani kule Arumeru? Ningetamani mjadala huu uanzishwe na mtu mwingine hasa wa CCM anayetafuta ku-divert attention ili watu tusiangalie yanayotokea kule Arumeru. Kwamba, mjadala huu unaanzishwa na mwana Chadema inatia shaka sana. Tuuweke kiporo, tuanze nao tarehe 2 April baada ya kujua mbivu na mbichi huko Arumeru.
Kwa faida ya CHADEMA wafike sehemu huu upuuzi unapaswa kwisha kwa kuwa kuendelea kufuga kidonda ni kukalibisha magaonjwa na hatimae kilema.Kwa sasa Zitto kuingiza CDM kwenye michezo hii ni kutengeneza mazingira ya kuinyongonyeza CDM kisayansi,hivyo wanachedema kwa kuwa lengo ni ukombozi someone should stop this kind of game,manke watu wazima ambao imewachukua karibu miaka ishirini na ushee kusimamisha chama leo ambacho kinainyima CCM usingizi kisha wanaibuka vijana kuanza mbwembwe zisizo na nidhamu na maadili hata kama ujana ni maji ya moto heshima nayo ni mlango wa adabu.Mimi naamini kila mtu anao uhuru wa kusema anautaka uraisi, hii ndio freedom yenyewe. Lakini timing ya kauli kama hizi ndio inayoleta maswali ya kujiuliza pengine wengi wetu tunaishia kukosa majibu. Hiki kijitabia cha mtu kuona watu wanamuandika andika kwenye magazeti kila siku akafikiri kila kitu anaweza ni hatari sana. Mh. Zito anakurupuka mambo mengi sana, siasa makini haziendi namna hiyo, mtu anajengwa kwenye chama na kuna wakati unafika unakuwa automatic choice, sio lazima ujitangaze bila taratibu.
Wakati ule anataka kugombea uenyekiti, ijapokuwa ni haki lakini mtu unajiuliza hivi kweli kwa umri wake wakati ule tuseme 33 hata ukiupata huo uenyekiti je unaweza kuvutia watu wa rika zote kujiunga na chama? je umekomaa kiasi cha kutosha kuweza kuhimili hiyo nafasi? Hekima nyingine jamani zinakuja na umri, kwa nchi zetu za kiafrika na tamaduni zake Mh Zito bado hawezi kukabidhiwa chama akiongoze, ni mtu anayetakiwa kulelewa na kukuzwa na chama kwa ajili ya miaka ijayo.
Hata nafasi anayosema anaitaka ya uraisi bado mda wake, he is not matured enough. Amelewa sifa na anatumiwa vibaya. Chadema lazima msimame makini na mtu wa namna hii, akileta za kuletwa mnafanya maamuzi magumu maana he always create unnecesary distractions. Chama ni taasisi lazima kiheshimiwe kama taasisi, chama kinapogeuka kuwa ni majina ya watu huwa hakina muda kinakufa. Kunao watu wengi tu, wazuri wenye mvuto mkubwa wa kiuongozi ijapokuwa huwezi kuwasikia kwenye magazeti kila kukicha, wapewe nafasi.
Chaguzi ndani ya vyama ziwe mahali ambapo talents zinavumbuliwa, mtu anasikilizwa hoja zake,vision zake na strategies zake na kama ziko convincing mtu apate nafasi, sio hii tabia ya kushabikia majina yasiyo na chochote ndani yake. Ndio maana vyama vya siasa huwa vinakufa maana vimejengwa juu ya majina ya watu. Ati watu wanakuwa na makundi, upuuzi mkubwa kabisa huu badala ya kuangalia ni nani anatoa sera za maana yunashadadia majina, mara Zitto, mara Slaa mara Mbowe n.k Haiwezekani mtu ambaye ni mwanachama wa kawaida tu wala hana kashfa wala nini akapewa nafasi mbele ya kamati akajieleza akapita kwa ubora wa hoja zake! lini tutafika hapo?