MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Kuna nguvu za kisiasa (political force) zinazopambana kwa kusigana kwa sasa nchini huku cheche zake za kisiasa zikiwapata baadhi ya wananchi wasiofahamu chanzo chake.
Ninaamini kuna wananchi wanashangaa na kujiuliza sababu ya uwepo wa hizi nguvu zinazosigana na matokeo yake.
Mwanasiasa Zitto Kabwe anamwamuru Kiongozi Mkuu wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete amdhibiti Rais Magufuli ili ikiwezekana awe ''one term President'' na anaenda mbali zaidi na kudai Rais Magufuli asifikiri Kikwete ni mjinga kwasababu aliruhusu uhuru wa kujieleza katika utawala wake pamoja na kwamba wapinzani walimwita ni Rais dhaifu.
Pastor Josephat Gwajima anamwamuru Rais Magufuli asikubali kudhibitiwa na Kiongozi Mkuu wa CCM, Jakaya Kikwete na kama ataendelea kumdhibiti basi achague mambo mawili ambayo ni kuhama/kuachana na CCM au kuanzisha mchakato wa kuondoa/kubadilisha Ibara ya 46(1-3) inayohusu Kinga dhidi ya madai na mashataka kwa Rais wa Tanzania.
Ukiangalia kwa undani huu msuguano utagundua Zitto na Gwajima ni mawakala wa kisiasa (political agent) ambao wanawakilisha kundi la wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya nchi.
Kwa sasa siasa za Tanzania ziko kwenye mpito na katika mpito huo kuna political consolidation ambayo hatimaye itajenga mwelekeo wa nchi katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania 1977 mwenye rungu la mpito ni Rais wa Tanzania.
Wakati Zitto akiwakilisha kundi linaloathirika kwa sasa kwenye utawala wa Rais Magufuli katika political consolidation. Gwajima anawakilisha kundi lililoathirika na political consolidation wakati wa utawala wa Rais Kikwete.
Kundi ambalo halijaathirika limekaa pembeni linaangalia mwelekeo wa political consolidation na hatima yake.
Katika utawala la Rais Kikwete, Gwajima na kundi lake waliathirika sana nakwa ujumla ninaweza kusema walishindwa vita mpaka wakasambaratika pamoja na kutumia nguvu za pesa na imani za kidini katika mapambano.
Gwajima wa sasa anafahamu madhara ya kupambana na mtu mwenye rungu na kwa maana hiyo kwa sasa inabidi awahi kiti cha mbele kwenye utawala wa Rais Magufuli.
Gwajima bado ana hasira za kushindwa vita na kwa sasa anajaribu kumshawishi Rais Magufuli amsaidie kwa kutumia rungu lake kwa wabaya wake.
Kwa sasa ameibuka Zitto ambaye pia ni wakala mwenye ‘nguvu za kisiasa’. Sifahamu kwa kiwango gani hizi nguvu zake zinaweza kupambana na rungu la Rais Magufuli kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Hata hivyo historia inatuambia ukipambana na Rais wa Tanzania huwezi kushinda vita. Mpito wa kisiasa wa sasa unamwathiri sana Zitto katika nyanja ya kifedha na kisiasa.
Zitto anajinadhibisha ni mpigania demokrasia lakini pia hatuwezi kufahamu walioko nyuma yake wana nguvu ya kifedha kiasi gani na katika nguvu hizo, wataathiri utawala wa Rais Magufuli kwa kiwango gani huku wakimnufaisha Zitto kifedha na kisiasa.
Je, hii vita aliyoanza Zitto kupigana atashinda?
Je, Gwajima atapata kile anachokitafuta kutoka kwa Rais Magufuli?
Muda utatoa majibu kwa sababu muda ni mwalimu mzuri!