Zitto na Kikwete, Gwajima na Magufuli!

Zitto na Kikwete, Gwajima na Magufuli!

Zitto ni kama Mengi tu, huwezi shindana nao ukashinda.
Huu mtifuano, kifo kitaamua.
RIP Mudhihir Mudhihir na yule Mama wa Moshi.
Mkuu kumbuka hapa anapambana na raisi na hakuna mtu mmoja asiye na ufuasi wa umma aliewahi kuingusha dola mkuu! Mifano ni Osama na dola la kimarekani, Kodokovirsky na dola la Urusi na kumbuka hao walikuwa na hela na nyenzo acha zitto anaetafuta huruma ya wafuasi wake laki sita.
 
huyo kiongozi wa dini sio wakuaminika sana na huyo mwanasiasa naye sio wakuaminika kwahiyo utaona maslahi binafsi ndiyo yanatafutwa hapo
Mbaya zaidi, siasa ndiyo zinaamua au kuyakinisha maisha yetu hapa duniani na pia dini inayakinisha maisha yetu baada ya kifo.
 
Nyie CCM kuna kitu mnakitengeneza & kukitafuta kupitia PROPAGANDA zenu hizi.

Endeleeni; Sisi tupo!
 
Historia inaonyesha yeyote atakaepambana na Zitto atadondoka kisiasa na kupotea kabisa.Mpaka sasa mkulu anajitaidi kujinasua kwenye tope ila sidhani kama ataweza kujinasua.Ngoja niweke akiba ya maneno.Mda utasema
 
Kuna nguvu za kisiasa (political force) zinazopambana kwa kusigana kwa sasa nchini huku cheche zake za kisiasa zikiwapata baadhi ya wananchi wasiofahamu chanzo chake.

Ninaamini kuna wananchi wanashangaa na kujiuliza sababu ya uwepo wa hizi nguvu zinazosigana na matokeo yake.

Mwanasiasa Zitto Kabwe anamwamuru Kiongozi Mkuu wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete amdhibiti Rais Magufuli na anaenda mbali na kudai Rais Magufuli asifikiri Kikwete ni mjinga kwasababu aliruhusu uhuru wa kujieleza katika utawala wake pamoja na kwamba wapinzani walimwita ni Rais dhaifu.

Pastor Josephat Gwajima anamwamuru Rais Magufuli asikubali kudhibitiwa na Kiongozi Mkuu wa CCM, Jakaya Kikwete na kama ataendelea kumdhibiti basi achague mambo mawili ambayo ni kuhama/kuachana na CCM au kuanzisha mchakato wa kuondoa/kubadilisha Ibara ya 46(1-3) inayohusu Kinga dhidi ya madai na mashataka kwa Rais wa Tanzania.

Ukiangalia kwa undani huu msuguano utagundua Zitto na Gwajima ni mawakala wa kisiasa (political agent) ambao wanawakilisha kundi la wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya nchi.

Kwa sasa siasa za Tanzania ziko kwenye mpito na katika mpito huo kuna political consolidation ambayo hatimaye itajenga mwelekeo wa nchi katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania 1977 mwenye rungu la mpito ni Rais wa Tanzania.

Wakati Zitto akiwakilisha kundi linaloathirika kwa sasa katika political consolidation. Gwajima anawakilisha kundi lililoathirika na political consolidation wakati wa utawala wa Rais Kikwete.

Kundi ambalo halijaathirika limekaa pembeni linaangalia mwelekeo wa political consolidation na hatima yake.

Katika utawala la Rais Kikwete, Gwajima na kundi lake waliathirika sana nakwa ujumla ninaweza kusema walishindwa vita mpaka wakasambaratika pamoja na kutumia nguvu za pesa na imani za kidini katika mapambano.

Gwajima wa sasa anafahamu madhara ya kupambana na mtu mwenye rungu na kwa maana hiyo kwa sasa inabidi awahi kiti cha mbele kwenye utawala wa Rais Magufuli.

Gwajima bado ana hasira za kushindwa vita na kwa sasa anajaribu kumshawishi Rais Magufuli amsaidie kwa kutumia rungu lake kwa wabaya wake.

Kwa sasa ameibuka Zitto ambaye pia ni wakala mwenye ‘nguvu za kisiasa’. Sifahamu kwa kiwango gani hizi nguvu zake zinaweza kupambana na rungu la Rais Magufuli kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Hata hivyo historia inatuambia ukipambana na Rais wa Tanzania huwezi kushinda vita. Mpito wa kisiasa wa sasa unamwathiri sana Zitto katika nyanja ya kifedha na kisiasa.

Zitto anajinadhibisha ni mpigania demokrasia lakini pia hatuwezi kufahamu walioko nyuma yake wana nguvu ya kifedha kiasi gani na katika nguvu hizo, wataathiri utawala wa Rais Magufuli kwa kiwango gani huku wakimnufaisha Zitto kifedha na kisiasa.

Je, hii vita aliyoanza Zitto kupigana atashinda?

Je, Gwajima atapata kile anachokitafuta kutoka kwa Rais Magufuli?

Muda utatoa majibu kwa sababu muda ni mwalimu mzuri!
zitto ni mwanasiasa hatari anajidai na ana dharau. kuna wakati alijidai nani asiyemjua tanzania na kusema mwanasiasa fulani sio size yake. mtu anahangaika kutaka kua rais wa nchi hii siku moja. sio kosa ila njia anayotumia haina tija. watanzania wameshajua namna ya kupata kiongozi. sio mtu anayehangaika kutufata uongozi ila mtu anayejitokeza kama kiongozi bora. wameanza na jpm na atakayefuata atakua kiongozi bora sio msaka urais.
 
Zitto ana hasira sana na Magufuli hasa baada ya swahiba wake Dr Ramadhan Dau kutumbuliwa kwa kuahidiwa kupewa Ubalozi ambapo mpaka sasa anakalia benchi. Hatafanikiwa vita hii kwa sababu anapambana bila ya ridhaa ya Mungu
Nadhani hizi ni hisia tu!
 
Rais haongozi kwa kuota. Kuna mawili makubwa moja ni aliyoshuhudia wakatia akiwa waziri. pili ni taarifa anazopata kutoka sehemu na hasa watoa taaarifa na mapitio ya nyaraka.

Kwa hiyo hao wanaosemwa ni tone tu katika kuinfluence utawala wa rais.
Labda kama na wao ni sehemu ya watoa taarifa au kama rais ni mtu wa kulewa sifa au wa kukasirika haraka.

Aliyoshuhudia rais alipokuwa waziri alianza nayo vizuri na yamempayusha .

Taarifa alizopata zina mawili moja ama zinaweza kumdhoofisa au kumpayusha kutegemeana na lengo la watoa taarifa na uwezo binafsi wa kuzitasiri na kuchukua hatua.
 
Zitto ana hasira sana na Magufuli hasa baada ya swahiba wake Dr Ramadhan Dau kutumbuliwa kwa kuahidiwa kupewa Ubalozi ambapo mpaka sasa anakalia benchi. Hatafanikiwa vita hii kwa sababu anapambana bila ya ridhaa ya Mungu
Haha wewe, nilichelea kidogo kutana Dau na chimbo la akina zitto la hela za wavuja jasho.
 
Zitto Na Gwajima wote wanafiki tu.

Gwajima anawasilisha hasira za kundi la Lowasa walivyokatwa Dodoma.

Zitto anawasilisha hisia za kundi la utawala wa Kikwete liloumizwa Na utawala wa Magufuli, hasa wale wanaosambaza kampeni za kumnyima Magufuli uenyekiti.

Hivyo kati yao sioni Mwenye dhamira ya dhati kwa Taifa.

Magufuli awapotezee tu, wote mamluki hao.

Mkuu ahsante kwa hoja yako makini mno..
 
sidhani kama gwajima yuko na jpm kama ambavyo zzk yuko na jk! zzk yuko kimkakati zaidi, lakini gwajima ni proker tu if u read between lines.
 
Hivi ukiulizwa unafiki wa Zitto kwenye mambo anayoyalalamikia unaweza sema ni uko wapi?

Hivi unapata wapi upuuzi wa kusema Zitto anatumwa na wafanyabiashara na waadhirika wa magufuli?

Ni UPUUZI mkubwa sana huu.

Zitto anasimama kama kiongozi wa chama chake ...kama kutumwa anatumwa na chama chake.

ACHENI CHUKI KWA ZITTO ZISIZO NA MSINGI.
 
Japo gwajima hayupo karibu na magufuli
Amemsaidia magufuli kupata picha kamili linaloendelea chini ya kapeti

Maana magufuli fitina za ndani ya ccm haziwez, ye amekaa kufikiria namna ya kuitokomeza Ukawa

Subir achezweshe gwaride na kikwete kupitia kwa Zito

JK ni mtu atari sana kwenye figisu figisu yule mzee muone vile
 
Kuna nguvu za kisiasa (political force) zinazopambana kwa kusigana kwa sasa nchini huku cheche zake za kisiasa zikiwapata baadhi ya wananchi wasiofahamu chanzo chake.

Ninaamini kuna wananchi wanashangaa na kujiuliza sababu ya uwepo wa hizi nguvu zinazosigana na matokeo yake.

Mwanasiasa Zitto Kabwe anamwamuru Kiongozi Mkuu wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete amdhibiti Rais Magufuli na anaenda mbali na kudai Rais Magufuli asifikiri Kikwete ni mjinga kwasababu aliruhusu uhuru wa kujieleza katika utawala wake pamoja na kwamba wapinzani walimwita ni Rais dhaifu.

Pastor Josephat Gwajima anamwamuru Rais Magufuli asikubali kudhibitiwa na Kiongozi Mkuu wa CCM, Jakaya Kikwete na kama ataendelea kumdhibiti basi achague mambo mawili ambayo ni kuhama/kuachana na CCM au kuanzisha mchakato wa kuondoa/kubadilisha Ibara ya 46(1-3) inayohusu Kinga dhidi ya madai na mashataka kwa Rais wa Tanzania.

Ukiangalia kwa undani huu msuguano utagundua Zitto na Gwajima ni mawakala wa kisiasa (political agent) ambao wanawakilisha kundi la wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya nchi.

Kwa sasa siasa za Tanzania ziko kwenye mpito na katika mpito huo kuna political consolidation ambayo hatimaye itajenga mwelekeo wa nchi katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania 1977 mwenye rungu la mpito ni Rais wa Tanzania.

Wakati Zitto akiwakilisha kundi linaloathirika kwa sasa katika political consolidation. Gwajima anawakilisha kundi lililoathirika na political consolidation wakati wa utawala wa Rais Kikwete.

Kundi ambalo halijaathirika limekaa pembeni linaangalia mwelekeo wa political consolidation na hatima yake.

Katika utawala la Rais Kikwete, Gwajima na kundi lake waliathirika sana nakwa ujumla ninaweza kusema walishindwa vita mpaka wakasambaratika pamoja na kutumia nguvu za pesa na imani za kidini katika mapambano.

Gwajima wa sasa anafahamu madhara ya kupambana na mtu mwenye rungu na kwa maana hiyo kwa sasa inabidi awahi kiti cha mbele kwenye utawala wa Rais Magufuli.

Gwajima bado ana hasira za kushindwa vita na kwa sasa anajaribu kumshawishi Rais Magufuli amsaidie kwa kutumia rungu lake kwa wabaya wake.

Kwa sasa ameibuka Zitto ambaye pia ni wakala mwenye ‘nguvu za kisiasa’. Sifahamu kwa kiwango gani hizi nguvu zake zinaweza kupambana na rungu la Rais Magufuli kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Hata hivyo historia inatuambia ukipambana na Rais wa Tanzania huwezi kushinda vita. Mpito wa kisiasa wa sasa unamwathiri sana Zitto katika nyanja ya kifedha na kisiasa.

Zitto anajinadhibisha ni mpigania demokrasia lakini pia hatuwezi kufahamu walioko nyuma yake wana nguvu ya kifedha kiasi gani na katika nguvu hizo, wataathiri utawala wa Rais Magufuli kwa kiwango gani huku wakimnufaisha Zitto kifedha na kisiasa.

Je, hii vita aliyoanza Zitto kupigana atashinda?

Je, Gwajima atapata kile anachokitafuta kutoka kwa Rais Magufuli?

Muda utatoa majibu kwa sababu muda ni mwalimu mzuri!

Mkuu umetisha ngoja nikugongee like kwanza...iwe anakosea ama yupo sahihi Maghufuli ana akili sana zaidi ya watu wanavyomchukulia...!!! over.. time will tell
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom