Zitto kuwasilisha hoja J3 wamo wabunge watano wa CCM

Wabunge wa CCM waliweka saini zao kwenye orodha ya ZIto ni mashujaa ambao ingawa wako kwenye chama cha mafisadi wamedhirisha kuwa wao si mafisadi. Na hii iwe ni heshima kwao na heshima kwa wale walio wachagua kule majimboni. Tunajua mambo ya ccm yalivyo kuwa wabunge hawa huenda wakasubuliwa na pengine hata kuvuliwa uanachama kwa vile watakuwa wamekiuka misingi ya chama hicho ya kilindana hata katika mambo yasiyofaaa.
nionavyo ni kuwa wao wasiogope kwa kuwa wamejionesha kuwa wao ni wabunge wa wananchi na bahati nzuri wananchi wao wamewaona. Wote tumewaona kama wakitokea kusumbuliwa wajue kuwa watakuwa wanasumbuliwa ni wapiga kura wao. wasiogope. TUNAWAPENDA NA TUNAWAPA BIG UP.
Mbunge wangu wa Iramba mashariki, Salome D. Mwambu [CCM] hajasaini!. Ngoja niandae mikutano mikubwa jimboni ya kumshitaki kwa umma. Lazima kieleweke.
 
yah ki ukweli hao ni wapenda mabadiliko, hawaburuzwi na chama, big up. weken majina yao
 
yah ki ukweli hao ni wapenda mabadiliko, hawaburuzwi na chama, big up. Weken majina yao
1. Ni mheshimiwa deo fiklikunjombe
2. Ni mheshimiwa kangi lugora
3. Ni mheshimiwa issa keisy
4.
5.
N.k.
 
Si kutegemea kama Lugora ni jembe la ukweli kiasi hicho. Huo ndo uzuri wa kupata ubunge ukiwa umejiweza ki-maslahi. Hebu watu wa Mwibara wekeni hapa wasifu wa mh. Lugora watu wamjue. Keisy naye kajipambanua vizuri CDM kama mna kesi na huyu jamaa hebu ifuteni na mkaribisheni kwenye chama la watu!
 
Licha ya kuwapo kwa fununu ya mawaziri kujiuzulu lakini Zitto amesema azima ya kuwasilisha hoja yake Jumatatu iko pale pale.

"Spika hajasema kitu, wamejipanga tu hawa, sisi hatujampelekea hoja yetu tunampelekea Jumatatu kisha ataamua. Ili mradi iwe siku 14 kabla ya siku ya kutoa hoja. Wanaweweseka tu," alidai Zitto.

Hadi jana jioni sahihi 75 zikiwemo 5 za wabunge wa CCM zilikuwa zimeshapatikana.

Majina ya wabunge wa CCM waliotia sahihi ni,

1. Deo Philikunjombe wa Ludewa,
2. Ally Keissy Mohamed wa Nkasi Kaskazini,
3. Alphaxard Kange Lugola wa Jimbo la Bunda,
4. Murtaza Ally Mangungu na
5. mbunge mmoja wa Viti Maalumu(CCM) kutoka Kanda ya Ziwa ambaye hakutaka atajwe kwa sasa.

Source: Gazeti la Mwananchi.

Point of correction:

Lugola ni mbunge Jimbo la Mwibala na Mangungu ni mbunge Jimbo la Kilwa Kaskazini!!
 
inaombwa orodha ya mbunge ambao walitia saini zao ili mbivu na mbichi zao zaandaliwe tangu sasa
 
Sasa mbona sioni sign ya Zambi au zilikuwa kelele za bure.
Alafu Sitta na Mwakyembe vip ndo mnatutosa?au bse ni mawaziri
 
Licha ya kuwapo kwa fununu ya mawaziri kujiuzulu lakini Zitto amesema azima ya kuwasilisha hoja yake Jumatatu iko pale pale.

"Spika hajasema kitu, wamejipanga tu hawa, sisi hatujampelekea hoja yetu tunampelekea Jumatatu kisha ataamua. Ili mradi iwe siku 14 kabla ya siku ya kutoa hoja. Wanaweweseka tu," alidai Zitto.

Hadi jana jioni sahihi 75 zikiwemo 5 za wabunge wa CCM zilikuwa zimeshapatikana.

Majina ya wabunge wa CCM waliotia sahihi ni,

1. Deo Philikunjombe wa Ludewa,
2. Ally Keissy Mohamed wa Nkasi Kaskazini,
3. Alphaxard Kange Lugola wa Jimbo la Bunda,
4. Murtaza Ally Mangungu na
5. mbunge mmoja wa Viti Maalumu(CCM) kutoka Kanda ya Ziwa ambaye hakutaka atajwe kwa sasa.

Source: Gazeti la Mwananchi.

Point of correction:

Lugola ni mbunge Jimbo la Mwibala na Mangungu ni mbunge Jimbo la Kilwa Kaskazini!!
 
CCM kuna wabunge wa aina mbili, wapo wanao rely heavily kwenye chama kwa ajili ya kupata jimbo. Yaani kwa kifupi wao wanabebwa na chama tu kwenye eneo husika. Na pia wapo wabunge ambao wanapendwa wao kama wao.
 
Zama za kufichana zimekwisha. Napendekeza wananchi wa Ludewa mumuunge mkono Mbunge wenu kwa kuonyesha ujasiri wa hali ya juu sana. Ni viongozi wachache sana wenye ujasiri huo wa kuweka maslahi ya taifa mbele na hata amediriki kuweka rehani si ubunge wake tu kupitia chama chake bali pia maisha yake na familia yake kwa ujumla maana hawa jamaa wapo radhi kutoa roho ya mtu ili wabaki madarakani.
 
Tunaomba Zito atupe majibu ya wabunge wafuatao alipowafuata kutaka saini zao:
1. Edward Lowasa
2. Ole Sendeka
3. Anna Kilango
4. Serukamba
5. Idd Azan
6. Lembeli
7. John Cheyo
8.Hamadi Rashid
9. Godfey Zambi

Ongeza list kwa wabunge wote wanaovaa ngozi ya kondoo
 
hawa jamaa watalindana tu lakini watanzania tumeshaujua ukweli nani ni nani ccm wanabebana wote mafisadi na wamepita kwa fedha za kifisadi tuwape pole mwisho wao unazidi kukaribia:bump2::bump2::bump2::bump2:
 
Kwa mwendo huu, mafisi wa ahadi hawatakuwa na chao 2015. Nilitegemea Six, Kilango na sendeka wangeuwa kwanza kusaini kumbe wale si majembe ni wembe wa kukata huku na huku
 
Back
Top Bottom