Mchome akalia kuti kavu CHADEMA

Mchome akalia kuti kavu CHADEMA

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
562
Reaction score
522
26 Agosti 2026

Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Lembrus Mchome, anadaiwa kukabiliwa na hatua zaidi za kinidhamu ndani ya chama hicho, baada ya viongozi kujadili uwezekano wa kumvua uanachama.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama, Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, alijadili suala hilo na Samwel Welwel, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini.

Mchome, ambaye awali alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, aliondolewa katika nafasi hiyo na uongozi wa chama, huku akidaiwa kukosoa mwenendo wa chama na kutuhumiwa kutumika na Serikali.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa Golugwa alimwelekeza Welwel kuandaa barua inayoeleza mchakato uliotumika kumuondoa Mchome kwenye nafasi ya uenyekiti, ili kubaini kama taratibu zilifuatwa na, endapo zilikuwa halali, kuendelea na hatua nyingine za kinidhamu zinazoweza kufikia kuvuliwa uanachama.

Hatua hiyo inadaiwa kuchochewa zaidi na kauli za Mchome za hivi karibuni, ambapo alihoji hadharani sababu za Tundu Lissu kuendelea kukabiliwa na kesi ya uhaini huku John Heche akiwa huru, licha ya madai kwamba amewahi kutoa kauli zinazofanana.

Katika mazungumzo hayo, Golugwa anadaiwa kusema:

“Tusipomchukulia hatua Mchome, ataonekana ni untouchable, na wataendelea kuongezeka watu wengine wa aina hiyo.”

Kwa upande wake, Welwel anadaiwa kusema hatua zitachukuliwa kwa utaratibu uliowahi kutumika katika suala la Odello, ambapo ngazi ya Mkoa iliwataka viongozi wa Tawi kusimamia hatua zaidi za kinidhamu.

Hata hivyo, hadi wakati wa kuchapishwa kwa taarifa hii, Chanzo chetu kinaonesha hakuna tamko rasmi la CHADEMA lililothibitisha kwamba Mchome amevuliwa au yuko katika hatua ya mwisho ya kuvuliwa uanachama.

Soma

1787738584690.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom