Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Mkuu Nguruvi3,

Waliokusoma na kukuelewa ni wengi tu, hizi porojo za wenzetu zitakuja fikia tamati muda sio mrefu, tuwe na Subira Kidogo, tutarudi to prove kwanini Tunasema Kwamba zitto wa "buzwagi" sio zitto wa "escrow", na kwanini zitto Hana Tena integrity ya kupambana na ufisadi.
Naona umegeuka ghafla kuwa msemaji wa watanzania na umeshika mikoba ya Sheikh Yahaya ya utabiri.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi ziwezi weka tumaini lolote juu ya Zitto.
Zitto si huyu huyu mwenye list ya watu wenye "vijisenti" uswis?
Au hizo za uswis zimekosa thamani?
Kama Zitto kweli anaogelea kwenye uzalendo na nchi kwanza,atuambie uzalendo wake kwenye hela za uswis umeenda wapi maana ana ushahidi.

Hii list aliotoa mbinguni au? Maana alivyoshindwa Zitto suala likaisha, hao wengine tunaowaamini kwa nini wasitusaidie hii orodha? Kama tunaambiwa kua kuna watu wameficha senti uswizi ZK ameshindwa kuwataja kwa nini wengine wasiwataje?
 
Zitto i see your intention, go on brother..you have my full support.
 
Big up zitto kabwe nimeanza kuku rudisha kwenye kichwa changu but icje ikawa changa la macho tena
 
Mungu akutie NGUVU ndugu Zitto usiogope kebehi na Maneno ya dharau..
 
Mkuu wangu gkileo.

Usiseme hivyo wachambuzi na wale Great Thinkers maghumashi wasikusikie.
 
Last edited by a moderator:
Hii list aliotoa mbinguni au? Maana alivyoshindwa Zitto suala likaisha, hao wengine tunaowaamini kwa nini wasitusaidie hii orodha? Kama tunaambiwa kua kuna watu wameficha senti uswizi ZK ameshindwa kuwataja kwa nini wengine wasiwataje?

mkuu

ndipo watu wetu walipofikia!! ni kama wengine vita hii hawahusiki

the real us

kuna mmoja alisema wazi sna vijisenti tu...tukamchekea na baadae katuandikia katiba!! mr. chenge

alitoa sababu ya wazi kabisa kuwa wako wenye hela clean na wako wenye hela chafu. mamlaka husika zifanye probing na kugundua nani msafi na nani mchafu

majina yao yanajulikana lakini si kila mwenye pesa uswis ni fisadi! angetaja na clean ones kesho si wanamfungulia mashtaka? kuna watu watu wana biashara huko nje....je wakiweka pesa huko si kosa!

pccb, bot, polisi n.k wana wajibu wa kufanya hiyo kazi
.
zitto ali initiate na the fact kuwa wanamkumbuka kwa hiyo ajends then he did his part
 
Integrity anayo nani?

Na anasubiri nini kulibeba?

We ----- nini, yaani swali GUMU hivi unawauliza GT wetu...?
nguruvi & Mchambuzi, eti na nyie mnakubali muulizwe swali gumu hivi, huyu jamaa hajui kuwa ni chuki yenu tu kwa zitto ndio inawafunika msiuone ukweli...?
 
Last edited by a moderator:
katika mada hii Mchambuzi na rafiki yake wana argue "emotionally" na siyo "rationally". na hii inachangiwa na chuki zao binafsi dhidi ya mheshimiwa Zitto.

ndiyo maana Wameshindwa kutueleza ni nani mwenye integrity wanayedhani anafaa kuongoza vita hii!

na kibaya zaidi hawatuelezi kwa nini hao wenye Integrity wamejikunyata kimyaa hawataki kusimama kuongoza vita hii!

Mchambuzi na mwenzie wanaona ni heri PESA ZA ESCROW ZIACHWE MIKONONI MWA MAFISADI KULIKO MHESHIMIWA ZITTO KUZIPIGANIA!!. huwezi kuamini "magreat thinkers" wameamua kujigaragaza mavumbini kiasi hiki!!.

Nguvu zao za kumshambulia Zitto wanazielekeza mahali pasiko, wao walitakiwa sasa hivi kuungana na wazalendo wengine kuwashambulia mafisadi wa Escrow, na siyo mheshimiwa.
 
Waberoya, Gamba la Nyoka, Granta, Ritz, Topical, na Wengine, kwa kweli mnaamua tu kujitoa ufahamu Katika suala husika, kwa maana ya hoja zangu juu ya Zitto & integrity. Awali nilifafanua maana ya Neno hili yani "integrity", pamoja na jinsi gani nimelitumia Katika ujenzi wa hoja husika.

Mwezi October 2012, Zitto alinukuliwa na vyombo vya habari akitamka maneno ambayo kwa kweli yaliongeza kasi ya wananchi wengi kuzidi kumuunga Mkono, Mimi Nikiwa ni mmoja wao Tena kwa maandishi hata humu jamiiforums. Hata Nguruvi3 nae amekiri Hili kwa upande wake.

Zitto alinukuliwa akisema hivi:

"Tutaweka wazi majina ya watanzania wenye akaunti uswisi kwa utaratibu na umakini. Nitataja Orodha hiyo bungeni na Kamwe sitotaja nje ya bunge."

Umma ukamsubiri kwa hamu sana, lakini hakutekeleza alichoahidi watanzania. Kufuatia Hali hiyo, Katika mahojiano mengine, Tena humu humu jamiiforums, AshaDii akamuuliza swali lifuatalo:

"Huku ukijua serikali haina nia ya kuwataja walioficha fedha mabenki ya nje huku wewe ukiwa na majina, unayashikilia ili nini na kwa faida ya Nani?"

Majibu ya zitto kwa swali hili yakawa Kama ifuatavyo:

"Kwa faida ya uchunguzi. Lazima serikali ijenge uwezo wake wa Kuchunguza na kuweka mambo sawa baada ya uchunguzi. Sasa ikiwa nini Kama mbunge nitatoa jina la watoroshaji pesa kwa sasa, Nani Atatoa majina hayo kesho? Mbunge mpya wa Kigoma kaskazini?"
Waberoya, Gamba la Nyoka, Granta, Ritz, Topical, na Wengine, tunapohoji integrity ya zitto Katika Sakata husika, kwanini mnatanguliza kwetu shutuma za chuki, Wivu, pamoja na matusi, kejeli na mipasho Wakati hoja zetu Zipo bayana na zinaendelea kuelea bila ya Kupata majibu?

Kwanini mnajitoa ufahamu na kunishutumu pale naposema "zitto wa buswagi sio zitto wa escrow"? Kwa mfano, ukiangalia majibu ya zitto kwa AshaDii hapo juu kuhusiana na swali kwanini hataji majina hadharani, hoja yake ya msingi ni Kwamba hataji kwa faida ya "uchunguzi". Ninaposema Kwamba zitto wa buzwagi sio zitto wa escrow ni Katika hoja hiyo hiyo.

Katika siasa za nchi yetu, Neno "uchunguzi" ni Neno ambalo huwa linatumiwa sana na Wanasiasa kuficha maovu na ufisadi. Uchunguzi, uchunguzi, uchunguzi. Hatukutegemea kiongozi Kama zitto aje kutumia neno hili Kama sababu kwanini aligairi kutaja majina ya mafisadi wa uswisi. Kama nilivyowahi jadili Huko nyuma, Dhana ya integrity inahusisha mambo Kama vile consistency Katika maamuzi Bila ya kujali unawaumiza akina Nani, ili mradi ni kwa maslahi ya taifa. Iwapo zitto wa escrow Angekuwa ni Yule Yule wa buzwagi, basi asingetumia Neno "uchunguzi" Kama kisingizio cha Kulaghai watanzania, kwani Katika Sakata la buzwagi, hakusubiri uchunguzi Kabla ya kutaja majina ya mafisadi Bali aliwataja wazi wazi, na matokeo yake ikawa ni manufaa kwa taifa. Zitto alisema hivi bungeni July 2007 bila ya kutafuna maneno:

"Kinachosikitisha ni kuwa mkataba huo umetiwa Saini kwa niaba ya serikali na waziri wa sasa wa madini na nishati, Tena utiaji Saini mkataba huo umefanyika London Uingereza na sio Tanzania."

Hatua hii ya zitto ilisaidia sana taifa kuokoa rasilimali za umma, lakini muhimu pia viongozi mafisadi wakatimuliwa. Muhimu pia ni Kwamba ilifikia hatua ya spika wa Wakati ule Samuel Sitta kumsimamisha zitto asiingie bungeni lakini Katika hili mbinu chafu ya Ccm kuficha maovu ilikuwa na mafanikio ya muda tu kwani zitto alikuwa upande wetu wananchi. Ndio maana hatua ya Sitta ikazidi kumpandisha zitto Katika medani za siasa kwani sisi Kama sehemu ya umma tulikuwa nyuma yake and we openly said tutafanya hivyo, "come what may".
Waberoya, Gamba la Nyoka, Granta, Ritz, Topical, bado kweli Hamuoni msingi wa hoja yangu?

Kweli hamuelewi sababu kwanini baadhi yetu hatuna Imani na zitto Tena Katika harakati za kuliondolea taifa na mafisadi?

Kweli mnataka tusahau yote haya na badala yake tusimame na kumpigia vigele gele zitto Katika suala la escrow?

Kwa faida ya nani?

Swali lenu Kwamba Nani basi Ndio aaminiwe badala ya zitto ni swali lenye nia ya kulenga kuondoa Watu Katika hoja ya msingi. Tulimwamini zitto huyo huyo kwani alionyesha uwezo mkubwa sana, integrity na uzalendo wa Hali ya juu. Kwa maana hii, zitto huyo huyo aendelee na harakati hizo, sisi hatuna shida, lakini tuna Haki ya Kuhoji masuala kadhaa Kama nilivyoainisha hapo juu na tunastahili kupewa majibu ya kuridhisha Kabla hatujaendelea kuwa nyuma yake. So far, hamjaja na majibu na badala yake ni matusi, mipasho, vijembe, na mengine mengi ambayo hayamsaidii zitto, na hayamsaidii mwananchi aliyemuunga Mkono zitto wa buzwagi.

Cc Mag3, Bongolander, MTAZAMO, Mtanganyika, Jasusi, JokaKuu, Dingswayo, Ben Saanane.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

Maelezo mengi ni dalili ya UNAFIKI, kupindisha maswali i.e. longolong za mtu ambaye si MKWELI, MUONGOetc...

Maswali tunayarudia
a. Nani huyu wenu mwenye integrity ???? unatakiwa kutaja jina

b. Anasubiri nini kulibeba...?? hata ikibidi mpeni baci nyinyi kama mna uchungu na nchi au ni wakweli hata kidogo kwenye moiyo yenu

conclusion:

a. Wewe na wenzako ni wanafiki, siyo wakweli vita yenu kuhusu ufisadi haiko focused ni personalized;

b. Zitto pambana achana na wanafiki ukifaulu tutashukuru, usipofaulu tutaamini na kusema umejitahidi..period..
 
Hapa yanajadiliwa majibu ya Mh Zitto kama alivyoyaweka kwa msingi wa ujibuji tuhuma zilizoelekezwa kwake,

Majibu yake yameacha baadhi tuhuma zikiwa hazina majibu.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

Maelezo mengi ni dalili ya UNAFIKI, kupindisha maswali i.e. longolong za mtu ambaye si MKWELI, MUONGOetc...

Maswali tunayarudia
a. Nani huyu wenu mwenye integrity ???? unatakiwa kutaja jina

b. Anasubiri nini kulibeba...?? hata ikibidi mpeni baci nyinyi kama mna uchungu na nchi au ni wakweli hata kidogo kwenye moiyo yenu

conclusion:

a. Wewe na wenzako ni wanafiki, siyo wakweli vita yenu kuhusu ufisadi haiko focused ni personalized;

b. Zitto pambana achana na wanafiki ukifaulu tutashukuru, usipofaulu tutaamini na kusema umejitahidi..period..

umeingia kwenda mjadala baadae sana, maswali yako nilishajibu kwa kina huko nyuma. the rest i consider as commentary...
 
Waberoya, Gamba la Nyoka, Granta, Ritz, Topical, na Wengine, kwa kweli mnaamua tu kujitoa ufahamu Katika suala husika, kwa maana ya hoja zangu juu ya Zitto & integrity. Awali nilifafanua maana ya Neno hili yani "integrity", pamoja na jinsi gani nimelitumia Katika ujenzi wa hoja husika.

Mwezi October 2012, Zitto alinukuliwa na vyombo vya habari akitamka maneno ambayo kwa kweli yaliongeza kasi ya wananchi wengi kuzidi kumuunga Mkono, Mimi Nikiwa ni mmoja wao Tena kwa maandishi hata humu jamiiforums. Hata Nguruvi3 nae amekiri Hili kwa upande wake.

Zitto alinukuliwa akisema hivi:

"Tutaweka wazi majina ya watanzania wenye akaunti uswisi kwa utaratibu na umakini. Nitataja Orodha hiyo bungeni na Kamwe sitotaja nje ya bunge."

Umma ukamsubiri kwa hamu sana, lakini hakutekeleza alichoahidi watanzania. Kufuatia Hali hiyo, Katika mahojiano mengine, Tena humu humu jamiiforums, AshaDii akamuuliza swali lifuatalo:

"Huku ukijua serikali haina nia ya kuwataja walioficha fedha mabenki ya nje huku wewe ukiwa na majina, unayashikilia ili nini na kwa faida ya Nani?"

Majibu ya zitto kwa swali hili yakawa Kama ifuatavyo:

"Kwa faida ya uchunguzi. Lazima serikali ijenge uwezo wake wa Kuchunguza na kuweka mambo sawa baada ya uchunguzi. Sasa ikiwa nini Kama mbunge nitatoa jina la watoroshaji pesa kwa sasa, Nani Atatoa majina hayo kesho? Mbunge mpya wa Kigoma kaskazini?"
Waberoya, Gamba la Nyoka, Granta, Ritz, Topical, na Wengine, tunapohoji integrity ya zitto Katika Sakata husika, kwanini mnatanguliza kwetu shutuma za chuki, Wivu, pamoja na matusi, kejeli na mipasho Wakati hoja zetu Zipo bayana na zinaendelea kuelea bila ya Kupata majibu?

Kwanini mnajitoa ufahamu na kunishutumu pale naposema "zitto wa buswagi sio zitto wa escrow"? Kwa mfano, ukiangalia majibu ya zitto kwa AshaDii hapo juu kuhusiana na swali kwanini hataji majina hadharani, hoja yake ya msingi ni Kwamba hataji kwa faida ya "uchunguzi". Ninaposema Kwamba zitto wa buzwagi sio zitto wa escrow ni Katika hoja hiyo hiyo.

Katika siasa za nchi yetu, Neno "uchunguzi" ni Neno ambalo huwa linatumiwa sana na Wanasiasa kuficha maovu na ufisadi. Uchunguzi, uchunguzi, uchunguzi. Hatukutegemea kiongozi Kama zitto aje kutumia neno hili Kama sababu kwanini aligairi kutaja majina ya mafisadi wa uswisi. Kama nilivyowahi jadili Huko nyuma, Dhana ya integrity inahusisha mambo Kama vile consistency Katika maamuzi Bila ya kujali unawaumiza akina Nani, ili mradi ni kwa maslahi ya taifa. Iwapo zitto wa escrow Angekuwa ni Yule Yule wa buzwagi, basi asingetumia Neno "uchunguzi" Kama kisingizio cha Kulaghai watanzania, kwani Katika Sakata la buzwagi, hakusubiri uchunguzi Kabla ya kutaja majina ya mafisadi Bali aliwataja wazi wazi, na matokeo yake ikawa ni manufaa kwa taifa. Zitto alisema hivi bungeni July 2007 bila ya kutafuna maneno:

"Kinachosikitisha ni kuwa mkataba huo umetiwa Saini kwa niaba ya serikali na waziri wa sasa wa madini na nishati, Tena utiaji Saini mkataba huo umefanyika London Uingereza na sio Tanzania."

Hatua hii ya zitto ilisaidia sana taifa kuokoa rasilimali za umma, lakini muhimu pia viongozi mafisadi wakatimuliwa. Muhimu pia ni Kwamba ilifikia hatua ya spika wa Wakati ule Samuel Sitta kumsimamisha zitto asiingie bungeni lakini Katika hili mbinu chafu ya Ccm kuficha maovu ilikuwa na mafanikio ya muda tu kwani zitto alikuwa upande wetu wananchi. Ndio maana hatua ya Sitta ikazidi kumpandisha zitto Katika medani za siasa kwani sisi Kama sehemu ya umma tulikuwa nyuma yake and we openly said tutafanya hivyo, "come what may".
Waberoya, Gamba la Nyoka, Granta, Ritz, Topical, bado kweli Hamuoni msingi wa hoja yangu?

Kweli hamuelewi sababu kwanini baadhi yetu hatuna Imani na zitto Tena Katika harakati za kuliondolea taifa na mafisadi?

Kweli mnataka tusahau yote haya na badala yake tusimame na kumpigia vigele gele zitto Katika suala la escrow?

Kwa faida ya nani?

Swali lenu Kwamba Nani basi Ndio aaminiwe badala ya zitto ni swali lenye nia ya kulenga kuondoa Watu Katika hoja ya msingi. Tulimwamini zitto huyo huyo kwani alionyesha uwezo mkubwa sana, integrity na uzalendo wa Hali ya juu. Kwa maana hii, zitto huyo huyo aendelee na harakati hizo, sisi hatuna shida, lakini tuna Haki ya Kuhoji masuala kadhaa Kama nilivyoainisha hapo juu na tunastahili kupewa majibu ya kuridhisha Kabla hatujaendelea kuwa nyuma yake. So far, hamjaja na majibu na badala yake ni matusi, mipasho, vijembe, na mengine mengi ambayo hayamsaidii zitto, na hayamsaidii mwananchi aliyemuunga Mkono zitto wa buzwagi.

Cc Mag3, Bongolander, MTAZAMO, Mtanganyika, Jasusi, JokaKuu, Dingswayo, Ben Saanane.

Sasa umeanza angalau kutambua umuhimu wa vita hii, na angalau umeanza kutambua kuwa Pesa za Umma ni za kupiganiwa kwa nguvu zote.

Nimefurahi sasa kwa Wewe kutambua kuwa Si busara kususia shamba na kumwachia Nguruwe.

Na pia Nimefurahi kwa wewe kukiri wazi kwamba ZITTO HUYU HUYU PAMOJA NA MAPUNGUFU YAKE AENDELEE NA HARAKATI HIZI.

Hata mimi ninaona kuwa , Pamoja na mapungufu ya kibinadamu ya Mheshimiwa Zitto, lakini ni kamanda muhimu wa vita hii, YATUPASA MIMI NA WEWE KUMUUNGA MKONO, KUMSHAURI NA IKIBIDI KUMSAIDIA KADRI TUNAVYOWEZA, KWA SABABU ANAWEZA AKAWA NA NIA NZURI LAKINI AKAKOSEA TACTICS.

INAPOTOKEA AKAKOSEA TACTIC AU APPROACH YA UPAMBANAJI, MIMI NA WEWE HATUTAKIWI KUANZA KUBEZA JUHUDI NA NIA YAKE. BALI INABIDI TUMPE MOYO NA KUMSAIDIA MAWAZO. HII VITA NI YETU SOTE, ILA KUNA WENGINE WAKO FRONT WANATUONGOZA NI LAZIMA TUSAIDIANE NA TUWASAIDIE, SI KUWABEZA, HAWA NI BINADAMU NA SI MALAIKA!.
 
Back
Top Bottom