Maono yangu kwenye hili naona yafuatayo.
1) Zitto ni mwanasiasa mwenye utata sana, ukifuatilia historia yake ya kisiasa utaligundua ninaloliongelea, wakati wa kipindi cha Kikwete alikuwa mtu ambaye huwezi amini ni mpinzani kwa kuwa mienendo yake na watawala hususani raisi Kikwete ilitia Shaka, alipochaguliwa magufuli wakati anaenda kuzindua bunge wabunge wa upinzani walitoka nje ila zito alibaki na akamwagiwa sifa na Magufuli na ukiangalia clip utaona zitto alionyesha tabasamu, hakugundua zilikuwa sifa za muda mfupi na mheshimiwa baada ya hapo hatakuwa tena na mawasiliano na zitto kama zitto alivyo tegemea,
Zitto alikuwa na mawili moyoni mwake moja awe puppet wa serekali akubali kudhalilika na iliposhindikana akaamua kujiunga na wakosoaji na wajeruhiwa wa Magu kumyumbisha, zitto hajawahi na hatowahi kufanya siasa za kiunaharakati kwa ajili ya Taifa bali siasa zake zimekuwa aidha za kutafuta umaarufu wake binafsi au kulinda tumbo lake na ushahidi upo kwa waliokuwa wanamfuata nyuma kama kina machari and co.
2)Kuhusu Gwajima kuna mambo kama mawili, kwanza Gwajima kuonyesha chuki ya wazi kwenye Clip yake kwa kutaja neno YULE akimlenga raisi mstaafu na ukimsikiliza vizuri ni kwamba ana chuki na YULE, Chuki hii iko wazi kwa kuwa ni mjeruhiwa wa matendo ya YULE na kutokana na hilo anatafuta njia ya kumaliza machungu kwa kuside na mtu anayeona anaweza kumsaidia ambaye ni Magufuli,
Pili kumbuka hatujui Gwajima ameyumba kiuchumi na kiwafuasi kiasi gani kwani wafuasi wengi kanisani ndio kipato kikubwa na anaamua kucheza na fursa na hii ni pale Raisi alipoenda kusali kwa Mzee wa upako na yeye akaona kuside na huyu mtu huenda kutanifanya nitengeneze fursa kwani raisi kwenda kusali kanisani kwake ni kumfanya atengeneze wafuasi kupitia mlango huo. Haya ni mawazo yangu najua wafuasi wa zitto watakuja na matusi na pia wanaoamini dini watakuja na mapovu mdomoni kama wametafuna sabuni ila muda ni mwalimu mzuri