Zitto kufukuzwa CHADEMA siku chache zijazo

Zitto kufukuzwa CHADEMA siku chache zijazo

Wakiongea katika vijiwe vya ujiji na mwanga wamesema kuwa wanasubiria maamuzi ya kamati kuu kwa hamu kuwa siku hiyo ya ijumaa, "tunachosubiria ni kumrejeshea zitto nafasi zake zote ndani ya chama na endapo watamfukuza chama basi hatutaweza kuendelea kubaki ndani ya Chadema tutmfuata Zitto chama chochote atakachohamia" walisema wakazi hao wa kigoma.

Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya mtu na chama chake maana mafanikio ya mtu mmoja mmoja ndani ya chama huleta sifa kwa chama chote, matamsha au vitendo visivyofaa vya mtu mmoja, vinaweza kuchafua chama kwa ujumla wake!

Ikithibitika kuwa, mtu amefanya makosa, ni kosa kubwa sana kumuonea aibu mtu huyo, bila kujali nafasi yeyote ile aliyonayo ndani ya chama chake, kama mtu huyo amefanya kosa linaloweza kukiangamiza chama anachokitumikia, bila kuchukuliwa hatua. Mafanikio ya mtu na heshima aliyojijengea ni lazima viendane na matakwa na katiba ya chama anachokitumikia na siyo kutumia chama chake kwa maslahi yake binafsi. Vyama si vya watu fulani fulani, ni vya wanachama wote.
 
Wakiongea katika vijiwe vya ujiji na mwanga wamesema kuwa wanasubiria maamuzi ya kamati kuu kwa hamu kuwa siku hiyo ya ijumaa, "tunachosubiria ni kumrejeshea zitto nafasi zake zote ndani ya chama na endapo watamfukuza chama basi hatutaweza kuendelea kubaki ndani ya Chadema tutmfuata Zitto chama chochote atakachohamia" walisema wakazi hao wa kigoma.
sio wote sisi wengine tutabaki chadema maana tunachotufanya tuwe chadema ni sera zake sio Zito,tunajua zitto ataamia ccm nyinyi mfateni huko mkazame pamoja
 
Inategemea na "vijiwe" wanavyokalia...kama vipo hivi ...^... watagea nini!!?
 
Mkuu wamesema popote..

Vipi mkutano wa Tabora Zitto alihutubia? Naapa kwamba watakaomfuata Zitto ni hao wanywa kahawa wa vijiweni. Mbona zitto anatambia hapo ujiji na si jimboni kwake kigoma kaskazini na ikumbukwe hao wana wa ujiji mbunge wao ni Serukamba wa CCM so watamfuata vipi zitto wakati si mbunge wao?
 
Mh ZZK ni mamluki ndani ya CHADEMA. Intelijensia ya CDM ipongezwe kwa kazi kubwa waliyoifanya. Wapo viongozi wengi wa upinzani waliofukuzwa au kunyang'anywa vyeo vyao,hawakuwahi kuonewa huruma na CCM,kwa nini ZZK? Mh S Wasira amesahau kiapo/ahadi kuiua CDM kabla ya 2013 kuisha? Zitto nje ya CDM ni samaki nje ya maji. Kama atafukuzwa CDM(tegemeo la wengi)atakwenda mahakamani,kama madiwani wa Arusha. Tutakuwa na mbunge wa mahakama.
HERI YA MWAKA MPYA 2014!!
 
Anayedhani watanzania huchagua chama na si mtu wanajiongopea, mwaka 2005 watu walimchaguga JK na si CCM, mwaka 2010 watu walimpenda Slaa na si Chadema. KWANI CHAMA NDO DUBWANA GANI?, MTU KWANZA CHAMA BAADAE!
Hawa ndio washauri wa Zitto wanaomvimbisha kichwa na yeye anaingia kichwa kichwa.
 
umekisoma kisa cha WAMBURA , aliyetoroka jela kupitia njia ya jeneza ?
Nimekisoma, Zitto na Mwigulu walikuwa wanamtegemea Nchimbi afungue jeneza lakini wameduwaa kukuta yeye ndiye katangulia ndani ya jeneza.
 
Ndugu zangu watanzania wenzangu,awali ya yote napenda kumshukuru M/MUNGU wa rehema kwa uzima na afya njema. Kwa habari za uhakika zlzonfikia hv punde kutoka makao makuu ya CHADEMA,kamati kuu itawahoji watajwa hapo juu na hatima yao ndani ya chama itajulikana ijumaa ikiwa ni maamzi ya pili baada ya kuwavua nyazifa zao.Aidha habari za ndani zinasema Zitto Zuberi Kabwe na Mwigamba Samson watafukuzwa rasmi na kupokwa uwanachama.Ukimya wa Kitila umekuwa silaha yake ya kujilinda dhidi ya maamzi haya mhimu na endelevu kwa chama.
 
Timua wasariti woooooteee cdm hakuna aliyejuu ya sheria, tena akiachwa atasumbua sana na taswirw ya chama itabadilika sana
 
Acha afukuzwe alikuwa miongoni mwa role model wangu kwa masuala ya siasa ametuabisha vijana wasomi na hata ambao sio wasomi.tanzania kwanza ana hammer na bilioni nyingi kwenye akaunti akafundishe sayansi kimu na sio siasa
 
ukabila auto wafikisha popote zitto achukuwi posho atakuwa kiongozi bora
 
Achukui posho bali anachukua posho ya kubomoa chama, sisi wana ccm tunataka upinzani uwepo maendeleo yawepo
 
Back
Top Bottom