Zitto: Kwanini Mama Rwakatare haagwi Bungeni kwa mujibu wa Kanuni za Bunge? Kwanini azikwe na Serikali kama hajafa kwa COVID19?

Itasaidia kwa wale aliokuwa na marehemu kabla hajafa bwana
 
Kwani Utaratibu wa mbunge anapofariki ukoje?
 
Nadhani tulikwishaambiwa kuwa marehemu wote waliofariki kwa Covid 19, watazikwa na Serikali. Hivyo kioindi hiki ukiona marehemu anzikwa na Serikali maana yake ni kuwa amefariki kwa Covid 19.

Lakini sina uhakika - Marehemu Rwakatare atazikwa na Serikali?
 
Haa haa just haa haa

Manispaa washafukia kitambo sana. Kudhibiti Maumbukizi.

Nakuelewa mhe, ZITTO ila nakuomba sana, usipige zauso, piga hizi hizi za mbavu lazima wakae.
..
 
Ujumbe mjaarabu huo aliutoa Rais wa Amerika Miaka hiyo! Unatufundisha mambo mengi hasa kuwa mkweli. Wakati wa Crisis kuwa mkweli ni jambo muhimu sana.

Ona sasa nasikia kazikwa leo na serikali hata waumini wake hawaja ruhusiwa kumuaga! Akili za kudanganywa usichanganye na zako.

Aidha kanuni za watunga sheria zina taka akikufa mmoja miongoni mwao basi sharti mwili wake upelekwe akaagwe huko. Haja pelekwa!! Kwanini? Tatizo ni kubwa ji-lockdown mwenyewe.

Ukisema ukweli watu watajua ukubwa wa tatizo.

Jamani nimeamua naanza lockdown yangu na wanangu basi. Msiwategemee katika hili janga hili.
 
Kwa tweet hii nimeamini Mh. Zitto anatatizo kubwa sana na uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…