Zitto kahudumia kama Mbunge katika Utawala wa Kikwete, Mbunge gani ambaye alikuwa hot na aliplay party kubwa kuidhibu Serikali unamlinganisha na Zitto?, hivi Zitto alikuwa na urafiki sana kuliko Mbatia na Kikwete?.
Suala la siasa za Kiunaharakati, labda hujui kwamba ukiitaja chadema na siasa zao za kiuhanaharakati waasisi wake ni pamoja na Zitto na alianza siasa hizo tokea akiwa chuo ndiyo maana hata Mbowe alimuona tusiwe tunarishwa vyakula bila kuvipima kwa mapana, Mbowe alimchukua Zitto kwa sababu aliona kitu ambacho leo mnakigeuza na kuonekana si kweli.
Leo hii sasa chadema wana Lowasa ambaye hataki siasa za kiuharakati, nani anamsema?, nani anaongea?, tatizo la Zitto na Chadema ni Mbowe na hii ndiyo iliyomfanya Mbowe ahakikishe anaua nguvu ya Zitto chadema tokea 2010 maana uchaguzi ulikuwa unakaribia alafu ilipofika 2012 akafanikiwa hadi kubadili katiba maana aliona anaweza kutokea mtu mwingine badala ya Zitto kwani mtangulizi wake alikuwa Marehemu Chacha Wangwe kuhoji Kiti cha Mwenyekiti wa Chama, alipofanikiwa na sasa kaona Zitto siyo threat tena kwake na hakuna atakayetokea ameamu kusema amemsamehe Zitto.
Mtoa post anasema Zitto anamuomba Kikwete amdhibiti Magufuli asigombee awamu ijayo?, kwani unataka kusema Zitto ni mjinga hajui kwamba Uenyekiti wa Kikwete unaisha?, kwamba Magufuli ndo atakuwa Mwenyekiti?, au unataka kutuaminisha kwamba Kikwete ana nguvu ya kuamua nani aje kuwa rais ajaye baada ya Magufuli?, hoja ya Zitto ni kwamba Magufuli adhibitiwe kuhusu suala la kuminywa Demokrasia na mara zote Zitto amekuwa akisema anamuunga mkono Magufuli kwa juhudi zake za kupambana na ufasadi lakini analaani kitendo chake cha kuminya Demokrasia na ndiyo msimamo wa chama cha ACT, tunaamini Mapambano aliyoanzisha Magufuli kuhusu ufisadi ni ya heli lakini asiminye Demokrasia maana kupitia hiyo atazidi kugundua na kuyapata mengi sana, Zitto si wa kwanza kumsifu Kikwete Mbunge wa kwanza tena alitamka bungeni alikuwa Peter Msigwa, ila naona mnagusa penye effect, mmeamua kumuandama Zitto.