Zitto: Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki"

Mkuu, baada ya kutujulisha kuwa Zitto hana integrity wala political maturity, sasa tupe way forward kwa mtazamo wako ni nani anafit kwenye hiyo nafasi aliyojikalisha Zitto ambaye hatoshi

Tuambie huyu na huyu na huyu wanafaa kwahiyo Zitto awaachie

Mkuu Granta, Swala hapa si nani zaidi ya Zitto anafaa kupigiaa mbinja swala la ufisadi wa IPTL-ESCROW, bali hoja iliyopo mezani ni "Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC 'Hatutetereki' kama alivyowasilisha mwenyewe ZZK. Hili tumelipokea vizuri lakini kabla hatujabeba mbeleko na kupiga vigelegele na nderemo na vifijo yakawepo maswali ya msingi ya kujibiwa na mleta mada, yaani Zitto ambaye mpaka muda huu kapotea mazima, wamebaki watu wanaoshabikia na kumsifia mtu ambaye hana moral authority yeyote na kumnyooshea mwingine kidole.

Kwa hiyo kabla hatujaenda mbali ajibu maswali yetu ili asije akatuacha solemba njiani
 
Last edited by a moderator:
Kafulila huyuhuyu SISIMIZI...? teh teh teh

Huyo huyo sisimizi, sasa kaiva. Kawa na nidhamu sana, ndani ya NCCR baada ya Mnafiki Zitto kutaka kumponza.

Kafulila alienda kumpigia magoti Mbati na kulia sana, asipokunywe uanachama hii ndio "political Maturity"

Zitto kutokana na kiburi, ubinafsi, jeuri, ufisadi akaona waliomtangulia hawana uwezo wowote, hawajui lolote.kasoma na anajua "ndumba"

Sisimizi tokea hapo akapendwa na watanzania hasa na mie binafsi.
Nilimuona kweli Kafulila kakua. Na kwa hili la Escrow ndio mshindi wetu.
 
But hizo media zipo upande wa umma pia!! Je Zzk si anapigania the same hoja au? kwangu Mimi hata Makinda,Makonda au Sitta wakisaidia kupambana hela zirudi nitasapoti!! Tuamue, tuungane hela zirudi au tutengane kisa sasa zetu na hela zisirudi kwenye maslahi ya Taifa tunatakiwa kwenda mbali zaidi ya uchama !!

am out

Mkuu Deo Corleone hakuna shida yeyote ya kuungana lakini lazima wawepo viongozi wenye nia safi ya kutuunganisha. Siyo political opportunists wenye hidden agenda ambao tukiwapa sapoti yetu watatugeuka na kutuacha njia panda, hao ni sumu na hatari sana
 
Last edited by a moderator:
But hizo media zipo upande wa umma pia!!

Je Zzk si anapigania the same hoja au?

kwangu Mimi hata Makinda,Makonda au Sitta wakisaidia kupambana hela zirudi nitasapoti!!

Tuamue, tuungane hela zirudi au tutengane kisa sasa zetu na hela zisirudi

kwenye maslahi ya Taifa tunatakiwa kwenda mbali zaidi ya uchama !!

am out

Mkuu, tutaungana lakini ni nani tunamtanguliza mbele?

Zitto alishafahamika ni mpiga dili tu. Tukimwachia atatupiga changa la macho.

Hafai kwakuwa tayari kaomba rushwa ili awapoze wenzie na bahati nzuri Kafulila kashamstukia.

Hatuwezi mkuu, kumtanguliza mtu yupo karibu na Nzowa wa TISS.

Kila ushahidi tulionao atauvujisha kwa sababu hana integrity tayari.

Tuwe makini na ZZK
 
Mkuu Granta, Swala hapa si nani zaidi ya Zitto anafaa kupigiaa mbinja swala la ufisadi wa IPTL-ESCROW, bali hoja iliyopo mezani ni "Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC 'Hatutetereki' kama alivyowasilisha mwenyewe ZZK. Hili tumelipokea vizuri lakini kabla hatujabeba mbeleko na kupiga vigelegele na nderemo na vifijo yakawepo maswali ya msingi ya kujibiwa na mleta mada, yaani Zitto ambaye mpaka muda huu kapotea mazima, wamebaki watu wanaoshabikia na kumsifia mtu ambaye hana moral authority yeyote na kumnyooshea mwingine kidole.

Kwa hiyo kabla hatujaenda mbali ajibu maswali yetu ili asije akatuacha solemba njiani

Mkuu, nikuulize tu swali rahisi, kwann Zitto anarushiwa tuhuma nyingi wakati HUU ambao kamati yake ( PAC) inalifuatilia suala hili...

Huoni tuhuma hizi(ziwe kweli au la) zinafnaywa makusudi ili kuwakatisha tamaa kina Zitto na kamati yake...?

Imekuwa ni kawaida linapotokea jambo zito linapotokea basi wanaoisukuma hiyo AGENDA hutungiwa tuhuma nyingi sana, utasikia mbona huyu Katembea na Mke wa mtu, sijui ana kimada, n.k

Huoni tukianza kujadili tuhuma ni kuingia kwenye 18 za MAFISADI...?
 
Last edited by a moderator:
Huyo huyo sisimizi, sasa kaiva. Kawa na nidhamu sana, ndani ya NCCR baada ya Mnafiki Zitto kutaka kumponza.

Kafulila alienda kumpigia magoti Mbati na kulia sana, asipokunywe uanachama hii ndio "political Maturity"

Zitto kutokana na kiburi, ubinafsi, jeuri, ufisadi akaona waliomtangulia hawana uwezo wowote, hawajui lolote.kasoma na anajua "ndumba"

Sisimizi tokea hapo akapendwa na watanzania hasa na mie binafsi.
Nilimuona kweli Kafulila kakua. Na kwa hili la Escrow ndio mshindi wetu.

Teh teh teh ni lini Kafulila alikiri kufanya kosa hadi akafukuzwa CHADEMA...!

Mngejua tu mnavyoonesha chuki za waziwazi ndio mnampaisha jamaa
 
Huyo huyo sisimizi, sasa kaiva. Kawa na nidhamu sana, ndani ya NCCR baada ya Mnafiki Zitto kutaka kumponza.

Kafulila alienda kumpigia magoti Mbati na kulia sana, asipokunywe uanachama hii ndio "political Maturity"

Zitto kutokana na kiburi, ubinafsi, jeuri, ufisadi akaona waliomtangulia hawana uwezo wowote, hawajui lolote.kasoma na anajua "ndumba"

Sisimizi tokea hapo akapendwa na watanzania hasa na mie binafsi.
Nilimuona kweli Kafulila kakua. Na kwa hili la Escrow ndio mshindi wetu.

Asante sana POMPO, Kiongozi mzuri ni yule mnyenyekevu ambaye hata akikosea hujirudi na kuomba msamaha. Huyo atasamehewa na kuheshimiwa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Granta, Swala hapa si nani zaidi ya Zitto anafaa kupigiaa mbinja swala la ufisadi wa IPTL-ESCROW, bali hoja iliyopo mezani ni "Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC 'Hatutetereki' kama alivyowasilisha mwenyewe ZZK. Hili tumelipokea vizuri lakini kabla hatujabeba mbeleko na kupiga vigelegele na nderemo na vifijo yakawepo maswali ya msingi ya kujibiwa na mleta mada, yaani Zitto ambaye mpaka muda huu kapotea mazima, wamebaki watu wanaoshabikia na kumsifia mtu ambaye hana moral authority yeyote na kumnyooshea mwingine kidole.

Kwa hiyo kabla hatujaenda mbali ajibu maswali yetu ili asije akatuacha solemba njiani

Mkuu lane Mchambuzi

Hiyo PAC anayosema "hatutetereki"
Ina wajumbe 18 na zaidi ya 80% ni wa ccm.

Je ccm walishawahi kuwajibishana wao kwa wao? Je Zitto ataiweza 80%

Mambo mangapi hupozwa?

Zitto anataka tumuamini na PAC yake ya CCM ambayo wamesha fail hata swala la mikataba TPDC.

Tuwe makini wasitupige cahanga la macho hawa PAC na Zitto wake.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Deo Corleone hakuna shida yeyote ya kuungana lakini lazima wawepo viongozi wenye nia safi ya kutuunganisha. Siyo political opportunists wenye hidden agenda ambao tukiwapa sapoti yetu watatugeuka na kutuacha njia panda, hao ni sumu na hatari sana

Tutajie viongozi wasafi tuwaunge mkono kwenye hili saga tuachane na Zitto
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, nikuulize tu swali rahisi, kwann Zitto anarushiwa tuhuma nyingi wakati HUU ambao kamati yake ( PAC) inalifuatilia suala hili...

Huoni tuhuma hizi(ziwe kweli au la) zinafnaywa makusudi ili kuwakatisha tamaa kina Zitto na kamati yake...?

Imekuwa ni kawaida linapotokea jambo zito linapotokea basi wanaoisukuma hiyo AGENDA hutungiwa tuhuma nyingi sana, utasikia mbona huyu Katembea na Mke wa mtu, sijui ana kimada, n.k

Huoni tukianza kujadili tuhuma ni kuingia kwenye 18 za MAFISADI...?

Mkuu Granta
Ni kwa nini Zitto tu wakati PAC ina wajumbe zaidi ya 18?

Tafakari, Chukua hatua...
 
Mkuu, usifiki wanaotulazimisha kutuhamisha kwenye mada ya msingi hawana akili...!

Ni lazima wamchague mtu ambaye ni popular kwenye jamii kama Zitto
 
Last edited by a moderator:
Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea kumkumbatia. Watanzania sio mabwege!

Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC

Dodoma, 9 Novemba 2014

Kweli watanzania sio mabwege lakini vile vile watanzania sio wasahaulifu. Katibu mkuu wa ACT, Samson Mwigamba, akihojiwa na redio ya sauti huru mwezi June, 2014, Alitamka haya:

"Lengo kubwa la chama cha ACT ni kuunganisha wananchi na kuwaeleza ubovu wa chama kikuu cha upinzani nchini, chadema."

"Imekuwa Vigumu kueleza ubovu wa chadema wananchi wakaelewa kwa sababu imetokea wananchi wanaiamini ukawa na hawataki useme chochote kuhusu mshirika wa umoja huo."

"Naamini Kwamba ukawa utasambaratika Kabla ya 2015 na hapo ndipo wananchi wataelewa kuhusu vita ya ACT na Chadema."

Lugha yako na ya mwigamba zinafanana. Kwa mfano, Katika hoja za mwigamba, chama kikuu cha upinzani kwa ACT ni chadema, sio CCM.

Isitoshe, umenukuliwa ukiita umoja wa ukawa Kwamba ni wasaka tonge, licha ya Kwamba hakuna Taratibu au kanuni waliyovunja, lakini umoja wako, mwigamba na kitila mkumbo kutafuta madaraka ndani ya chadema nje ya utaratibu, kwenu mliona Kwamba ni Haki ya kidemokrasia. This is Double standards in action and typical "political immaturity" that I discussed earlier.
 
Mkuu, mambo ya integrity umeyaleta wewe na kumuhusisha Zitto hana hiyo integrity, sasa mdau kakuuliza ni nani basi ambaye ana hizo integrity na political maturity ili tumuunge mkono na kuachana na Zitto, sisi lengo letu sio Zitto ama Kafulila , lengo letu ni pesa zetu zirudi, only that

Pesa zetu za uswisi zimerudi?
 
Mkuu, nikuulize tu swali rahisi, kwann Zitto anarushiwa tuhuma nyingi wakati HUU ambao kamati yake ( PAC) inalifuatilia suala hili...

Hapa hebu nisaidie kuelewa kwani ni 'tuhuma zipi' nyingi anazotumiwa zitto? zipi hizo maana kadri ninayoona watu wanahoji integgrity na political maturity wa zitto wenu kusimamia jambo la kitaifa kama la ESCROW. Na hii inatokana na hofu ya watu kwamba isije kuwa jamaa anatafutana nitoke vp kisiasa afu akatuacha solemba njiani kama alivyofanya yale ya Mabilioni ya Uswizi

Huoni tuhuma hizi(ziwe kweli au la) zinafnaywa makusudi ili kuwakatisha tamaa kina Zitto na kamati yake...?
Hizi ni hisia zako tu ambazo haziko justified, after all akatishwa tamaa ili iweje? Kama ana integity ya kufanya afanyalo let him go ahead

Imekuwa ni kawaida linapotokea jambo zito linapotokea basi wanaoisukuma hiyo AGENDA hutungiwa tuhuma nyingi sana, utasikia mbona huyu Katembea na Mke wa mtu, sijui ana kimada, n.k

Huku ni kujibu hoja kwa viroja mkuu, hii makitu umeitoa wapi? una ushahidi wowote ukiacha maswala ya petty politics?

Huoni tukianza kujadili tuhuma ni kuingia kwenye 18 za MAFISADI...?
Wasiwasi huu hauna msingi wowote mkuu

Again mkuu tujadili haya maswali siyo kwa ushabiki bali kwa hard facts
 
Mkuu, yaani kwa ujasiri kabisa unauliza ni tuhuma zipi anazoshutumiwa Zitto...? Nikusaidie tu kazisome kwenye post #1

Mkuu, unashindwa kabisa kuelewa wakati mtu(Zitto) ameshika mtutu(hoja) kwa ajili ya kumshambulia Adui(maCCM,IPTL) wewe uko bize kumchokonoa na singe kwa nyuma huoni unampotezea target...?

Mkuu, ni mara ngapi tumesikia pale Dr Slaa akianza kulisimamia jambo utawasikia wabaya wake kuwa "anatoka na mke wa mtu" "Padre Mzinifu" "katelekeza familia" "kibabu na mchumba", Mara ngapi tumepata kuona pale CDM ikiwabana Magamba utasikia "Chama cha mlengo wa kikristo" "Chama cha kikabila" " Chama cha kaskazini", mara ngapi personally wamesema Mbowe "anatoka na mbunge wa viti maalum" kama jitihada zao za kuzima hoja...!

Tumetoa tahadhari, kama mnasema Zitto hafai kuongoza haya mapambano, tutajieni Mtu mwingine tumuunge mkono na tuachane na Zitto otherwise mnaungana na MAFISADI ktk kuzuia hili lisifanikiwe
 
Msitume PRIVATE MESSAGES kuomba tufunike kombe mwanaharamu apite, ingieni jamvini tujadili hoja.

Teh teh teh, kwann usiwaambie huko huko PM kuwa waje jamvini...tutaamini vipi wamekufuata PM...

Tusaidie kutuonesha mmoja ambaye tutamfata na kumuacha Zitto kama kiongozi ambaye ana feature ulizosema za integrity na political maturity
 
Awali swali lako liliulizwa na Gamba la Nyoka, huku wewe ukishabikia Kwamba nitamtaja kafulila. Mimi nikajenga hoja ndogo na Rahisi sana kutokana na Ile post ya gamba la Nyoka nikilenga kujua kwanza tunasimamia wapi juu ya suala la integrity, na Nikasema Kwamba nikipata position yenu, nitajua mnasimamia wapi na kwa hoja gani, na hivyo ndivyo mjadala utakuwa na mtiririko mzuri. Lakini sio wewe Wala gamba la Nyoka mmenipa Maelezo. Mnachojaribu kufanya sasa ni kuhamishia goli kwingine.

Naomba Nikuhakikishie tu Kwamba tutalifuata goli hata liende wapi.

Vingine mnitukane na kutoa mipasho Kama Waberoya kwa hoja na maneno mepesi mepesi Kwamba "nachemka" hivyo sistahili Kujadiliana na Watu wa viwango vyenu kisha mtoweke kwenye hoja zangu Kama waberoya. Hilo nitaliheshimu. Not otherwise.
 
Mkuu, unasema Zitto hana integrity

Wengine tunaona anayo integrity

Unasema Zitto hajawa politically mature

Wengine tunaona kama ni issue ya maturity kwenye siasa basi Zitto kawazidi mbali wa na Sasa wengi nchi hii na pengine anaongoza...!

Sasa, kwa kuwa we unaona Zitto hana hizo feature, kindly tuoneshe mtu mwingine ambaye ana hizo sifa ili tuache kumfuata Zitto, only that
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, yaani kwa ujasiri kabisa unauliza ni tuhuma zipi anazoshutumiwa Zitto...? Nikusaidie tu kazisome kwenye post [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=1]#1 [/URL]

Mkuu, unashindwa kabisa kuelewa wakati mtu(Zitto) ameshika mtutu(hoja) kwa ajili ya kumshambulia Adui(maCCM,IPTL) wewe uko bize kumchokonoa na singe kwa nyuma huoni unampotezea target...?

Mkuu, ni mara ngapi tumesikia pale Dr Slaa akianza kulisimamia jambo utawasikia wabaya wake kuwa "anatoka na mke wa mtu" "Padre Mzinifu" "katelekeza familia" "kibabu na mchumba", Mara ngapi tumepata kuona pale CDM ikiwabana Magamba utasikia "Chama cha mlengo wa kikristo" "Chama cha kikabila" " Chama cha kaskazini", mara ngapi personally wamesema Mbowe "anatoka na mbunge wa viti maalum" kama jitihada zao za kuzima hoja...!

Tumetoa tahadhari, kama mnasema Zitto hafai kuongoza haya mapambano, tutajieni Mtu mwingine tumuunge mkono na tuachane na Zitto otherwise mnaungana na MAFISADI ktk kuzuia hili lisifanikiwe

Mkuu @ tutofautishe propaganda za kisiasa na ukweli

Ni kweli Dr Slaa ameshawahi kuwa attacked on a personal level mara nyingi tu akija na hoja nzito za taifa. Lakini mwenye akili angavu atajua tu kwamba hizi ni politics wala hayana madhara sana

Kwa Zitto sisi hapa hatufanyi politics mkuu. Hoja #1 nimeisoma na kuielewa lakini maswali mengi yalinijia na yanayohitaji majibu. Zitto atupatie hayo majibu la vp hattutakosea kuwa na doubt juu ya dhamira yake ya ndani ukizingatia yeye mwenyewe ndie ajuaye

Mkuu si vizuri hata kidogo kuwa shabiki wa siasa za matukio, through IPTL-ESCROW zitto anataka kupata kiki, hilo nalo si jambo baya lakini tatizo hana integrity na kusimamia anayoyahubiri. Yeye mwenyewe kapiga dili pale, kachota vya kutosha afu unaniambia nimpe sapoti, unataka aje kuniacha njiani solemba

somebody said - fool me once, shame on you BUT fool me twice, shame on me'. Kwa kifupi ZZK hatoshi kwenye sakata la ESCROW, he is equally guilt kama alivyo akija Seth
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom