Zitto na Kikwete, Gwajima na Magufuli!

Zitto na Kikwete, Gwajima na Magufuli!

Ninakubaliana na wewe kuhusu fitina ndani ya CCM.

Rais Magufuli hazifahamu fitina za kisiasa ndani ya CCM kwa sababu hakuwahi kwa muda mrefu kuwa hata Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Taifa.

Rais Magufuli ameanza kuingia Kamati Kuu baada ya kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.

Nadhani kutofahamu fitina ndani ya CCM kunamsaidia katika kazi zake za Urais kwa sababu anakuwa hana uhusiano wa karibu na wapiga majungu walioko ndani ya CCM.
Lakini pia akitaka kujua fitina za ndani ya ccm hashindwi,si unajua Rais ni taasisi??Kwani unafikiri wale TISS hawapo ndani ya CC ya ccm??
 
Ila Magufuli yupo tofauti na dhana zote anazoundiwa.mti wenye matunda kweli hupigwa mawe!Magufuli kwa tactics zake hawatamuweza wataumia wao.wanachotaka kukifanya ni kumdhoofisha magu ila jamaa ni heart of lion.

My take:
Tusikubali kuburuzwa na hawa wanasiasa uchwara wameshaona akili za watz za kuchezea kamari zao
Inawezekana wewe na mimi hatuwezi kukubali kuburuzwa kwa sababu tuna uwezo kifikra na tunaweza kuyaangalia masuala kwa kutumia 3D thinking.

Historia inabainisha kuna kundi kubwa wa wananchi ambao kwa siku za karibuni wanaitwa ''nyumbu'' kutokana na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. Hawa ndiyo mtaji mkubwa wa wanasiasa ambao ni wanafiki.
 
Hapa muheshimiwa Mbowe,anasubiria muda ufike abadili gia ardhini
Mbowe ni mzuri sana katika kuzicheza siasa za Tanzania kwa maana nyingine ninaweza kusema, mbowe ni mjasiliamali mzuri wa kisiasa nchini.
 
Kiukweli pamoja na Zitto sometimes kusimamia mambo ya msingi lakini mihemuko yake inayopitiliza kipindi hiki imetufanya wengine tupige hatua nyuma kujiuliza! JPM afanyi jambo bila nguvu ya " system" ambayo hakuna anayeweza kushindana nayo. Kwenye hili kama Zitto ataendelea na mwendo huu bila kuchunga vyema kauli zake zitampoteza kwenye siasa. Tetesi za kutumika na kundi la mstaafu zinazidi kupaa kwenye corridor za kisiasa.

hakunaga system nchi hii huwa mnajisanganya tu.
 
Napata shida sana kuwaelewa wanasiasa ambao wakati wa kampeni za kutafuta uongozi walituaminisha kwamba wakichaguliwa watatetea wananchi na kusimamia kwa nguvu zote upatikanaji wa maendeleo yao. Haya tunayoyaona yakifanywa na wabunge bungeni na mitaani yana uhusiano gani na maendeleo wanayotaka wananchi?

Tunawaomba wabunge na wanasiasa wote wawe na huruma na wananchi. Tunawaomba wawe na uzalendo waangalie vitendo vyao vinaipeleka wapi Tanzania?

Wananchi tumepiga kura tumewachagua viongozi tukiwa na mategemeo makubwa kwao kwamba baada ya uchaguzi kwisha wabunge kutoka vyama vyote na viongozi wote kwa ujumla wao wataelekeza nguvu zao kushughulikia maendeleo ya wananchi.

Lakini tunachokiona sicho kabisa. Rais Magufuli tangu kwenye kampeni na baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wetu ameonyesha nia ya dhati kabisa ya kutaka kuwasaidia wananchi. Hakuna wakati wowote ambao ameonyesha dalili za kurudi nyuma katika azma yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Hawa wanaopinga juhudi zake wana nia gani hasa?
 
Hivi kwanini ni Zitto tu na si Mbowe, kwani Mbowe anayoyafanya kule Mwanza sio kupingana na Magufuli??? kwanini Zitto aonekane ni kikwazo kwa Magu na si Mbowe??? napata ki harufu fulani hivi kinaniijia!
Ki harufu gani unachokipata?

Nipashe nami hicho ki harufu!
 
Mimi Gwajima ni Rafiki yangu tena sana. Ni kama Ndugu. Na hata harakati zangu za Siasa zilipiga kasi zaidi Pale Gwajima alipoitwa kuhojiwa na polisi kwa uonevu mkubwa kwa sababu za Kisiasa. Lakini pamoja na kuwa Askofu Gwajima anachomsifia Mh. Magufuli yaani kupambana na Ufisadi, ufujaji na uzembe, hata mimi nampendea Magufuli hicho hicho. Kufanana kwetu kimtazamo kunaishia hapo. Magufuli amekuwa Dictator kinyume na Demokrasia bila sababu. Udictator ni sawa na Ukoloni, N1 hatari kuliko ufisadi au kitu chochote. Naombeni sasa Viongozi wakuu was Dini, Maaskofu na Wazee wa Kuheshimika Mwiteni Magufuli mumshauri kuwa Udictator anaofanya ni usaliti kwa UHURU wa nchi yetu, Na mwisho utakuwa ni Usaliti kwa juhudi zake mwenyewe za Kuibadilisha nchi yetu ili iwe bora zaidi. Huwa nimejiuliza au ndio maana alizifuta sherehe za Uhuru?
 
Japo gwajima hayupo karibu na magufuli
Amemsaidia magufuli kupata picha kamili linaloendelea chini ya kapeti

Maana magufuli fitina za ndani ya ccm haziwez, ye amekaa kufikiria namna ya kuitokomeza Ukawa

Subir achezweshe gwaride na kikwete kupitia kwa Zito
Umegonga msumari.
 
Kiukweli pamoja na Zitto sometimes kusimamia mambo ya msingi lakini mihemuko yake inayopitiliza kipindi hiki imetufanya wengine tupige hatua nyuma kujiuliza! JPM afanyi jambo bila nguvu ya " system" ambayo hakuna anayeweza kushindana nayo. Kwenye hili kama Zitto ataendelea na mwendo huu bila kuchunga vyema kauli zake zitampoteza kwenye siasa. Tetesi za kutumika na kundi la mstaafu zinazidi kupaa kwenye corridor za kisiasa.
Kwa watu wanaofahamu nguvu ya Rais wa Tanzania wanajua huwezi kuweka mayai yote kwenye kapu moja ili upambane naye.

Watu wanaofahamu nguvu ya Rais wa Tanzania huwa wanaweka akiba ya maneno wakati wa kukabiliana naye.

Suala la Zitto kuhusiana na Rais Magufuli halina tofauti na suala la Mbowe lakini ukichunguza utagundua kuwa Mbowe amekuwa mwangalifu sana katika maneno yake kwa sababu anafahamu ukubwa wa madaraka ya Rais na umuhimu wa Rais katika masuala ya kisiasa.

Kauli za Mbowe kuhusu Rais Magufuli zinajenga mazingira ya uwepo wa majadiliano (compromise) kama itahitajika lakini kauli za Zitto zinaashiria mapambano na Rais Magufuli ambayo hayana nafasi ya majadiliano (compromise).
 
Zitto ni kama Mengi tu, huwezi shindana nao ukashinda.
Huu mtifuano, kifo kitaamua.
RIP Mudhihir Mudhihir na yule Mama wa Moshi.
Hii dhana ya kusema huwezi kumshinda Zitto mnaitoa wapi?

Au ni Zitto mwingine aliyepambana na Mbowe mpaka akajikuta akifukuzwa uanachama wa CHADEMA.

Hivi unazifahamu nguvu za Rais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania?

Reginald Mengi ni mfanyabiashara ambaye ni smart na kwa maana hiyo anafahamu nguvu aliyoyanayo Rais wa Tanzania na katika nguvu hiyo huwezi kumsikia akitoa maneno yanayoashiria mpambano na Rais wa Tanzania.
 
The summary of everything you have stated is that our Hon. President Magufuli is in trouble, of his own making, in my opinion. His fight against "dissent/upinzani" was not only unnecessary, but also completely worthless, because no one in a modern era can win against "democracy".

I was very excited when I first learned that he was proving to be our "Messiah" against corruption, but I am now deeply disappointed that he is seemingly gravely obsessed with cracking down on dissent and eager to fulfill his leadership ambition at the expense of past government achievements.

I really hope he will change his strategy, which of course will require a slight change of his leadership style, if you will.
 
Kuna nguvu za kisiasa (political force) zinazopambana kwa kusigana kwa sasa nchini huku cheche zake za kisiasa zikiwapata baadhi ya wananchi wasiofahamu chanzo chake.

Ninaamini kuna wananchi wanashangaa na kujiuliza sababu ya uwepo wa hizi nguvu zinazosigana na matokeo yake.

Mwanasiasa Zitto Kabwe anamwamuru Kiongozi Mkuu wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete amdhibiti Rais Magufuli na anaenda mbali na kudai Rais Magufuli asifikiri Kikwete ni mjinga kwasababu aliruhusu uhuru wa kujieleza katika utawala wake pamoja na kwamba wapinzani walimwita ni Rais dhaifu.

Pastor Josephat Gwajima anamwamuru Rais Magufuli asikubali kudhibitiwa na Kiongozi Mkuu wa CCM, Jakaya Kikwete na kama ataendelea kumdhibiti basi achague mambo mawili ambayo ni kuhama/kuachana na CCM au kuanzisha mchakato wa kuondoa/kubadilisha Ibara ya 46(1-3) inayohusu Kinga dhidi ya madai na mashataka kwa Rais wa Tanzania.

Ukiangalia kwa undani huu msuguano utagundua Zitto na Gwajima ni mawakala wa kisiasa (political agent) ambao wanawakilisha kundi la wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya nchi.

Kwa sasa siasa za Tanzania ziko kwenye mpito na katika mpito huo kuna political consolidation ambayo hatimaye itajenga mwelekeo wa nchi katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania 1977 mwenye rungu la mpito ni Rais wa Tanzania.

Wakati Zitto akiwakilisha kundi linaloathirika kwa sasa kwenye utawala wa Rais Magufuli katika political consolidation. Gwajima anawakilisha kundi lililoathirika na political consolidation wakati wa utawala wa Rais Kikwete.

Kundi ambalo halijaathirika limekaa pembeni linaangalia mwelekeo wa political consolidation na hatima yake.

Katika utawala la Rais Kikwete, Gwajima na kundi lake waliathirika sana nakwa ujumla ninaweza kusema walishindwa vita mpaka wakasambaratika pamoja na kutumia nguvu za pesa na imani za kidini katika mapambano.

Gwajima wa sasa anafahamu madhara ya kupambana na mtu mwenye rungu na kwa maana hiyo kwa sasa inabidi awahi kiti cha mbele kwenye utawala wa Rais Magufuli.

Gwajima bado ana hasira za kushindwa vita na kwa sasa anajaribu kumshawishi Rais Magufuli amsaidie kwa kutumia rungu lake kwa wabaya wake.

Kwa sasa ameibuka Zitto ambaye pia ni wakala mwenye ‘nguvu za kisiasa’. Sifahamu kwa kiwango gani hizi nguvu zake zinaweza kupambana na rungu la Rais Magufuli kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Hata hivyo historia inatuambia ukipambana na Rais wa Tanzania huwezi kushinda vita. Mpito wa kisiasa wa sasa unamwathiri sana Zitto katika nyanja ya kifedha na kisiasa.

Zitto anajinadhibisha ni mpigania demokrasia lakini pia hatuwezi kufahamu walioko nyuma yake wana nguvu ya kifedha kiasi gani na katika nguvu hizo, wataathiri utawala wa Rais Magufuli kwa kiwango gani huku wakimnufaisha Zitto kifedha na kisiasa.

Je, hii vita aliyoanza Zitto kupigana atashinda?

Je, Gwajima atapata kile anachokitafuta kutoka kwa Rais Magufuli?

Muda utatoa majibu kwa sababu muda ni mwalimu mzuri!
Hapo mwisho mwisho ulivyo andika umenikumbusha enzi zile za Hadithi za Pablo Zungu... Itaendelea toleo lijalo........
 
Binafsi sioni mtu ambaye anaweza kupambana na Rais Magufuli akafanikiwa. Jamaa yupo fit sana na hata kama ikibidi waingie ulingoni atawatwanga tu. zile Push Up bado hazijafanya kazi

Una hoja za kitoto sana mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom