Zitto, Kitila na Mwigamba wajisalimisha CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Nadhani huyu alikuwa ni Zitto ambaye hajavurugwa, baadae wakamtia ndani ya kumi na nane zao, chezea briefcase nyekundu ilijaa note!!
"Kauli ya Chacha Wangwe na baadhi ya Viongozi wa Chadema Kwamba Kuna Mgogoro (CHADEMA) Si ya Kweli, Kwani hali ni Shwari ila haya ni Mageuzi ya Kawaida katika Vyama vya Siasa, hasa inapoonekana Kuna Watu Wanakwenda Kinyume Cha Maadili na Madaraka Waliyonayo ......"

(Hii ni Kauli ya Zitto Kabwe aliyoitoa Mjini Tanga, tarehe 5.7.2008 akitetea Uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema Kumvua Madaraka aliye Kuwa Makamu Mwenyekiti (T) Marehemu Chacha Wangwe"
 
Unafiki wa chadema kwa hiyo kila kitu mnakiweka hadharani?
Hivi akina Zitto wakiamua kuweka kila jambo uchi mtabaki salama?

Acha kujifundisha ujinga wewe!!!
Kuropoka kote kwenye media waliacha nini? hawakupata tuhuma dhidi ya uongozi uliopo ndiyo maana wamesaidiwa na ccm kuunda uwongo!!
Kama Zitto mjanja wakati anasema chama hiki kimemtoa mbali angeongezea kuwa hata ada za chuo alilipiwa na Mbowe!

Zitto kwa usaliti wote ule akosamehewa nitawashangaa sana chadema
 
Nitafurahi sana akifukuzwa lakini kwakuwa ubavu huo hamna kamwe hamtoweza.
 
Huo ni uzushi zitto hajaomba msamaha mnazidisha uongo ili kujipa moyo na kutafuta la kuongea,chadema kimekwisha huu ndio mwaka wao wa mwisho,mnakikuuuza lkn wapi uroho wa madaraka kwa mwenyekiti,ukabila undugu na udini ndio sera za mbowe na chama chake.

barua imekabidhiwa kwako kwanini ccm hamtaki kukubali kudhindwa..
 
Hamuwezi kumfukuza nyinyi Wachaga,Na me naombea mumfukuze tuwe na ya kusema,wakanda wakubwa kudadadeki!!!Chama kinaniuma hiki ningekuwa na uwezo ningekifuta.Yan kila kitu wao Ukabila ,Ukanda ,Udini,Ulaghai.
 
Nitafurahi sana akifukuzwa lakini kwakuwa ubavu huo hamna kamwe hamtoweza.

Zitto asipofukuzwa nitasikitika sana.............. Unless akiri usaliti wake wote alioufanya ikiwemo kupoteza maisha ya watu, alivyoshiriki kuunda uhuni dhidi ya Lwakatare kwa kumtengeneza Dennis Msaki na Ludovic kama karata ya ushindi nk.
 
Hatuwataki CHADEMA..., warudi kwa mabwana zao CCM, wakawaambie kuwa kazi waliyotumwa wameshtukiwa, CDM hatudanganyiki.

Si wanapita huku na huko kutangaza Chadema ni chama cha Wachaga na Wakristo? Mbona hawatuelezi Chadema kimeacha lini huo uchaga na ukristo?

Si wamewatuma wahuni kwenda Kigoma kuvuruga mikutano na ziara ya Dr Slaa?

Watoke hadharani wakiri usaliti wao kwanza ndiyo waombe Radhi.
 
Hamuwezi kumfukuza nyinyi Wachaga,Na me naombea mumfukuze tuwe na ya kusema,wakanda wakubwa kudadadeki!!!Chama kinaniuma hiki ningekuwa na uwezo ningekifuta.Yan kila kitu wao Ukabila ,Ukanda ,Udini,Ulaghai.
"Nothing is more terrible than to see ignorance in action." (Johaan Wolfgang Von Goethe)
 
Hili ndio tatizo kubwa la Chadema, hakuna nidhamu ktk ofisi pale HQ, Nyaraka za kiofisi maelezo yake yanawekwa mtandaoni. Kila anayekiona kitu ofisini saa hiyohiyo anajifanya mjanja wa kuwahi kubandika mtandaoni na viongozi hawaoni madhara yake. Hakuna siri kila mtu ni msemaji wa Chama. Maana yake record office ya chama ina makanjanja wasio na ethics. ndio maana siri nyingi za chama zinavuja.
 
Unafiki wa chadema kwa hiyo kila kitu mnakiweka hadharani?
Hivi akina Zitto wakiamua kuweka kila jambo uchi mtabaki salama?[/QUOTE

Kweli wewe ndio mkuu,,ndu! Kwani kuna mtu kawazuia wasiseme wanachokijua?
Chadema hakiendeshwi kwa hisia,Bali kwa uhalisia.
Kwani walichokifanya kina Zitto ni kitu cha kufurahia?
Mbona kuna siri nyingi tu sana za kwao ambazo zilikutwa kwenye ile Computer ya Mwigamba na hazijawekwa bado hadharani?

Unadhani Wasaliti hawa wangekuwa hawajui kilichoko kwenye ile laptop yao si wangejitapa sana?
Wasaliti wote watimuliwe,wakitaka wakaanzishe chama chao,Zitto awe mwenyekiti,Kitila awe katibu.
 
Kwaheri Dr Kitila
Kwaheri Zitto
Kwaheri Mwigamba
Twawafukuzia mbali wasaliti nyie.
 
TAARIFA YA SAMSON MWIGAMBA KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WARAKA WA MKAKATI WA MABADILIKO 2013


Jumatano, 27 Novemba 2013
Jana katika taarifa kwa waandishi wa habari, Mhe. Tundu Lissu na Mhe. John Mnyika waliudanganya umma kuhusu waraka unaohusu Mkakati wa Mabadiliko 2013. Katika maelezo yao waheshimiwa hawa, pamoja na mambo mengine, walidai kuwa waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni feki. Ukweli ni kwamba:


  1. Ninathibitisha kwamba waraka uliosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ni sahihi neno kwa neno kama nilivyousoma katika magazeti ya HabariLeo, Jamhuri na Rai, pamoja na nakala iliyopo Jamii Forum. Ili kuthibitisha kwamba waraka ule ndio wenyewe, nawatumieni ‘soft copy’ kutoka kwenye kompyuta mpakato (laptop) yangu ambako ndiko ulikoibwa na viongozi wa chama baada ya kunipora kwa nguvu laptop yangu Oktoba 25 na kukaa nayo hadi jioni ya Oktoba 28. Naomba kila mtu asome neno kwa neno waraka ninaowapa leo halafu afananishe na ule uliopo kwenye magazeti na kwenye mtandao ili mjiridhishe kama kweli sio wenyewe. Kama Lissu na wenzake wana mpango wa kuuchakachua waraka huu wamekwama!
  2. Waraka huu si wa uhaini wala mapinduzi wala usaliti kama inavyodaiwa na akina Lissu. Huu ni waraka wa kusaka ushindi katika uchaguzi halali ndani ya chama ambao ulikuwa ufanyike Desemba 2013, na ambao sasa umesogezwa mbele.
  3. Napenda ijulikane kwamba wakati wa uchaguzi si jambo la ajabu kuwa kwa wanachama kuwaunga mkono wagombea tofauti. Nimekuwa karibu na Mwenyekiti Mbowe kwa miaka mingi na ninajua kwamba yeye naye anao mkakati tena unaohusisha mbinu haramu za kuhakikisha anammaliza Zitto na yeye kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi huo. Wanaoshiriki mkakati wake ni pamoja na Lema, Lissu na wakurugenzi kadhaa waliopo makao makuu.
  4. Waraka huu ulipaswa kuwa siri ndani ya watu watatu tu (M1, M2 na M3) na haikutarajiwa kwamba ungevuja kwa jamii. Bahati mbaya viongozi wa chama baada ya kuunasa waraka huu kutoka kwenye komputa yangu mpakato (laptop), na baada ya kikao cha Kamati Kuu, waliamua, kwa jazba na bila kutumia busara ya kiuongozi, kuusambaza waraka huo kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuwakomoa na kuwadhalilisha waandaji. Sasa baaada ya kugundua madhara ya waraka huo machoni pa jamii wameamua kuukana. Ni ajabu kwamba wanaukana waraka ambao waliusambaza wenyewe.
  5. Nasisitiza kwamba mambo yaliyopo kwenye waraka ni bayana na dhahiri. Sibahatishi kwa sababu mimi nimefanya kazi makao makuu kama Mhasibu Mkuu hadi Mwezi Aprili 2012. Ni kwa kutambua uozo uliopo katika uongozi wa chama makao makuu niliona umuhimu wa kubadilisha uongozi kwa njia za kidemokrasia ili tukiokoe chama na hatukuwa na nia wala sababu za kuanika haya yote kwenye umma. Kwa sababu za chuki na kukosa busara za kiuongozi huyo anayeitwa Mwanasheria Mkuu akawashauri viongozi wetu kijinga wauanike waraka mbele ya macho ya watanzania. Wangekuwa na akili na busara baada ya yote haya kutokea wangejiuzulu au kuitisha uchaguzi mara moja.
  6. Tunatambua kwamba viongozi wetu wanamchukia Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa siku nyingi sana na wametamani kumfukuza siku nyingi. Hata hivyo, ninawashauri watafute sababu nzuri za kumfukuza uongozi na hata uanachama kwa sababu yeye hahusiki na waraka wetu wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 hata chembe, pamoja na kwamba yeye ndiye alikuwa na bado ndiye mlengwa mkuu, kama atakubali.



Samson Mwigamba (M3)
Arusha
Jumatano, 27 Novemba 2013.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom