Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
kweli shepu ya kabwe zitto anaweza kufungua ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Israel akiwa raisi wa URT?
 
Msiwe wavivu wa kufikiri. Zitto hajasema anataka urais kwa kuwa yeye ni kijana,bali anataka urais kwa kuwa ana uwezo. Na ameweka clear kabisa,atafanya hivyo(kugombea) endapo chama chake kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CDM,na endapo wananchi watakubali kuwa anafaa. Kipi hamjaelewa? Wakati mwingine tujaribu kushirikisha ubongo kufikiri kidogo!..

mkuu mala kwa mala nimekuwa nikiwaeleza wanajamvi kuwa wanatakiwa kusoma maandiko na si kusoma tu na kuyaelewa pia.

lakini tatizo lilelile lina jitokeza kuwa watu hawasomi na kuelewa na mwisho wa siku ni kuchangia kwa kuangalia aliyeanza kutoa mchango kasema nini

kazi ipo hapa

ni vyema ndani ya JF kuwe kunaleta post ambazo zipo wazi zisizo hitaji kufikirisha akiri ila kuwepo uchangiaji ulio sawia
 
Msiwe wavivu wa kufikiri. Zitto hajasema anataka urais kwa kuwa yeye ni kijana,bali anataka urais kwa kuwa ana uwezo. Na ameweka clear kabisa,atafanya hivyo(kugombea) endapo chama chake kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CDM,na endapo wananchi watakubali kuwa anafaa. Kipi hamjaelewa? Wakati mwingine tujaribu kushirikisha ubongo kufikiri kidogo!..
Mkuu nadhani wewe ndo hujaushirikisha ubongo wako.
 
mpasuko kwako peke yako! nothing new! it seems u hav paid!
 
Naungana na Mh. Zitto, ukomo wa umri ushuswe. Tusimwongelee mtu fulani bali tujifikirie kama taifa, je kuna ukweli wowote kwamba busara za kiuongozi zipo kwa wazee pekee? Mbona Wasira na wazee wengine wengi tu hawana busara? Tunajiogopa wenyewe, kwamba hatujui utashi wetu? Tufike pahala pa kujadili hoja na sio mtoa hoja.
 
Kamanda ZITTO unanishangaza sana, viongozi wenzako wapo ARUMERU wanapambana kuakikisha NASSARI anashinda, macho na maskio ya wanachadema na wapenda haki yanangalia ARUMERU kinachoendelea, wewe uku unaleta UPUUZI (samahani nimekosa neno nzuri la kusema) wa URAISI.

Mwlimu Nyerere alisema tumuogope mtu anayekimbilia IKULU, IKULU pana nini pale?

ZITTO unakumbuka 2010 Dr SLAA akuomba chama chake kimpitishe kugombea URAISI bali wanachadema wenyewe walimuomba DR asimame ktk mtanange?

Tujenge chama chetu tuachane na mambo ya URAISI
 
yaani sasa hivi mnachoweza kuandika humu nyie vibara wa NAPE ni mambo ya chadema tu kwa lengo la kutaka kuvuruga.ila stahili hiyo bado naona ni ngumu kwenu,mlishajaribu hata ya kutoa pesa lakini na yenyewe haikuleta matokeo tarajiwa,anyway uko kazini endelea tu wewe mleta thread hii
 
Yani we ndio hufai kabisa sababu unatumia mas.. i yako kusoma. Na kwa taarifa yako sio wote ambao hatumsupport zitto ni CCM. mi CDM pure. Lakini kwa uongozi wa juu au uwakilishi wa juu katika chama mi binafsi nasema zitto ni BIG NO!!.
Wewe pia unatumia hayo yako kusomea... Mie sijakuuliza wewe unatoka chama gani hivyo usijipendekeze kunifafanulia!

Nakubaliana na wewe kuwa Zitto ni big 'NO' afu wewe ni big 'YES'
 
Nadhani Zitto amesema vema ukisoma kwa makini katika andiko lake.

"Hata hivyo kazi hii hata kama naitaka ni lazima wenye nchi waamue kunipa kazi hii. Ni lazima kwanza Chama changu kiseme wewe ndio mwanachama unaestahili kuifanya kazi hii. Ni lazima Watanzania wengi waseme wewe ndio mwananchi mwenzetu unayeweza kuchukua jukumu hili. Kuitaka tu haitoshi. Ni lazima wananchi wakuamini na kukupa jukumu hili. Sasa kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au hata 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo".

Bila shaka ataendelea kuwa mtu wa kuheshimu maneno yake na in 2015 ataheshimu uamuzi wa watz kuwa Dr.Slaa ndo chaguo lao though katiba ikibadilishwa atakuwa na uwezo wa kugombea. Pamoja na ushawishi wake hajafikia level ya Dr.Slaa kwa umakini na uwajibikaji
 
Zitto angekuwa na uhalali wa kuishikia bango hoja hii kama yeye mwenyewe asingeonyesha hamu ya cheo hiko. Vinginevyo anachokifanya sasa hivi ni kututaka wa-Tanzania tupunguze umri kwa faida yake mwenyewe! Hivi yeye ni nani na kafanya nini haswa cha kutufanya tumuhitaji kivile?

Na kama anaanza katabia haka cha kuwashawishi watu wampendelee yeye kwa kushusha umri, anakuwa na tofauti gani na Marais walafi kama akina Wade na Yoweri waliosukuma mabadiliko ya katiba kuwapendelea wao? With all due respect...mjadala huu umetusaidia kujua kilichomo ndani ya huyu kijana. Kesho na kesho kutwa akiupata Urais atatushawishi tugeuze katiba ile agombee kwa awamu ya 3 na ya 4 na kadhalika.
 
Hii nikazi ya usalama taifa wanapima upepo so wala msiumize vichwa.chadema wote wapo makini yeyote tuta muunga mkono.sisi tupo makini zaidi yao watabaki kuangaika izi abari niwezitoa wapi.wana chadema tulieni,bado naendelea nakazi.
 
AKSANTE BEN KUMBE SIKU HIZI WEWE NA ZITO MNA [BENZITO -ALLIANCE ] YANI BEN AND ZITTO-ALLIANCE=COALITION.
I doubt kama umesoma makala husika kwa umakini .Sijui umefikiaje hitimisho hili.Tujenge hoja tuache kujadili kitu kwa kuzunguka mantiki au nje ya mantiki(logic)

Ok nilitegemea kumuona Zitto lakini nimeona thanks yako na quote yako hapo juu.Hakika kabla ya hii mada thread kuwa hewani siku chake zilizopita nilichangia thread yenye kumuhusu zitto hii hapa chini, ambayo nilimtetea zitto toka kwenye thread ya Dk K kama ifuatavyo;

Dk k umezungumza jambo ila sijui ndani yako unadhamira gani Je ni dhamira ya kumjenga Zitto au Kumboa Zitto.Kwa kuwa maneno yako kwa namna fulani yeye binafsi Zitto akiyafanyia kazi na kujiangalia pengine unaweza kumsaidia.Kwaa sasa baadhi ya wancdm humu ndani wanakuona wewe kama mnoko fulani,lakini kwa mwanasiasa makini [Ambako mpaka sasa Zitto ajafika kuwa mwanasiasa makini japo analazimisha kuonekana kuwa mwanasiasa makini] maneno yako yangekuwa tiba na yeye kuyatumia kama kioo chake cha kupima jinsi jamii ya waelewa wengine wanamuonaje.

Moja ya tatizo la Mwanasiasa asie makini ni kutokuwa mwepesi wa kusikia mambo hasi [Negative Issues] zinazomuhusu yeye binafsi na utendaji wa mambo yake mazima kwenye mambo ya kisiasa.Wanasiasa makini daima uwa awasikilizi sifa zao utendeaji wao ,kwa kuwa sifa kwao ndio sehemu ya wajibu wao,Mwanasiasa makini daima uwa mwepesi kusikia maadui zake wa kisiasa na wakosoaji [Critics] wake wanasemaje kumuhusu.Kwa kuwa daima wakosaji wanakuonyesha mapungufu yako na kisha mhusika kutumia nafasi hiyo kunyoosha kisha sifa zinaludi palepale kwake kwa kuwa sifa kwake yeye ni wajibu sio kiburi au ujivuni.

Mwanasiasa mashuhuri na waziri mkuu wa Uingereza haijapata kuona Sir Churchill,alikumbana na wakosoaji kibao ndani ya maisha yake wakati wa harakati zake za kisiasa ikiwemo kuwa hana kiingereza kizuri,pata picha mwingereza anaambia hana kiingereza kizuri,kwa kuwa Sir Chuchill mwanzo wa ujana wake aliishi India kama mwakilishi wa serikali ya kikoloni ya waingereza hivyo kuathirika kwenye matumizi ya kizungu chake,pamoja na yote ndiye waziri mkuu bora kupata kutokea ndani ya ardhi hiyo ya markia.

Hivyo yanayosemwa kuhusu Zitto,kama atachukulia kuwa ni majungu na kuwa yeye yuko sawa uwo wote unaosemwa ni wivu wa kike,hakika ndani ya miaka kumi ijayo itakuwa imekula kwake.Zaidi akitaka kuwa Mwanasiasa makini yampasa kweli kubadilika na kuwa REAL MAN,mtu anaetembe kwenye kile anachoamini na si kufanya mambo ndani yake kuna migongo ya watu fulani,yampasa kuwa FREE MAN,kwa kuwa mtu aliye wazi daima ujisimamia,yasemwayo yapo kama hayapo yaja.Kuna jambo moja ambalo daima sijaliona kwa zitto ni mahusiano yake na baadhi ya vijana na watendaji wenzie ndani ya CDM.Ndoto zake haziwezi kufika popote bila ya kujipanga toka chini ukiwa na watu ambao wenye macho [Anawajua] yao wanaweza kuingiza mkono kukusaidia wewe na timu yako kufikia dhamila ya ndani,ikibidi wanauwezo wa kumpa support ya watu kutumika ili kutimiza dhamila yako kama kweli wanaiona ni GENEUINE.

Lakini ili la kujifanya mimi ndio mimi,the youngest CDM .........P Material ndani ya Nchi hakika atatumika vibaya na mwisho wake uenda ukawa mbaya sana na kuathili maono [vision] za vijana wengi sana.Kuachwe kale kauarrogance na stubborness kwa chama chake.Miaka ya tisini na ushee [1994s] kulikuwa na mwanasiasa machachali sana kwa jina la Amani Waridi Kabul hakika leo ni simulizi kwa Watanzania,kiasi kuwa wananchi hata hawana kumbukumbu zake kuwa alichangia sana kuinua CDM.Lakini ndani yake kulikuwa na kale kale katabia ka arrogance na stubborness hatimae ndio hivyo sijua kama yupo Bongo au alishaludi Marekani kufundisha.

Zitto usije ukaludi vyuoni kufundisha watch out,sikia...............jitahi di sana kusikiliza.........Pia tabia ya yeye kuonekana wazi wazi na watu ambao kwa namna nyingine wananchi wa kawaida hasa wana CDM watapokea mwonekano wake huo na wahusika kama USALITI.Na hata mimi binafsi sipendi tabia hiyo kumuona mtu ambae upande wa pili namuona kama opponet [rival] kisha the other side ndani ya timu anaonekana wazi wazi anamawasiliano ya wazi na dhahiri basi ni vyema mhusika akaamua kucheza American Sytle "IF YOU CANT DEFEAT THEM JOIN THEM".

Zitto is to young na anaitajika sana kujipanga na haya mengine ya siju.............kiti na vingora avipe muda miaka ishirini toka sasa,ajipange hata vijana wenzie kwa sasa watamuelewa sana hapo na kumuona kweli kaiva.Hata JK hapo alipo hakufika hivyo amepikwa akapikwa pata picha graduate unatupwa Lindi polini kisha watu wanauchubua,wala hawana time na wewe,wanakutoa hapo wanakurusha sijui Zanzibar wanakupotezea.Hayo yote ndio uzoefu wenyewe uliomfikisha hapo na ndio kiongozi anavyopita na kufundwa.

Tusikulupuke na ujana na mengineyo,daima ujana unatufanya siku zote kuwa over ambitious na kuona kila jambo tunaweza na kumbe mambo mengine hayaitaji nguvu za ujana bali busara za ujuvi wa hali halsi ya Kidunia,ambayo mhusika uwa ameshajifunza kupitia misukosuko kadha wa kadha yakiwemo majaribu ya makusudi ili kumfanya imara na mwenye uwezo wa kuamua mambo muhimu juu ya mamilioni ya watu wanaotegemea uamuzi wake kama ndio jibu kila mwisho la utatuzi wa hatima ya jamii.

Hivyo yanayomjenga Zitto, yasichukuliwe kama chuki kwa baadhi bali kama nafasi adimu ya yeye kujijua na kuona kioo kingine kinamuonaje.

Haya Ben ushauri wangu uliotaka kwa chama cha BENZITO-ALLIANCE AND COALITION, NILISHATOA HATA KABLA YA THREAD HII LEO SIKU KADHA HUKO NYUMA,MLISHA SOMA NDIO MKAAMUA KUJA NA TEAM YENU YA MAMR POPULARITY.

Mimi ni kijana kama ninyi,lakini uwa sisupporty ujana ovyo ovyo kwa kuwa nimejifunza kuwa unaweza ukawa kijana wa miaka kumi na nane akili zako zikawa sawa na Mzee asie na busara na hekima mwenye umri wa miaka 55,ama ukawa Mzee wa miaka 55 ukwa na akili, uwezo na kasi swa ya kuamua mambo yenye nguvu sawa na kijana wa miaka 18.Mwalimu mpaka kifo alikuwa ana umri wa miaka karibu sabini na tano lakini akili yake mpaka sasa na umri wangu na vijana wengine wa ujana wetu kwa mazingira yake hatujafikia alipokuwa yeye.

Wewe na mwenzio Zitto salamu zenu kuhusu umri sio tija sana kufanya watu wapoteze maana ya vifungu vya sheria Nchi yenye watu millioni 45,kwa ajili ya watu wawili BENZITO ALLIANCE aaaaaaaaah acheni masiahala ati msiavue c@%% hadharani watanzania kuwa hawajui na hawana ufahamu wowote kuhusu swala la umri hivyo UBENZITO uwe hojja ya msingi kuwa MADA YA KITAIFA KIMJADALA.Tunachotaka ni uwezo wa Rais mwenye Akili,Afya,Nguvu,Kasi,Mbunifu ,Mzalendo ,Mwenyeheshima, Mwadilifu, na yote kwa yote mwenye kuogopa Mungu.Haya ya umri sio tija sana marehemu mwanamuziki wa kimarekani ALIYAH alisema AGE ARE NOTHING BUT JUST A NUMBER.!!!!.

Na mwandishi wa hiyo mada ambayo nyie mmetoka kuisoma amerefer busra za mwalimu katika swala la number kuwa Urais klwa number sio jambo la msingi,namnukuu Bilabaye aliye toa thread yake inasema:
Wapo wanaotumia jina la Mwalimu kuthibitisha ‘uharamu' wa hoja zao. Kuna mtu alitolea mfano wa mwaka 1995, Mwalimu alipomwambia mmoja wa wagombea wa urais kupitia CCM, kuwa, ‘Wewe bado ni mdogo. Subiri kwanza ukue'. Lakini mtu huyo [tumwite ‘Bwana Mdogo'] alikuwa na miaka 45 wakati huo. Mwalimu mwenyewe hakuzuiliwa kugombea urais wa TAA na baadae TANU na kuongoza harakati za ukombozi licha ya udogo wake kiumri. Nijuavyo mimi, sina hakika kama Mwalimu angebadili mawazo yake, iwapo angekuwa hai, mwaka 2005 pale ‘Bwana Mdogo' alipojitokeza tena, akiwa na uzoefu mkubwa zaidi na umri wa miaka 55. Angalau karibu nizungumzaye nae ananiambia udogo na uchanga wa ‘Bwana Mdogo' huyo si wa umri, ni wa uwezo.

BENZITO muonapo red maana yake nasisitiza!!!!!!!!!!!!
 
Kamanda ZITTO unanishangaza sana, viongozi wenzako wapo ARUMERU wanapambana kuakikisha NASSARI anashinda, macho na maskio ya wanachadema na wapenda haki yanangalia ARUMERU kinachoendelea, wewe uku unaleta UPUUZI (samahani nimekosa neno nzuri la kusema) wa URAISI.

Mwlimu Nyerere alisema tumuogope mtu anayekimbilia IKULU, IKULU pana nini pale?

ZITTO unakumbuka 2010 Dr SLAA akuomba chama chake kimpitishe kugombea URAISI bali wanachadema wenyewe walimuomba DR asimame ktk mtanange?

Tujenge chama chetu tuachane na mambo ya URAISI
Alichokisema huyu Mzalendo ZITTO n cha msingi sana kuliko propaganda zinazoendeshwa na Chama chake kule Arumeru. Hawa MBOWE na SLAA tumeshawachoka ni haki kabisa wa-step down ili vijana wazalendo kama ZITTO wakijenge chama.
BIG UP ZITTO, tuko nyuma yako.
 
AKSANTE BEN KUMBE SIKU HIZI WEWE NA ZITO MNA [BENZITO -ALLIANCE ] YANI BEN AND ZITTO-ALLIANCE=COALITION.

Haya Ben ushauri wangu uliotaka kwa chama cha BENZITO-ALLIANCE AND COALITION, NILISHATOA HATA KABLA YA THREAD HII LEO SIKU KADHA HUKO NYUMA,MLISHA SOMA NDIO MKAAMUA KUJA NA TEAM YENU YA MAMR POPULARITY.

Mimi ni kijana kama ninyi,lakini uwa sisupporty ujana ovyo ovyo kwa kuwa nimejifunza kuwa unaweza ukawa kijana wa miaka kumi na nane akili zako zikawa sawa na Mzee asie na busara na hekima mwenye umri wa miaka 55,ama ukawa Mzee wa miaka 55 ukwa na akili, uwezo na kasi swa ya kuamua mambo yenye nguvu sawa na kijana wa miaka 18.Mwalimu mpaka kifo alikuwa ana umri wa miaka karibu sabini na tano lakini akili yake mpaka sasa na umri wangu na vijana wengine wa ujana wetu kwa mazingira yake hatujafikia alipokuwa yeye.

Wewe na mwenzio Zitto salamu zenu kuhusu umri sio tija sana kufanya watu wapoteze maana ya vifungu vya sheria Nchi yenye watu millioni 45,kwa ajili ya watu wawili BENZITO ALLIANCE aaaaaaaaah acheni masiahala ati msiavue c@%% hadharani watanzania kuwa hawajui na hawana ufahamu wowote kuhusu swala la umri hivyo UBENZITO uwe hojja ya msingi kuwa MADA YA KITAIFA KIMJADALA.Tunachotaka ni uwezo wa Rais mwenye Akili,Afya,Nguvu,Kasi,Mbunifu ,Mzalendo ,Mwenyeheshima, Mwadilifu, na yote kwa yote mwenye kuogopa Mungu.Haya ya umri sio tija sana marehemu mwanamuziki wa kimarekani ALIYAH alisema AGE ARE NOTHING BUT JUST A NUMBER.!!!!.

Na mwandishi wa hiyo mada ambayo nyie mmetoka kuisoma amerefer busra za mwalimu katika swala la number kuwa Urais klwa number sio jambo la msingi,namnukuu Bilabaye aliye toa thread yake inasema:Wapo wanaotumia jina la Mwalimu kuthibitisha ‘uharamu’ wa hoja zao. Kuna mtu alitolea mfano wa mwaka 1995, Mwalimu alipomwambia mmoja wa wagombea wa urais kupitia CCM, kuwa, ‘Wewe bado ni mdogo. Subiri kwanza ukue’. Lakini mtu huyo [tumwite ‘Bwana Mdogo’] alikuwa na miaka 45 wakati huo. Mwalimu mwenyewe hakuzuiliwa kugombea urais wa TAA na baadae TANU na kuongoza harakati za ukombozi licha ya udogo wake kiumri. Nijuavyo mimi, sina hakika kama Mwalimu angebadili mawazo yake, iwapo angekuwa hai, mwaka 2005 pale ‘Bwana Mdogo’ alipojitokeza tena, akiwa na uzoefu mkubwa zaidi na umri wa miaka 55. Angalau karibu nizungumzaye nae ananiambia udogo na uchanga wa ‘Bwana Mdogo’ huyo si wa umri, ni wa uwezo.

BENZITO muonapo red maana yake nasisitiza!!!!!!!!!!!![/QUOTE]

ZITTO,ZITTO, ZITTO anafaa sana, uwezo wake ni mkubwa kuliko hata MBOWE na SLAA. hana familia ndani ya chama, siyo mbinafsi kama MBOWE na SLAA. Hana biashara ndani ya chama kama ilivyo MBOWE na SLAA. Hana makundi ndani ya chama kama ilivyo SLAA na MBOWE.
"MBOWE NA SLAA NI LAZIMA WAONDOKE"
 
Kinachokusumbua wewe ni udini tu. Jaribu kuangalia habari imetoka wapi sio kukurupuka. Labda anaongelea urais 2025 Dr Slaa akishamaliza vipindi vyake, which kila mwana CDM atamuunga mkono. Lakini kwa sasa Zitto HAJAKWIVA kuwa rais na hata katiba haimruhusu
CHADEMA ni chama cha vijna , nadhani ZITTO atatufaa kwa mwaka 2015, SLAA amekwishajamani kwanza kashfa kibao mara kachukua mke watu, mara kajenga nyumba kunduchi kwa fedha za chama, mara mchumba wake anawaendesha viongozi ndani ya Chama. Kuna haja SLAA akae pembeni ili kukabiliana na matatizo na tuhuma zinazo mkabili. MBOWE vivyo hivyo akajitenge na biashara zake ili chama kiendeshwe na damu changa.
 
Chadema itakuwepo na itaendelea kuwepo hatakama viongozi wote wajuu wataondoka, walikuwepo waasisi wa chadema leo hii hawapo
na chama kinapiga mzigo kwa kwenda mbele. chama kina jengwa na wanachadema wote na si mtu mmoja moja kila mtu anamchango wake ndani ya chama.

PEOPLES POWER!!!!!!!!!!
 
Nadhani Zitto amesema vema ukisoma kwa makini katika andiko lake.

"Hata hivyo kazi hii hata kama naitaka ni lazima wenye nchi waamue kunipa kazi hii. Ni lazima kwanza Chama changu kiseme wewe ndio mwanachama unaestahili kuifanya kazi hii. Ni lazima Watanzania wengi waseme wewe ndio mwananchi mwenzetu unayeweza kuchukua jukumu hili. Kuitaka tu haitoshi. Ni lazima wananchi wakuamini na kukupa jukumu hili. Sasa kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au hata 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo".

Bila shaka ataendelea kuwa mtu wa kuheshimu maneno yake na in 2015 ataheshimu uamuzi wa watz kuwa Dr.Slaa ndo chaguo lao though katiba ikibadilishwa atakuwa na uwezo wa kugombea. Pamoja na ushawishi wake hajafikia level ya Dr.Slaa kwa umakini na uwajibikaji
Ni kweli SLAA ana ushawishi mkubwa kuliko ZITTO lakini siyo makini kama ZITTO. Ana ushawishi mkubwa sana kwa sababu watanzania tunapenda sana kusikia tuhuma za kugushi kama anavyofanya SLAA ila ukweli ni kwamba ZITTO ni mtu wa facts. Nadhani vijana tuachiwe tupendekeze anayefaa kugombea kupitia CHADEMA. tusiburuzwe kama ambavyo BAWACHA wanaburuzwa katika kuwapata wabunge wa viti maalum
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom