Zitto: Kwanini Mama Rwakatare haagwi Bungeni kwa mujibu wa Kanuni za Bunge? Kwanini azikwe na Serikali kama hajafa kwa COVID19?

Mh. Zitto tafadhali naomba tuheshimu maamuzi yoyote yaliofanywa na serikali au familia inapokuja swala la misiba.

Haina haja ya kuhoji, tuheshimu familia ya marehemu, tumuombee marehemu na wanafamilia wapate nguvu wakati huu mgumu wanaopitia.

Hoja yako haitabadilisha kitu, hata kama kafariki kwa Corona na ikatangazwa itakusaidia nini?

Pumzika Mama Rwakatare na poleni wafiwa.
Itasaidia kwa wale aliokuwa na marehemu kabla hajafa bwana
 
Mh. Zitto tafadhali naomba tuheshimu maamuzi yoyote yaliofanywa na serikali au familia inapokuja swala la misiba.

Haina haja ya kuhoji, tuheshimu familia ya marehemu, tumuombee marehemu na wanafamilia wapate nguvu wakati huu mgumu wanaopitia.

Hoja yako haitabadilisha kitu, hata kama kafariki kwa Corona na ikatangazwa itakusaidia nini?

Pumzika Mama Rwakatare na poleni wafiwa.
Kwani Utaratibu wa mbunge anapofariki ukoje?
 
Nadhani tulikwishaambiwa kuwa marehemu wote waliofariki kwa Covid 19, watazikwa na Serikali. Hivyo kioindi hiki ukiona marehemu anzikwa na Serikali maana yake ni kuwa amefariki kwa Covid 19.

Lakini sina uhakika - Marehemu Rwakatare atazikwa na Serikali?
 
Haa haa just haa haa

Manispaa washafukia kitambo sana. Kudhibiti Maumbukizi.

Nakuelewa mhe, ZITTO ila nakuomba sana, usipige zauso, piga hizi hizi za mbavu lazima wakae.
..
 
Ujumbe mjaarabu huo aliutoa Rais wa Amerika Miaka hiyo! Unatufundisha mambo mengi hasa kuwa mkweli. Wakati wa Crisis kuwa mkweli ni jambo muhimu sana.

Ona sasa nasikia kazikwa leo na serikali hata waumini wake hawaja ruhusiwa kumuaga! Akili za kudanganywa usichanganye na zako.

Aidha kanuni za watunga sheria zina taka akikufa mmoja miongoni mwao basi sharti mwili wake upelekwe akaagwe huko. Haja pelekwa!! Kwanini? Tatizo ni kubwa ji-lockdown mwenyewe.

Ukisema ukweli watu watajua ukubwa wa tatizo.

Jamani nimeamua naanza lockdown yangu na wanangu basi. Msiwategemee katika hili janga hili.
 
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Mbunge akifariki Dunia analetwa ndani ya Bunge na kuagwa. Hata Mbunge awe amefariki akiwa nje ya Nchi huletwa Bungeni. Mbunge Mama G Lwakatare ( Mungu amrehemu ) anazikwa na Serikali na hataagwa na Wabunge wenzake. Serikali inasema SIO #COVID19TZA

Kwa tweet hii nimeamini Mh. Zitto anatatizo kubwa sana na uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana.
 
39 Reactions
Reply
Back
Top Bottom